Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 23,526
- 34,057
Allen...Angalau wewe umesema ukweli.... Kuna wanahistoria uchwara hawataki kuonesha kuwa kabla ya Karume "kuitwa" aliyekuwa kiongozi wa yale Mapinduzi alikuwa ni John Okello!!
Kiongozi wa mapinduzi alikuwa Dar es Salaam.
Wakati mauaji yanaendelea Zanzibar na Mohamed Shamte anazungumza na Nyerere kutafuta msaada wa kukomesha mauaji, viongozi wa mapinduzi ya Zanzibar walikuwa Government House, Dar es Salaam wakizungumza na Mwalimu.
Karume hakuwa anasubiri kuitwa na yeyote kuja kuchukua uongozi.
Angekuja tu kaitwa au hakuitwa.
Askari mamluki kutoka Kipumbwi akiwa lindoni Zanzibar angalia vizuri kofia ya chuma aliyovaa na sura yake.