Kwani ninyi mnawafanyaga nini wanawake wa aina hii?

Kwani ninyi mnawafanyaga nini wanawake wa aina hii?

Joined
Dec 23, 2021
Posts
56
Reaction score
228
Habari wandugu,

Nimekutana na wanawake kadhaaa lakini sijawah kutana na mwanamke kama huyu ukweli ananipa changamoto sana.

Nimwanamke ambae nimekutana nae somewhere tukabadilishana namba baada ya kumuelewa kiaina. Nikaanza kuanzisha ukaribu nae kwa kuwasiliana nae mara kwa mara na hapo ndo nikakumbana na maswahibu.

Kwanza kabisa mwanamke hakutafuti mpaka wewe ufanye hivyo, pia wakati mnaongea inakuwa kama vile unamfanyia interview yani yeye anakuwa wakuitikia tu na hata ikitokea anaongea basi ni kwa ufupi sana, hii ni kwenye simu pia hata mkiwa live mwendo ni uleule.

Naombeni ushauri wakuu ninyi huwa mnafanya vipi kwa wanawake wa aina hii kwasababu Kuna muda huwa inafikia hatua wote tunakaa kimya tunabaki kuangaliana tu kama mabroiler.
 
kuna mawili bro
either hajakupenda/hana hisia na wewe au anakuogopa/hajakuzoea/sio muongeaji

kati ya haya moja ni jibu na njia ya kufika kwenye jibu ni kumpa muda.
Over am out.
 
images (6).jpg
images (4).jpg
images (3).jpg
 
Ni kawaida... Mkishazoeana ataongea kiasi na akiwa na hasira kama muimba taarabu kisha hasira zikimuisha ataendelea kuwa sio muongeaji sana.

Lakini kuhusu kuchat huenda akawa hivyo hivyo mzoee, utakumbana na magazeti mkitofautiana baada ya hapo hasira zikimuisha atarudi kwenye hali yake.

Jihadhari pia ukimya wake haumaanishi ujinga, unaweza kukumbana na maswali ambayo tayari anaujua ukweli wake anakuwa tu anataka akusikie kama utamwambia ukweli au lah.
 
Back
Top Bottom