Kwanini Abeid Amani Karume alimtimua John Okello "Empty Handed" licha ya kumsaidia kufanya Mapinduzi ya kumtoa Sultan?

Sababu aliogopa kupinduliwa,hii ipo kwa waafrika wote hata Kenyatta alimfunga odinga baba aliyefanikisha uhuru wa Kenya akihofia atamharibia shibe yake
 
Architect wa mapinduzi alikuwa Mwalimu. Ndiyo maana waliotekelezq walitokea Tanga wakishirikiana na Okello.
Mwalim amewahi kuliongekea hili hata kidogo ? Uhusika wake kwenye mapinduzi ? Najua askari wengi walitoka Tanga....wa Zbar walikuwa hata hawawazi ipo siku watapindua na kumkimbiza muarabu.....waliridhika na dhuluma ile....watu weusi tuna kasumba ya uoga??
 
Historia ya Mapinduzi Zanzibar inawezekana imehaririwa Sana kiasi ukweli wake haujulikani vizuri.

Ukweli ulio wazi ni kuwa Mganda John Okello ndiye aliyeongoza Mapinduzi yale ya Januari 12/1964 kwa kushirikia na watanganyika waliokuwa wanaishi Zanzibar.

Kitu kinachonitatiza, hakuna mahali kwa maelezo yake au ya ASP wenyewe, Kuonesha kuwa Okello aliwahi kuwa kiongozi mwandamizi au mwanachama wa kawaida wa ASP.

Jee ASP kupitia Mzee Abeid Karume ndiyo walishrikiana na Okello kufanya yale Mapinduzi au ASP walimpora Okello Mapinduzi aliyofanya bila ya kushirikiana nao?
 
HII MADAA UKITAKA KUJUA HASWAA، MUULIZE MOHAMMES SAID NDIO NGULI WA HISTORIA, ATAKUPA MTIRIRIKO WOOTE,
Yeye ana upande wake. Tunataka mtu atakayeisema historia kama ilivyotokea. Maana jinsi Okello alivyoondolewa Zanzibar, labda kama asingeondolewa, historia ya Zanzibar baada ya mapinduzi isingekuwa hii tuliyo nayo Leo!
 
Historia ya Mapinduzi Zanzibar inawezekana imehaririwa Sana kiasi ukweli wake haujulikani vizuri.

Ukweli ulio wazi ni kuwa Mganda John Okello ndiye aliyeongoza Mapinduzi yale ya Januari 12/1964 kwa kushirikia na watanganyika waliokuwa wanaishi Zanzibar.

Kitu kinachonitatiza, hakuna mahali kwa maelezo yake au ya ASP wenyewe, Kuonesha kuwa Okello aliwahi kuwa kiongozi mwandamizi au mwanachama wa kawaida wa ASP.

Jee ASP kupitia Mzee Abeid Karume ndiyo walishrikiana na Okello kufanya yale Mapinduzi au ASP walimpora Okello Mapinduzi aliyofanya bila ya kushirikiana nao?

Kama Zanzibar kuna Kitu kinaitwa "Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar," Je, kwa nini na Tanganyika napo kusiwe na kitu kinachoitwa kwa jina kama hilo???
 
Ni kinyume , Karume alishirikiana na Nyerere Okello akaitwa Dar kwa ziara, kufika akaambiwa hakuna kukanyaga tena Zanzibar rudi Uganda.
 
Hiyo ni baada ya mapinduzi. Jee kabla ya mapinduzi Okello na Karume waliwahi kupanga pamoja kuhusu kumpindua Sultan?
 
Tatizo Mohamed Said anaegemea upande wa dini zaidi
Yoda,
Mimi nimeandika kitabu: "The Life and Times of Abdulwahid Sykes (1924 - 1968) The Untold Story of the Muslim Struggle Against British Colonialism in Tanganyika," Minerva Press London 1998.

Kilichonisukuma kuandika kitabu hicho ni kule kuona kuwa historia ya uhuru ni historia ya Waislam jinsi walivyopambana na wakoloni kudai uhuru wa Tanganyika wakianza na African Association 1929 kisha wakaunda Al Jamiatul Islammiya fi Tanganyika (Umoja wa Waislam wa Tanganyika) 1933; na 1954 ikaundwa TANU.

Katika historia hiyo hapo juu Waislam walikuwa mstari wa mbele na mchango wao ni mkubwa kupita kiasi.

Bahati nzuri ni kuwa hawa waliofanya haya mimi baadhi yao ni wazee wangu kwa nasaba na wengine kwa ujamaa kwa hiyo ni watu ninaowajua vizuri.

Imeandikwa historia ya TANU na Chuo Cha CCM Kivukoni hawa wazee wangu waliounda African Association, Al Jamiatul Islammiya fi Tanganyika na chama Cha TANU hawamo ndani ya kitabu hicho, "Historia ya TANU," (1981).

Ndipo mimi nikaamua kuandika historia ya TANU na kupigania uhuru wa Tanganyika kama ninavyoijua.

Katika kitabu changu kama jina lake lilivyo nimeeleza mchango wa Waislam.

Ikiwa wewe unaona hili halikustahili kwa kuwa nimewataja Waislam fahamu kuwa wengi wameipenda historia hii kwa kuwa ndiyo historia ya kweli ya ukombozi wa Tanganyika.
 
Jee ASP kupitia Mzee Abeid Karume ndiyo walishrikiana na Okello kufanya yale Mapinduzi au ASP walimpora Okello Mapinduzi aliyofanya bila ya kushirikiana nao?
Soma historia ya Karume huko huko ndipo utapoona Okello alipatikana wapi na waliofanya mapinduzi sio Wanachama wa ASP au UP ni watu kutoka Bara wakipitia Bandari ya Tanga hata Okello mwenyewe alitoka UG ila alipitia Bara kwenda Zanzibar, wafanyakazi wa kwenye mitumbwi na majahazi kutoka Bara ndio waliompindua Mwarabu na Serikali yake mwishoni utagundua Jamshid alikua dhaifu ndio maana walimuweza kumwondoa na kumkimbiza akakimbia
 
Yoda,
Mimi nimeandika kitabu: "The Life and Times of Abdulwahid Sykes (1924 - 1968) The Untold Story of the Muslim Struggle Against British Colonialism in Tanganyika, Minerva Press London 1998.

Kilichonisukuma kuandika kitabu hicho ni kule kuona kuwa historia ya uhuru ni historia ya Waislam jinsi walivyopambana na wakoloni kudai uhuru wa Tanganyika wakianza na African Association 1929 kisha wakaunda Al Jamiatul Islammiya fi Tanganyika (Umoja wa Waislam wa Tanganyika) 1933; na 1954 ikaundwa TANU.

Katika historia hiyo hapo juu Waislam walikuwa mstari wa mbele na mchango wao ni mkubwa kupita kiasi.

Bahati nzuri ni kuwa hawa waliofanya haya mimi baadhi yao ni wazee wangu kwa nasaba na wengine kwa ujamaa kwa hiyo ni watu ninaowajua vizuri.

Imeandikwa historia ya TANU na Chuo Cha CCM Kivukoni hawa wazee wangu waliounda African Association, Al Jamiatul Islammiya fi Tanganyika na chama Cha TANU hawamo ndani ya kitabu hicho, "Historia ya TANU," (1981).

Ndipo mimi nikaamua kuandika historia ya TANU na kupigania uhuru wa Tanganyika kama ninavyoijua.

Katika kitabu changu kama jina lake lilivyo nimeeleza mchango wa Waislam.

Ikiwa wewe unaona hili halikustahili kwa kuwa imewataja Waislam fahamu kuwa wengi wameipenda historia hii kwa kuwa ndiyo historia ya kweli ya ukombozi wa Tanganyika.
Mzee mbona hujamtaja Okello? Tuambie kama hakuhusika! Au hujui vyema historia ya mapinduzi ya Zanzibar?
 
Back
Top Bottom