Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hii kitu inaumiza we acha tu. Wanapiga hesabu ya msosi sahani sh. 20,000. Bia minimum 3 * 100, maji kilimanjaro, juice..dah!! Acha kabisa..! Ukitoka hapo hata sherehe huiwezi tena...na ukianza maisha ya ndoa mifuko imetoboka kabisa.
nimekulia dar mkuu nitawatoa wapi hao viumbe wa miguu minne
Halafu baada ya muda unasikia mke wako anachepuka aisee!!
Tunakomoana
Usiombe uoe uchagani au umasaini...utajuta kuzaliwa
Kwa gharama ya maisha haya ya sasa hivi ukioa mchaga wa mjini jiandae kutokwa na kitita kama cha milioni 3 kwenda juu...
mie najua mtu alielipiwa mahari Tshs 1,000/= tu. Hiyo ilikuwa ng'ombe wanne na mbuzi tatu za wajomba. Hapo mbuzi ya mama ilipelekwa physically na mablanket na vitenge vitatu. Sio kila familia haijastaarabika kaka
kwetu usukumani ukiwa umeoa kitamaduni unawajibika moja kwa moja kutatua tatizo ukweni kama utahitajika na hapo ndipo utaojulikana kama wewe ni mkwilima magumashi ama wa ukweli.Kwa mzazi ambae anategemea kuwa huyo mkwewe ataendelea kuwa kama mwanae; na kuwajibika kuja na mafurushi ya vyakula wakati anamtembelea. Na hata kusaidia matibabu ama elimu za ndugu na majukumu ya kiafrika. Sidhani kama atadai mahari ya hela nyingi. Roho ya kimaskini tu hiyo, kijana wa watu anakaa nyumba ya kupanga halafu udai mahari milioni mbili?
huu ndio utaratibu wetu. wewe si umeuliza mahari kwetu zikoje? ndo ziko hivi. tena hapo sijakupa mashariti'
1.lazima ng'ombe mmoja awe ana mtoto yaani tayari ana maziwa ili wakifika tu waanze kukamua na kunywa maziwa.
2.lazima ng'ombe wanne wawe makisai ili wakifika tu ukweni wawe na makisai za kulimia.
3.ng'ombe wanajichagulia wenyewe upande wa mke. wewe kazi yako ni kuwaonyesha zizi tu. alafu wanatabia ya kuchagua majike tu yaliyo karibia kupandwa lakini hayajawahi kuzaa ili kwa mfano yakiwa 30 baada ya mwaka majike yote yanazaa na idadi inaongezeka mara dufu.
4.kama ng'ombe huna ila umewanunua mnadani bado watawatathimini ubora wao na wanaweza kuwakataa baadhi kawa hawajaridhika nao. inabidi ukanunue tena
5.na mbuzi wa mjomba lazima,mashangazi nao kuna chao, bibi na babu nao kama kawaida.
karibu usukumani.
huu ni utaratibu tu wala hatumkomoi mtu.
Mkuu sisi si wafugaji,je watu ambao si kabila lenu inakwaje?utaratibu haubadiliki?
hapo inategemea sana na mambo yafuatayo.
1.uelewa wa hao wazazi.
2.uelewa wa msichana.
MNAWEZA KUKUBALIANA IDADI YA NG'OMBE MATHALANI 20 ALAFU UKIWA HUNA ZA KUTEMBEA(REAL CATTLE) BASI MNAWEKA KWENYE THAMANI YA PESA.
UKIAMBIWA NG'OMBE MMOJA WA MAHALI ANA THAMANI YA 300,000. MAANA YAKE NI 300,000X20=6,000,000.
KAMA NI 200,000 MAANA YAKE NI 200,000X20=4,000,000.
hapo taratibu zilizobaki pia bado. kwa maana ya bibi,babu,shangazi na mjomba.
ALAFU KWETU UKIWA BADO HUJATOA MAHALI ILA UMECHUMBIA NIKIJA MIMI NIKATOA MAHALI KUKUSHINDA WEWE BASI NAOA MIMI NA WEWE UNAPIGWA CHINI.
LA SIVYO URUDI HARAKA KABLA JAMAA HAJATOA NA WEWE UPANDISHE MAHALI.
MFANO KAMA MLIKUBALINA NG'OMBE 18, MIMI NIKAJA KESHO YAKE NIKAAHIDI KUTOA 22 HAPO NISHAKUPOKA MCHUMBA. KAMA UNAMTAKA INABIDI URUDI HARAKA SANA UAHIDI ZAIDI YA 22MFANO 25.JAMAA AKIONA ANAMHITAJI SANA HUYO BINTI ANAWEZA KURUDI TENA AKAWEKA 30.
TE TE TE TE TE TE HAPO MPAKA JASHO LITAKUTOKA.
UNLESS UMPATE ANAYEPELEKA MAMBO KISASA KUWA MAPENZI NI MLIOKUBALIANA.
Kwa mtindo huu usukumani hatuoi
Tuambizane basi posa/mahari huwa ni kiasi gasi kwa kabila yenu?maana suala la kuoa huwa huwezi kukwepa utaratibu wa kikabila.
Mnapokea viumbe wanaohema wangapi kama mbuzi, kuku, ng'ombe, kondoo?
Kabila langu dume la ng'ombe mmoja (hata awe mdogo), ndama mmoja,kondoo wawili.
Inavyoonekana wasukuma na wamasai wana dau kubwa,sijui kama wahaya, wangoni, wasambaa, warangi, wambulu,wameru,wanyamwezi,waluguru, wazaramo, wachaga, wapare,wazanaki, wamakonde etc.
Naomba kujua kabila lenu mahari ni kiasi gani,je hao wanaotaka ng'ombe wengi msichana wao akikutana na kijana wa kizaramo(mfano),hiyo rules za mahari hawabadilishi?
...........
kuna majina mengine huezi kuyasikia kwingine zaidi ya wasukuma wanaojua.
KUNA WATU WANAITWA
1.WASUKUMA(WATU WA KASIKAZINI)
2.WADAKAMA(WATU WA KUSINI=WANYAMWEZI)
3.WANANG'WELI(WATU WA MAGHARIBI)
4.WANAKIYA(WATU WA MASHARIKI)
HAWA WOTE COLLECTIVELY NI WASUKUMA.