Kwani mngegomea, mngepungukiwa na nini?

Viongozi wa Upinzani sio kwamba Wana vichwa vigumu hapana,Ni ubinfsi ndio unafanya waonekane Wana vichwa vigumu
 
Sawa.

Wafanye wanavyotaka basi.

Mimi kamwe sitojihangaisha na kupiga kura chini ya haya mazingira. Kamwe daima!

Nyie anzeni kujipanga kwa ajili ya 2025 [emoji1787][emoji1787].
Bila Tume huru au katiba mpya uchaguzi wa mwaka huu ndio ulikuwa wa mwisho mie kupiga kura.
 
Haondoki huyu. Katiba inakwenda badilishwa. Kisingizio ni ili amalizie miradi yake.
Walishasema..... ‘atake asitake’!

Yeye anaweza kujifanya kukataa ila mwisho wa siku by early 2024 atakubali baada ya ‘kuombwa sana’ na wazee na viongozi wa dini. Kagame style!
 
Sawa.

Wafanye wanavyotaka basi.

Mimi kamwe sitojihangaisha na kupiga kura chini ya haya mazingira. Kamwe daima!

Nyie anzeni kujipanga kwa ajili ya 2025 🤣🤣.
Kwa bahati mbaya mimi sio mwanachama wa chama chochote na wala sina mpango wa siasa nilishaona upuuzi tokea zamani.
 
Siyo uchaguzi wa serikali za mitaa tu.

Kama ulikuwepo 2010 na 2015, wapinzani hawa hawa waliyakataa matokeo.

Hawakuwa na imani na tume.

Lakini cha kustaajabisha, huwa wanayakataa matokeo na kusema kuwa tume si huru, lakini muda wa uchaguzi ukifika wanashiriki tena.

Na wanashiriki chini ya mazingira yale yale.

Kama huamini, subiri uone 2025 watafanya nini.

Mimi natabiri kuwa watashiriki tena na itakuwa kwenye mazingira haya haya yaliyopo sasa hivi.

Halafu matokeo yakishatangazwa, watasema hawayatambui.

Tuombeane uzima tu ili tuwepo hiyo 2025 ili tuweze kukumbushana.
 
Kwa bahati mbaya mimi sio mwanachama wa chama chochote na wala sina mpango wa siasa nilishaona upuuzi tokea zamani.
Good for you!

Kuendelea kushiriki chaguzi za maigizo ni uwendawazimu.
 
Wamekosa kila kitu iwe bara au visiwani.sasa wale wa visiwani hawajawai kupata uwakilishi toka walivyosusa wenzao wakala na mwaka huu wameshiriki na wamekosa kila kitu.
 
Asiekubali kushindwa sio mshindani! Kubalini mmepigwa kipigo kitakatifu, msijifariji bure! Laana ya kumkimbatia lowasa kisa vihela na kumuacha Slaa aliyeijenga chadema ikaonekana!
 
Ta
Wamekosa kila kitu iwe bara au visiwani.sasa wale wa visiwani hawajawai kupata uwakilishi toka walivyosusa wenzao wakala na mwaka huu wameshiriki na wamekosa kila kitu.
Tatizo huko visiwani wanataka sultan arudi, ccm hatuwezi kukubali toka tulivyofanya mapinduzi matukufu!
 
Makamanda ni Wajinga sana hawaelewi wanachotaka kabisa hawana long term plan zaidi ya kukurupuka sasa acha wavune walichopanda, walio soma soma watafute kazi za kufanya
 
Ndugu yangu Nyani kugoma sio suluhisho kabisaaaa maana wakina Sipunda na shibuda watashiriki ikiwezekana watapewa na wabunge 10 kila mmoja ili kuonyesha demokrasia ipo kama ilivyokua zanzibar

Nakubaliana na wewe pia kuendelea kushiriki chaguzi kwenye mazingira haya nayo ni sawa na sifuri maana ccm wana means zote za kupora kura

Tunahitaji njia bora zaidi ya kususia.........watasusia cdm labda act tu halafu vyama mamluki 20 vitashiriki, mwisho wa siku chama kitakosa hata uwezo wa kujiendesha au kifutwe kabisa kama ambavyo kimefanyiwa kwenye uchaguzi huu

NGUVU YA UMMA NDIO SULUHISHO PEKEE......AMINI NAKWAMBIA
 
Sawa.

Mimi sijasema kugoma ndo suluhisho pekee au mwarobaini.

Kugoma ni sehemu tu ya harakati. Ni sehemu ya mapambano.

Na ukigoma leo haina maana kesho utapata unachokitaka.

Licha ya hivyo, acha waendelee kushiriki tuone kama watapata chochote kilicho cha maana....

Maana mimi Ngabu ni kilaza tu niliyeishia kidato cha nne. Sina nilijualo.
 
U

Umma upi? je Wa Ccm sio Umma? Maana mashabiki na wanachama wa Ccm ndio wengi zaidi ya vyama pinzani je wa Ccm wakiandamana (nguvu ya Umma) kuunga mkono serikali 😁 au Neno nguvu ya umma ni mali tu ya upinzani?
Kwa muktadha wako huu unadhani watu kama akina Gadafi na wenzake walioondolewa kwa nguvu ya umma unajua walikua na wafuasi kiasi gani?

Umewahi kujiuliza hivi wale uliojua unawaona wanamshangilia lissu kwenye mikutano yake wakiamua kiandamana itakuaje?
 
Nilikuwa Mjinga mwaka huu kushiriki uchaguzi lakini stakuwa Mjinga Tena kushiriki uchaguzi mwingine wowote Kama Mazingira ya uchaguzi Ni hayahaya
 
Nilikuwa Mjinga mwaka huu kushiriki uchaguzi lakini stakuwa Mjinga Tena kushiriki uchaguzi mwingine wowote Kama Mazingira ya uchaguzi Ni hayahaya
2015 na 2010 hukushiriki?

Na ulikuwa hujui kuwa mwenyekiti wa CCM ndo huunda tume ya uchaguzi?
 
Nyani ngabu toka huko USA njoo njoo uishi na sisi hapa Miaka 5(Wala vumbi) ndio tutaelewana

Ukisemea kwa huko hatukuelewi unapiga kelele tu[emoji2][emoji3577]
 
Kuna watu huwa mnaandika vitu ili mradi umeandika tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…