Kwanini Abeid Amani Karume alimtimua John Okello "Empty Handed" licha ya kumsaidia kufanya Mapinduzi ya kumtoa Sultan?

Mzee mbona hujamtaja Okello? Tuambie kama hakuhusika! Au hujui vyema historia ya mapinduzi ya Zan
Mzee mbona hujamtaja Okello? Tuambie kama hakuhusika! Au hujui vyema historia ya mapinduzi ya Zanzibar?
Licking...

HII MADAA UKITAKA KUJUA HASWAA، MUULIZE MOHAMMES SAID NDIO NGULI WA HISTORIA, ATAKUPA MTIRIRIKO WOOTE,
Seli...
Makala hiyo hapo chini nimeiandika mwaka wa 2023:

MIAKA 20 BAADA YA KUFIKA PWANI YA KIPUMBWI: HISTORIA YA KAMBI YA KIPUMBWI KATIKA MAPINDUZI YA ZANZIBAR

Miaka 20 iliyopita tarehe kama ya leo 9 December, 2003 ndiyo siku Mohamed Omari Mkwawa alipotufikisha mimi na Dr. Harith Ghassany Kipumbwi.

Siku hii iliangukia kuwa siku Tanganyika ilipopata uhuru wake.
Kipumbwi ni kijiji kidogo cha wavuvi kilomita chache kutoka Tanga.

Hapa Kipumbwi ndipo ilipowekwa kambi ya askari mamluki wengi wao Wamakonde waliokuwa wanapewa mafunzo ili washiriki katika mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964.

Historia hii si ngeni kwa sasa kwani Dr. Ghassany kaieleza kwa kirefu katika kitabu chake, "Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru," (2010).

Lakini kabla ya yeye kufika Kipumbwi na kushuhudia kwa macho yake yale aliyoelezwa na Mzee Mkwawa Tanga mjini kuwa alihusika katika kuwavusha Wamakonde kwa siri kuingia Zanzibar kushiriki katika mapinduzi hii ilikuwa siri kubwa sana.

Sikupata siku kumuona Dr. Ghassany kafurahi kama siku ile.

Kwa hakika kabisa alikuwa na haki ya kufurahi kwani alikuwa amekitegua kitendawili kikubwa; kwanza kuwa kuwa kulikuwa na kambi ya mamluki katika ardhi ya Tanganyika waliovushwa na kuingia Zanzibar kusaidia mapinduzi.
Kafika Kipumbwi na Mzee Mkwawa akatupitisha sehemu zote kuanzia pango la chini walikukuwa wanaficha majahazi yao hadi kutuonyesha mgahawa mdogo walipokuwa wakila usiku kabla ya kuingia katika vyombo na kuanza safari.
Pili Kipumbwi ilisaidia kueleza mauaji yaliyotokea mashamba ambako Waarabu wengi waliuliwa.

Leo naikumbuka siku hii miaka 20 iliyopita na naweka picha tulizopiga Kipumbwi.
PICHA: Picha ya mwisho ni Mzee Mohamed Omari Mkwawa na mkewe.

1751726225728.png

1751726287490.png

1751726338470.png

1751726413947.png
 
View attachment 3395100
View attachment 3395102
View attachment 3395103
View attachment 3395104
Ninauliza kuhusu John Okello mzee wangu? Sijaona akitajwa! Alikuwepo au hakuwepo?
 
Mzee mbona hujamtaja Okello? Tuambie kama hakuhusika! Au hujui vyema historia ya mapinduzi ya Zanzibar?
Licking...
Makala hii nimeiandika mwaka wa 2023 na ni ndefu lakini nakuomba uisome yote ili umjue John Okello:

KUTOKA PEMBA: SURA USIYOIJUA YA ‘’FIELD MARSHAL’’ JOHN OKELLO

Historia ya Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka wa 1964 haiwezi kukamilika bila ya kumtaja John Okello.
Ukweli ni kuwa historia ya mapinduzi ipo na kwa miaka mingi imekuwa ikizungumzwa bila ya kutajwa John Okello.
Lakini wako wengi ambao hawatajwi lau kama wanatakiwa kutajwa na watambuliwe kama washiriki katika historia ya mapinduzi.
Wanamapinduzi wanayaita ‘’Mapinduzi Matukufu.’’
Wapinzani wa mapinduzi wanayaita, ‘’Mavamizi.’’
Katika miaka ya hivi karibuni katika mitandao ya kijamii John Okello anatajwa na wengine wanakwenda mbali kufikia kumwita, ‘’Baba wa Taifa wa Zanzibar,’’ ‘’Che Guevara wa Afrika,’’ nk.
Sifa hizi wanazitoa tu bila ya kufikiri kwani John Okello yuko nje kabisa ya kuwa muasisi wa Zanzibar iliyopo achilia mbali kuwa anaweza kufananishwa na Che Guevara.
Lakini hawa wenye kumpa lakabu hizo si Wazanzibari wengi wao huwa watu kutoka Tanzania Bara na hawana uelewa wa historia yoyote ila wanasukumwa na hamaki ndani ya nyoyo zao.
Labda tujiulize kwa nini iwe watu kutoka iliyokuwa Tanganyika ndiyo yanawatoka maneno hayo isiwe Wazanzibari wenyewe wenye mapinduzi yao?
Wanafanya hivi kwa chuki.
Wanadhani wakimnyanyua John Okello kama kiongozi wa mapinduzi watawaudhi Wazanzibari na hili pia litakuwa jibu kwa historia ya uhuru wa Tanganyika ambayo kwa kiasi kikubwa ilitawaliwa na Waislam ndani yao akiwemo Mufti wa Tanganyika wa miaka ile Mzanzibari, Sheikh Hassan bin Ameir.
Haya ni mambo mapya yaliyokuja miaka hii ya hivi karibuni pamoja na uandishi wa kusahihisha historia iliyokuwapo.
Wakati wa Mwalimu Nyerere na Mzee Karume historia hii haikuwapo.
Hapakuwa na watu wenye ujasiri wa kumtukuza John Okello wala kuandika historia kinyume ya historia rasmi iliyokuwapo wakati viongozi hawa wamekalia viti vyao.
Kwa nini haya hayakuwapo?
Ukiondoa uoga sababu nyingine ni kuwa ilikuwapo hali ya utulivu baina ya Wazanzibari na Watanganyika na watu wa pande zote mbili za muungano waliikubali hali iliyokuwako.
Ilitaka moyo mgumu sana kwenda kinyume na Mwalimu Nyerere au Mzee Karume kwa lolote lile lililowagusa wao au kuigusa Tanzania.
Viongozi hawa walikuwa na nguvu na wakitawala unaweza kusema kwa upande mwingine kwa mkono wa chuma.
Wakisemacho na wakitakacho wao huwa na ndiyo sheria.
Ikiwa hawa hawakutaki katika historia yao hakuna wa kukuingiza.
Mzee Karume hakumtaka Abdallah Kassim Hanga awepo katika historia ya mapinduzi na kwa hakika kabisa Hanga hayumo katika historia ya mapinduzi.
Mwalimu Nyerere hakutamtaka Oscar Kambona katika historia ya uhuru wa Tanganyika na kwa hakika Kambona hayumo katika historia ya uhuru wa Tanganyika.
Mwalimu Nyerere na Mzee Karume hawakumtaka John Okello awe sehemu ya historia yao na hakuwa.
Katika katika hali hii John Okello ikawa kama vile hakupata kuwako katika maisha ya siasa ya viongozi hawa.
Hili lilidumu kwa miaka mingi sana.
Mabadiliko ya siasa Tanzania khasa baada ya kuja mfumo wa vyama vingi mlango wa kughitilafiana ukafunguka na mlango huu
ukakaribisha mengi ambayo yalikuwa hayasemwi kabla sasa yakawa yanasemwa waziwazi kila mtu kuyasikia.
Yale yaliyokuwa ‘’nyeti’’ na ‘’mwiko’’ kusemwa yakapata nafasi katika vyombo huru vilivyokuja pamoja na mabadiliko haya.
Magazeti huru yakawa na pupa yakishindana kuchapa habari zilizokuwa zimefunikwa kwa miaka mingi.
Kubwa katika mapinduzi haya ya siasa ilikuwa ujio wa kupashana habari kupitia mitandao.
Katika hali kama hii ya uhuru wa kupitiliza ndipo lilipojitokeza jina la John Okello.
Katika hali ya kutaka kumtukuza John Okello aliyejipa cheo cha Field Marshal akaongezewa cheo kingine kikubwa kuliko Field Marshal, John Okello, wakatokea waandishi katika mitandao bila hofu yoyote wakamwita ati ni ‘’Baba wa Taifa la Zanzibar.’’
Hili limezua mjadala mkali kupita kiasi.
Historia ya John Okello katika mapinduzi ya Zanzibar ni historia ya umwagaji damu mkubwa uliotokea katika mapinduzi.
Hii ndiyo historia ya Zanzibar.
Dr. Harith Ghassany katika kitabu chake, ‘’Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru,’’ (2010) kaeleza hili kwa kirefu na kawataja wahusika wote kwa majina yao.
Historia ya John Okello ni historia ya hotuba zake kali kupitia Sauti ya Unguja hotuba ambazo ndizo zilizomfanya ajulikane ndani na nje ya mipaka ya Zanzibar.
Hivi ndivyo anavyokumbukwa John Okello na wale ambao walioshuhudia mapinduzi.
Bila ya hotuba hizi John Okello anakuwa mtu kama walivyokuwa wanamapinduzi wengine katika orodha ya waliofutwa kwa makusudi katika historia ya mapinduzi ya Zanzibar.
Bila ya hotuba hizi John Okello anakuwa sawasawa na wale Wamakonde waliovushwa kutoka Pwani ya Kipumbwi kuingia
Zanzibar kuja kusaidia kuiangusha serikali ya Waziri Mkuu Sheikh Mohamed Shamte.
Haya ndiyo yaliyopo katika historia ya mapinduzi.
Nimefika Pemba na nimekuwa na hamu kubwa sana ya kuona wapi John Okello aliishi alivyofika katika kisiwa hicho kutafuta maisha.
Wakati huo District Commissioner au kwa jina lingine, Mudir wa Pemba alikuwa Suleiman Mbaruk.
Familia hii bado ipo Pemba sehemu inayoitwa Mkanjuni na nimepata bahati ya kzungumza na baadhi yao.
Tunaweza kusema familia hii ndiyo iliyompokea John Okello Pemba mwaka wa 1959.
Nimeonyeshwa nyumba aliyokuwa akiishi Suleiman Mbaruk aliyekuwa Liwali wa Pemba maarufu inaitwa, ‘’Nyumba ya Kasuku,’’
kwa kuwa kulikuwa na kasuku barazani ambae alikuwa mtu akipata atamtolea maneno ya kumnanga.
Kwa ajili hii inasemekana watu walikuwa wanaogopa kupita mbele ya nyumba hiyo kwa kumuogopa kasuku yule kwani kasuku huyu anaweza kusikika akikusema, ‘’Muone hata viatu hakuvaa,’’ na ikasadifu kuwa hakika mtu huyo hakuwa na viatu.
Lakini umaarufu wa nyumba hii si tu kwa ajili ya huyu kasuku mropokaji na kuwa ilikuwa nyumba ya Liwali, la hasha, umaarufu wake ulikuwa Sultan wa Zanzibar, Khalifa bin Haroub alikuwa akija Pemba kufanya ziara anafikia hapo nyumbani kwa Liwali Suleiman Mbaruk ingawa alikuwa analala kwenye meli yake iliyotia nanga baharini.
Kuwa John Okello, mtu dhalili kutoka Uganda alikuja kuingiliana na watawala wa kisiwa cha Pemba hapana maelezo ila kusema ilikuwa Qadar ya Allah.
Mwenyezi Mungu alipanga iwe hivyo.
Watu ambao walimjua John Okello katika siku zake za mwanzo akiwa anafanya kazi za ujenzi kama kibarua kujipatia rizki yake wengi wao wametangulia mbele ya haki.
Lakini familia iliyopata kuishi na John Okello alipofika Pemba na wakampatia mahali pa kukaa ni familia ya Mohamed Nassor Mazrui na aliishi kati ya jamii hii hapo Mkanjuni hadi alipoondoka kuelekea Unguja mwaka wa 1963.
Bahati mbaya nyumba aliyokuwa akiishi John Okello haipo na imeanguka miaka hii ya karibuni.
Kwa hakika haikuwa nyumba bali banda.
Banda hili aliloishi John Okello kama lingehifadhiwa ingekuwa sehemu muhimu ya historia ya Zanzibar na Tanzania kwa ujumla na pengine ingesababisha na nyumba ya Mudir Suleiman Mbaruk nayo ihifadhiwe kama sehemu muhimu katika historia ya Pemba.
Nyumba ya Kasuku ya Liwali Suleiman Mbaruk Bedui bin Salim bado ipo lakini ni gofu imehamwa hakuna anaeishi hapo na si muda mrefu itakuwa nayo vilevile haipo, italala mchangani na mchanga utazolewa na mvua na kusukumwa Bahari ya Hindi kubakiza kiwanja kitupu.
Wakati huu ilikuwa ikijengwa shule, Seyyid Khalifa Secondary School na John Okello alikuwa kibarua hapo kama mbanjuaji wa kokoto zilizokuwa zinatumika katika ujenzi.
Mjenzi wa shule hii alikuwa Ahmed Nassor Mazrui na bila shaka hii ndiyo ikawa sababu ya John Okello kupata kazi katika ujenzi wa shule hii ya Seyyid Khalifa ambayo baada ya mapinduzi ikabadilishwa jina jina ikaitwa, ‘’Fidel Castro,’’ jina la kiongozi wa mapinduzi ya Cuba.
John Okello ndiyo huyu akiwa sehemu ya historia ya Pemba akiishi kama waivyoishi wengi waliokwenda Pemba kutafuta maisha katika kuchuma karafuu na kazi nyingine.
John Okello akaondoka Pemba mwaka wa 1963 kwenda Unguja kujaribu kuboresha maisha yake.
Bila ya shaka yoyote nyumba aliyopewa John Okello na Mazrui ilipata kukaliwa na vibarua wengine kama yeye na wao pia walikaa hapo na wakaondoka na wengine wakaja na yawezekana hawakurejea tena Pemba.
Si John Okello.
John Okello alirejea Pemba mwaka wa 1964 baada ya miezi miwili kutokea mapinduzi
John Okello hakurejea Pemba kama kibarua.
John Okello alirejea Pemba akiwa ‘’Field Marshal’’ akisindikizwa na askari wake.
Hapa haijalishi kama John Okello alikuwa kweli ni Field Marshal kama Joseph Tito wa Yugoslavia aliyepigana Vita Vya Pili Vya Dunia (1939 - 1945) au vinginevyo.
Bila shaka asubuhi ya kuamkia mapinduzi, wahisani na wenyeji wa John Okello pale Mkanjuni walisikia sauti yake katika Sauti ya Unguja akitangaza kupinduliwa kwa serikali ya Zanzibar.
Nakuachia wewe msomaji ufikirie wale waliokuwa wanamjua John Okello kama foreman mbanja kokoto akijenga shule ya Seyyid Khalifa bin Haroub hali yao ilikuwaje?
Hebu fikiri mshangao wao ulikuwa mkubwa kwa kiasi gani?
Tumekaa na mpashaji habari wetu Sheikh Abdallah Nassor Suleiman, mjukuu wa Liwali Suleiman Mbaruk ndani ya Msikiti wa Ibadh wa Mkanjuni baada ya Sala ya Ijumaa msikiti ukiwa mtupu tuko peke yetu pembeni.
Sheikh Abdallah Nassor Suleiman katuteka kwa ufasaha wake wa kuzungumza akitueleza historia hii ya baba na babu zake na John Okello.
Sheikh Abdallah anasema John Okello alifika nyumbani kwao miezi miwili baada ya mapinduzi kwa vishindo vikubwa akiwa kafuatana na askari wa mapinduzi lakini vishindo vile havikuwa vya shari.
Ugeni huu wa Field Marshal utakuwa mwezi wa March, 1964.
John Okello aliingia uwanjani akipiga hodi na kuita majina ya wazee wake kwa furaha na bashasha, ’Yuko wapi Mzee Ahmed Nassor wakasalimiana kwa adabu pamoja na mkewe Bi. Mariam, akatoka akaenda kwa Mzee Mohamed Suleiman akamsalimu.’’
Kote humu anapita askari wa mapinduzi wanamfuata nyuma.
John Okello akawaambia askari wake kuwa wale ni wazee wake na ameishinao kwa wema wasibughudhiwe.
Hivyo ndivyo ilivyokuwa.
Watu hawa hawakupata kumnyanyasa John Okello.
Waliishi na yeye kwa salama na amani.
Askari wakatoa stengun wakapiga mfulilizo wa risasi juu kama ishara ya furaha na uwanja mzima ukajaa watu na watoto wadogo wanafurahia kuwaona askari na kusikia mlio wa risasi.
Hawa aliokuja kuwasalimua na kuwahakikishia usalama wao na kuwaita wazee wake ni ‘’Waarabu’’kama walivtyokuwa ‘’Waarabu,’’ wengine waliouliwa Unguja lakini John Okello anasema hawa wa Mkanjuni waliompa kazi na mahali pa kuishi walikuwa watu wema.
Hapa panafikirisha.
Tunaweza kusema wale ‘’Waarabu’’ wa Unguja waliokuwa mashamba ambako wengi ndiko walipouawa laiti wangelipata fursa ya kuishi na wale Wamakonde kutoka Kipumbwi na wao wangeliushuhudia wema wao na kutokana na wema huo wangenusurika kuuawa.
Huu ni upande wa pili wa John Okello ambao wanahistoria bado hawajaueleza.
Hapa panahitaji utafiti.
Gramafoni za wanaomwandika John Okello zimekuwa zikipiga na kusikiliza upande mmoja tu wa santuri za His Master's Voice (HMV).
Okello hakurejea tena Pemba baada ya safari ile kwake ilikuwa kama kaja kuwaaga nduguze na akayasema maneno hayo ya shukurani kwa kinywa chake tena hadharani.
John Okello aliporejea Unguja hakukaa sana alifukuzwa Zanzibar akarejeshwa kwao kwa idhara kubwa na wale waliomtumikisha na kumsabilia radio kutangaza mapinduzi.
Baada ya mapinduzi mwezi January hadi kufika March John Okello baada ya kupita miezi miwili akawa muhamiaji asiyetakiwa Zanzibar.
Siku moja ni nyingi katika siasa sikwambii miezi miwili.
PICHA:
1. John Okello
2. Sheikh Abdallah Mohamed Nassor kushoto aliyeegemea ukuta
3. Mabaki ya nyumba ya Liwali Suleiman Mbaruk naarufu kwa jina la "Nyumba ya Kasuku."
4. Nyumba ya Mazrui kama ilivyo hivi sasa
5. Shule ya Fidel Castro (zamani Shule ya Seyyid Khalifa bin Haroub)

Mzee utamkandia sana John Okello kwa kuwa hakuwa mmoja wa "wazee wako" ila historia yake adhimu katika mapinduzi ya Zanzibar kuundoa utawala dhalimu wa mwarabu haitafutika bali itaendelea kuenziwa daima.
 
Hiyo ni baada ya mapinduzi. Jee kabla ya mapinduzi Okello na Karume waliwahi kupanga pamoja kuhusu kumpindua Sultan?
Inasemwa Okello ndio alikuwa field front kabisa wakati wa mapinduzi, Karume hata haijulikani alikuwa wapi siku ya mapinduzi.
 
Yoda,
Hilo haliwezekani.

Mipango yote ilifanyika Dar es Salaam na wahusika wakuu walikuwa Oscar Kambona na Abdallah Kassim Hanga.

Kisha kulikuwa na wahusika wengine Tanga waliokuwa wakisimamia kambi ya Kipumbwi.

Hawa walikuwa Jumanne Abdallah, Regional Commissioner wa Tanga na District Commissioner, Ali Mwinyi Tambwe.

Hawa wakisaidiwa na Victor Mkello, Kiongozi wa Chama Cha Wakata Mkonge na Mohamed Omari Mkwawa waliokuwa wasimamizi wa kambi ya Kipumbwi walikowekwa mamluki waliovushwa kwenda Zanzibar na majahazi nyakati za usiku.

Okello hakupata kufika Kipumbwi wala hakujua mpango wa Kipumbwi.
 
Yoda,
Hilo haiwezekani.
Mipango yote ilifanyika Dar es Salaam na wahusika wakuu walikuwa Oscar Kambona na Abdallah Kassim Hanga.

Kisha kulikuwa na wahusika wengine Tanga waliokuwa wakisimamia kambi ya Kipumbwi.

Hawa walikuwa Jumanne Abdallah Regional Commissioner wa Tanga na District Commissioner Ali Mwinyi Tambwe.

Hawa wakisaidiwa na Victor Mkello na Mohamed Omari Mkwawa waliokuwa wasimamizi wa kambi ya Kipumbwi walikowekwa mamluki waliovushwa kwenda Zanzibar na majahazi nyakati za usiku.

Okello hakupata kufika Kipumbwi wala hakujua mpango wa Kipumbwi.
Umemaliza kila kitu Mzee wangu, wapo watu hawajui hilo
 
Mzee utamkandia sana John Okello kwa kuwa hakuwa mmoja wa "wazee wako" ila historia yake adhimu katika mapinduzi ya Zanzibar kuundoa utawala dhalimu wa mwarabu haitafutika bali itaendelea kuenziwa daima.
Yoda,
Mimi nimetafiti na naandika kile nilichokiona katika utafiti wangu.

Kuhusu "udhalimu."
Kuwa makini na neno hilo.

Unaelewa yaliyotokea baada ya Mapinduzi?
 
Kwa Jinsi Mapinduzi yenyewe yalivyotokea John Okello unamweka kwenye daraja gani kuhusu Mapinduzi yale?
Allen...
Sauti ya Okello akitangaza kuanguka kwa serikali ya Zanzibar kuliwatisha wananchi wengi.

Ile lafidhi yake na maneno ya kuua yalitia hofu kubwa.
Achilia mbali mauaji yaliyokuwa yameshatokea.
 
Haya maelezo nayajua... Wewe kama mfuatiliaji wa historia, nataka kujua Okello unamweka kwenye daraja lipi?

1. Jee ni sehemu ya mamluki toka kambi ya kipumbwi?

2. Ni sehemu ya waliopanga Mapinduzi akiwa ni mwan ASP na kuongozwa na kina Karume?

3. Au yeye alikuwa ni sehemu ya wanamapinduzi ambao historia imepindishwa ili wasitambulike?
 
Okello hakuwa kokote katika hayo uliyouliza ila no. 3 ni kuwa alishiriki kama walivyoshiriki wengi ambao hawatajwi.
 
Sasa ilikuwaje Karume akaomba usaidizi wa Nyerere ili Okello aondolewe Zanzibar?

Siku ya mapinduzi na siku kadhaa baadae kabla yeye Okello kutangaza Karume "achukue madaraka" Okello alikuwa na nguvu Sana.

Ni kweli Okello hakuwa na taathira yoyote kwenyw yale Mapinduzi?
 
hadi leo alivyoficha na ku edt tunahangaika namna ya kupata
Kina...
Nimetafiti historia ya wazee wangu...

ABDULWAHID SYKES NA HISTORIA YA TANU: "WE MZEE!" LUGHA YA DHARAU, KEJELI NA VITISHO''

Baada ya uhuru zilipoanza kauli ya kukashifu TAA na yeye mwenyewe Abdul kuwa hakuwa anaongoza chama cha siasa bali cha starehe mmoja wa marafiki zake aliyekuwa anaumizwa na maneno yale alikuwa Ahmed Rashad Ali.

(In Shaa Allah nitaweka historia ya Ahmed Rashad hapa kwa faida yetu sote).

Ahmed Rashad akawa anamuomba Abdul aeleze historia ya TANU kuanzia jinsi baba yake alivyoanza harakati kupitia African Association mwaka wa 1929.

Abdul Sykes alikataa akimwambia kuwa kama tatizo ni nani kaunda TANU yeye hilo halimshughulishi na hakika Abdul hakufungua kinywa chake hadi anaingia kaburini.

(In Shaa Allah nitakuwekeeni hapa yale aliyoandika Daisy kuhusu vipi baba yake alikabiliana ni fitna hii katika kipindi hiki).

Nilipokuwa nasafiri kuwatafuta hawa wazalendo ilikuwa tukimaliza mazungumzo nataka kunyanyuka kuondoka wananambia nisubiri tupige fatha, yaani tufanye dua.

Wakisema kuwa hili jambo nililokuwa nalifanya ni kubwa sana linahitaji msaada wa Allah.

Baadhi ya wazee hawa wengi walifariki kabla kitabu hakijatoka na wengine nilibahatika kuwapa nakala ya kitabu kwa mkono wangu ingawa kilikuwa kwa Kiingereza na wasingeweza kukisoma.

Moyoni walikuwa wanasononeka kuwa mchango wao katika kupigania uhuru haukuzaa matunda waliyotegemea.

Leo nafarajika ninaposoma jina la Abdul Sykes lililofutwa katika historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika lilivyorejea na sasa limekuwa maarufu watu wakibishana kuhusu yeye.

Kleist Sykes mtoto wa Abdul Sykes alikuja ofisini kwangu Tanga kunishukuru baada ya baba yake na baba yake mdogo Ally Sykes, kutunukiwa Medali ya Mwenge wa Uhuru kwa mchango wao katika kuunda TANU na kupigania uhuru wa Tanganyika.

Kleist alinipa mkono huku akibubujikwa na machozi.

Leo ninaposoma lugha za "We mzee," lugha za dharau na kejeli na wakati mwingine vitisho dhidi yangu sikasiriki.

Wale wazee waasisi wa TANU walinambia hii kazi niliyoamua kufanya ni nzito.

Daisy anaeleza chokochoko zilizivyoanza karibu ya kupata uhuru na zikaendelea baada ya uhuru:

‘’...uhuru ulipokuwa dhahiri sasa unapatikana na ulipopatikana ulikuja na changamoto nyingi ambazo naamini baba hakuzitegemea.

Haitakuwa sawasawa ikiwa sitaeleza upeo wa juu wa baba yangu katika wema, huruma na unyofu aliokuwanao.

Hata nilipokuwa mtoto nilipata kushuhudia na kuona chokochoko na chuki dhidi yake bila shaka kwa ajili ya hasad kwani baba kwa kiwango chochote kile alikuwa mtu aliyefanikiwa na kwenye ngazi nyingi wengi hawakuthubutu hata kuota kukanyaga, lakini sikumuona baba kukasirika wala kutaka kulipiza kisasi.

Katika unyofu wa hali ya juu aliendelea na maisha yake...’’
Katika kipindi hiki Abdul Sykes alikuwa anatembelea Mercedes Benz 220 SE.

Kijana mwingine Dar es Salaam aliyekuwa na gari kama hii alikuwa kijana wa Kiarabu Abbas Abdulwahab.

Huenda maisha kama haya ndiyo yaliyosababisha hasad na wivu dhidi yake na Abdul alikuwa hata hajafikisha miaka 35.

Kuna msemo wa Kiarabu unaosema kuwa, ''Sababu huondoa ajabu.''

Jibu tunalo kwa nini magazeti TANU ya chama alichoasisi na kukifadhili kwa miaka mingi hayakuweza kumpa Abdul Sykes ile heshima ndogo aliyostahili katika umauti wake.

Kuchapa taazia yake ndani ya magazeti ya Uhuru na The Nationaist na kueleza yale aliyoyafanya kwa Nyerere na TANU wakati wa kupigania uhuru wa Tanganyika ilikuwa ni kumnyanyua juu katika sifa na heshima isiyo kifani.

Maadui wa Abdul Sykes walitaka jina lake lipotee kabisa katika ramani ya historia ya Tanzania.

Lakini Brendon Grimshaw alipochapa taazia ya Abdu Sykes katika Sunday News (20 October, 1968) kichwa cha taazia ile ilikuwa katika wino mweusi uliokoza: ''ABDUL SYKES WAS A TANU PIONEER.''

Hiyo picha ni siku watoto wa Abdul Sykes waliponiita nikaione Medali aliyotunukiwa baba yao (posthumous) katika kumbukumbu ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanganyika.

Aliyevaa nguo nyekundu ni Daisy na kushoto wa kwanza ni Kleist.

Screenshot_20200801-201940.jpg

MEDALI YA MWENGE WA UHURU.jpg
 
Attachments

  • 1751747285489.gif
    1751747285489.gif
    42 bytes · Views: 22
Allen...
Sauti ya Okello akitangaza kuanguka kwa serikali ya Zanzibar kuliwatisha wananchi wengi.

Ile lafidhi yake na maneno ya kuua yalitia hofu kubwa.
Achilia mbali mauaji yaliyokuwa yameshatokea.
Unamaanisha kwamba Okello alikuwa msemaji kama msigwa wa Serikali ya Mapinduzi kwa sababu tu ya sauti na lafudhi yake!?
 
Ozan,
Nia ilikuwa kuitia hofu jamii wapigwe na butwaa hawa watu gani wamevamia Zanzibar wanaua watu na sasa wameteka radio.

Hii ilifanikiwa sana.
 
Back
Top Bottom