Detective J
JF-Expert Member
- Oct 17, 2016
- 24,058
- 41,518
I think migomo haisaidii. Haisaidii kabisa... wakae wajipange upya kimkakati. Hatakama wamechezewa foul.. lazima wajui wana counter vipi hizo mbinu.Swali kwa wapinzani.
Kwani mngegomea kushiriki haya maigizo ya uchaguzi wa 2020, mngepungukiwa na nini?
Na hivi mlivyoshiriki, mme-gain nini?
Mimi msimamo wangu uko wazi. Unajulikana.
Hakuna kushiriki chaguzi za maigizo ambazo mtu hauhitaji hata uwe genius kujua matokeo yake yatakuwaje.
Kushiriki chaguzi za hivyo, chaguzi za kutimiza wajibu tu, ni umajinuni.
Baadhi yenu mmetaja chaguzi za serikali za mitaa mwaka jana ambapo wapinzani walizisusia.
Kwanza, chaguzi za serikali za mitaa si sawa na uchaguzi mkuu.
Pili, migomo ya kushiriki chaguzi za maigizo ni lazima iwe endelevu.
Kama mwaka jana mligoma na CCM wakajipa ushindi wote, mwaka huu mmeshiriki na mmeambulia nini zaidi ya kipigo cha mbwa?
Zigomeeni hizo chaguzi. Wekeni mashinikizo mpaka zipatikane taasisi zilizo huru za kusimamia na kuendesha chaguzi.
La sivyo, mtaendelea kutegemea hisani ya CCM kupata ushindi.
Na siku mkikutana na jitu lenye roho mbaya, hata hizo nafasi chache mnazoshindaga, mtanyimwa.
Na jinsi mlivyo na vichwa vigumu, si ajabu mkaanza ule upuuzi wenu wa twende na Shangazi 2025.
Bure kabisa.
Target yao kubwa iwe ni katiba katibaa.