Kwani mngegomea, mngepungukiwa na nini?

Na 2025 watashiriki tena katika mazingira haya haya na watategemea kushinda!
 
Kuna sababu nyingi za kushiriki uchaguzi. Kwa uongozi wa sasa kususia uchaguzi ni kosa kubwa kwani kunawanufaisha sana wanasiasa wasiokuwa na uwezo wa kushindana kwa hoja. Faida ya kushiriki ni kubwa sana kuliko kususia uchaguzi.
1. Kampeni ilidhihirisha udhaifu mkubwa wa ccm; hasira hiyo ya kuzidiwa hoja jukwaani ndiyo imepelekea uharamia tunaoshuhudia kama njia ya kujifariji.
2. Pamoja na ubabe wote wagombea wa ccm walilazimika kupiga magoti kuomba kura
3. Watanzania na dunia nzima sasa wanajua ccm hawana uwezo wa kushindana kwenye uchaguzi.
4. Matokeo yanayotangazwa ni hadaa tu kuwa upinzani umefutika wakati kila mtu anajua wameporwa ushindi.
 
Haya, na waendelee kushiriki tu na nyie msiache kupiga kura.
 
Mkuu Nyani Ngabu wazo lako zuri sana hata mm nilikuwa nafikiria hivyo ila shida inakuja ukiachilia mbali ACT na Chadema vile vyama vingine mi naona sio wapinzani wangeshiriki kwakuwa vile vyama viliwahi kulaani Chadema wanatoa kauli za uchochezi
Je kugoma kwa Chadema na ACT tu ingewasaidia ilihali vyama kama TADEA vinashiriki?
 
Hapana!

Hakuna kilicho kipya!

Mazingira ya uchaguzi wa 2020 ndo yale yale ya 2015, 2010, 2005!

Tatizo ni usahaulifu wenu tu.

Mwaka jana wapinzani waligomea uchaguzi serikali za mitaa-kulitokea nini?

Mwaka 1995 waligomea uchaguzi wa marudio Dar-Kitu gani kilifanyika?

Bunge la katiba walisusia-Ilisaidia nini?
 
Tadea hata wakishiriki siwezi kukosa usingizi.

They are a non-factor.

Mimi nazungumzia vyama vinavyo matter.
 
Mwaka jana wapinzani waligomea uchaguzi serikali za mitaa-kulitokea nini?

Mwaka 1995 waligomea uchaguzi wa marudio Dar-Kitu gani kilifanyika?

Bunge la katiba walisusia-Ilisaidia nini?
Kugoma kunapaswa kuwe sustained.

Pia, kunapaswa kuendane na mbinu zinginezo.

Sijasema kugoma kuwe ndo kila kitu.

Hata hivyo, mimi sina akili. Nimeishia kidato cha 4. Ndo maana nabeba maboksi sasa hivi.

Na ndo maana labda ninatoa ushauri wa kizuzu.

Basi ni bora waendelee tu kushiriki hizo chaguzi maana wao na wafuasi wao wana akili kuliko mimi.

Wasubiri 2025 wagombee tena.
 
Kweli bila ya hivyo kugoma labda CHADEMA na ACT tutafute mbinu nyingine ila sio kwa Masanduku ambayo kila kitu wanafanya CCM kuaandaa uchaguzi au tufanye kampeni ikifika uchaguzi tunagoma maana hata ukishiriki wanashinda wao
 
Kweli bila ya hivyo kugoma labda CHADEMA na ACT tutafute mbinu nyingine ila sio kwa Masanduku ambayo kila kitu wanafanya CCM kuaandaa uchaguzi au tufanye kampeni ikifika uchaguzi tunagoma maana hata ukishiriki wanashinda wao

Kushiriki ukafanyiwa uovu ndo unakuwa na proof kuwa ni waovu kweli, otherwise watakugeuzia kibao kuwa hauko serious katika kutafuta ridhaa za wananchi.
 
Unavyo jifanya unajua hebu jaribu kuongoza hata chama chama marehemu Mtikila tukuone, ni rahisi sana kukosoa fanya wewe tuone mfano
 
Kwenye mpangilio wa siasa za vyama vingi nikiangalia kushoto kulia tuna lean towards the rwandan model. Au mnasemaje great thinkers?
 
Hapana mkuu sina chuki na Lowasa. Ila hayo yote si mapya kwenye chaguzi zetu. Hivi kweli unategemea hiyo fairness itatoka mbinguni? Anyway tuendelee kuomba CCM wawe fair [emoji41]
Nope una blame upinzani kwa kitu ambacho Kiko nje ya uwezo wao hasa awamu hii wamepitia machungu mengi so kulaumu wao ni uonevu, Kuna mtu anaweza shindana na mkono wa chuma wa jiwe Jana tu hyo unaenda piga kura wako ccm maboksi yamejaa kura hamna mawakala wengine. Jukumu la kutetea masilahi ya nchi ni letu sote sio kulaumu upinzani na Sasa wamebaki ccm ndio furaha ya wengi
 
Kwangu kushiriki uchaguz ni fursa isiopaswa kuachwa kwa sababu
[emoji3577]Tumekagua uhai wa chama to the grassroots
[emoji3577]Wamemuonesha mtawala vile hakubaliki.
[emoji3577]Wamefungua ufaham wa watu wengi zaid n kuongeza wanachama.
[emoji3577]Wamejenga Imani zaidi kwa watu.
[emoji3577]Wamesikiliza kero za watu.
Mwisho huwez msusia fisi bucha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…