Kwani mngegomea, mngepungukiwa na nini?

Mimi siwalaumu wapinzani hata kidogo.
Nawaona ni washindi.
Kila mtu ana macho anajionea japo watu wa ccm mnajifanya vipofu
 
Mambo mengine mpaka nahisi ni makubwa kuliko akili zenu. Hivi uchaguzi gani ambao hakukuwa na matukio ya kura feki? Mmesahau? Au kwavile zama hizi mitandao imetawala ndio mnafikiri this time ni too much [emoji41].

Tunashauri Chadema ina matatizo from within na hilo pekee linadhoofisha nguvu ya uwezo wa chama kupambana na hujuma kama hizo. Bila determinant leadership hamuwezi hata kuwa na ajenda mtayoisimamia kikamilifu kuwafikisha mnapotaka ikiwemo tume huru ya uchaguzi.

Huu uchaguzi shujaa ni Tundu Lissu, with disorganised party ameweza walau kutoa ushindani ktk mazingira magumu sana. Lazima Chadema wakae chini na wazee, wanachama wajipange upya ikiwemo kuvunja uongozi wote na kupanga safu upya na Lissu apewe uenyekiti kamili.
 
1985-1995 mtarajie kuiona ikijiludia pia msisahau mmeendelea karne ya 20
 
Bila kushiriki uchaguzi huu ingekuwa vigumu sana kuuaminisha ulimwengu kuwa Tanzania hakuna demokrasia. Katika hali ya udikteta ulivyo Tanzania, wananchi wanahitaji msaada wa kimataifa ili kujikwamua hapa tulipo, peke yetu hatuwezi kabisa kupata demokrasia ya kweli.
Hivyo tuvipongeze vyama vya upinzani kwa kushiriki uchaguzi huu. Sasa ni wakati wa kuomba msaada kwa kutoka nchi na jumuia za kimataifa kwa sababu kuna ushahidi wa kutosha wa dhuluma iliyofanywa na serikali hii kwa wananchi wake.
 
Mkuu, posho imetoka?
 
Magufuli ana roho mbaya sijapata kuona. Walimwita JK dhaifu. Kweli Magufuli sasa atakuwa Rais wa maisha ila wananchi wajiandae kulia.
Kinachonichosha ni yeye kuhudhuria ibada na kunyenyekea huku matendo yakiwa tofauti, nadhani Africa unafiki na roho mbaya ni janga letu licha ya kujaa nyumba za ibada, nimeishi na watu hawajui milango ya makanisa Ila Wana utu na upendo Hadi nikaona waenda ibadani ndio mashetani wenyewe
 
Unazungumzia hivyo vyama vya upinzani ambavyo vinapokea na kusimamisha mataga(reject)wa sisiem kama wagombeaji wakuu?
 
Shida sio kuingia barabarani bali shida ni virungu vya ugoko na risasi za moto 😂😂😂! Consequences zinazoambatana na hayo maandamano ndio shida kubwa na hii inazalisha hofu miongonia mwa raia kiasi kwamba huwezi thubutu kuingia front.

Ingelikuwa maandamano yanaheshimiwa nchi hii hata muafaka wa katiba mpya ungelikuwa ushaafikiwa siku nyingi.
 
Mkuu huwa una chuki na upinzani kisa lowasa unasahau hata mstakabali wa taifa lako kwa situation ilivo unaweza laumu upinzani kweli, sie tulioenda kupiga kura Jana tulijionea upumbavu wakiwango Cha lami kiasi hata hao wapinzani unaowasema ungebadili kauli yako. Tutetee masilahi ya nchi yetu na sio kulaumu kitu ambacho upinzani hawawezi badili
 
True but 1995 unamskia Lyatonga analalamika kuibiwa tu na ITV filtered news.

In 2020 unaona live kwenye social media askari na bags za kura feki.

Even a doubting Thomas now believes.
2015 ilikuwa hivi hivi.

2010 ilikuwa hivi hivi.

Na 2020 hakuna tofauti na ilivyokuwa 2015 na 2010.

Seems to me you are just being a prisoner of the moment!
 
Kuna viumbe wanasikitisha Sana hoja zao mfu aisee, that's why ka taifa umaskini hauiishi
 
Hapana!

Hakuna kilicho kipya!

Mazingira ya uchaguzi wa 2020 ndo yale yale ya 2015, 2010, 2005!

Tatizo ni usahaulifu wenu tu.
 
CDM Ina matatizo vipi act wazalendo na uhuni waliofanyiwa?
 
Naona unatetea majambazi wa ccm..
Wangegomea uchaguzi ili iweje?.
Swali kwanini ccm waibe kuraa?.
Kwanini unawashambulia upinzani kosa lao nini?.
Au ndo mahaba niue?
Sawa.

Shirikini na 2025, 2030, 2035....
 
[emoji23][emoji23][emoji23]kirungu Cha ugoko noma sana
 
Hatuhitaji ma Rais, period.

Vyama vinatugawa na kuna uonevu wa waziwazi...

Kuliko kuwa na chama kimoja bora tusiwe navyo kabisa
 
Akili za kushikiwa hizi eti upinzani una matatizo makubwa lakini matatizo ya wafanyakazi, wakulima, wafanyabiashara mabilioni yao huyaoni! Matatizo ya Katiba, Bunge, mahakama na Watanzania kudharauliwa huyaoni! Matatizo ya pesa za walipa kodi kuchotwa hazina kinyemela hadi CAGs kuandika 2.7 trillions zimepotea hazina huyaoni! Matatizo ya uchaguzi uliojaa wizi, vitisho na mauaji ya kutisha huyaoni!
Hebu tuondolee UPUMBAVU wako hapa

 
Kuna mtu kasema hapo juu eti bila upinzani kushiriki uchaguzi huu basi eti ingekuwa ni vigumu kuiaminisha dunia kuwa kuna figisu kwenye chaguzi zetu!

Imagine that!

Sijui hawa watu wengine walikuwa wapi 2015, 2010, 2005 nk!

Sina hakika hata kama wanajua kinachojadiliwa hapa.
 
Hapana mkuu sina chuki na Lowasa. Ila hayo yote si mapya kwenye chaguzi zetu. Hivi kweli unategemea hiyo fairness itatoka mbinguni? Anyway tuendelee kuomba CCM wawe fair [emoji41]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…