Kwanini Abeid Amani Karume alimtimua John Okello "Empty Handed" licha ya kumsaidia kufanya Mapinduzi ya kumtoa Sultan?

Allen...
Sijui hii ya Karume aliomba usaidizi wa Nyerere kumuondoa Karume umeipata wapi.

Okello alizuiwa na Hashil Seif Hashil asiingie Zanzibar akiwa ndani ya ndege.
 
achana na hao father ,wanaokuita "we mzee"

kikubwa mungu akuzidishie urefu wa maisha yako na mama yangu hapo nyumbani ili uendelee kutupa maswala haya yenye tija kihistoria
 
hebu tuambie mchango wa Okelo, usiwe na kigugumizi kwa sababu alikuwa kafiri kwako.
 
hebu tuambie mchango wa Okelo, usiwe na kigugumizi kwa sababu alikuwa kafiri kwako.
Yesu...
Kwa lugha kama hiyo yako siwezi kujadiliana na wewe.
Ungeweza tu kwa adabu ukaniuliza mchango wa Okello.

Ningekueleza.
 
Yesu...
Kwa lugha kama hiyo yako siwezi kujadiliana na wewe.
Ungeweza tu kwa adabu ukaniuliza mchango wa Okello.

Ningekueleza.
nilijua tu hauwezi kuueleza, kwa sababu hakuwa wa dini yako. hata mimi sio kwamba nilikuwa naomba sana ueleze kwa sababu siujui, ninaujua ila nilitaka wote waone namna unavyopata kigugumizi kueleza mchango wa mtu asiye wa dini yako kwenye mapinduzi ya eneo lenye waut wengi wa dini yako. nakuelewa, sio rahis!
 
Yesu...
Hayo uliyosema ni fikra zako na una haki nazo.
Ila sioni hizi ghadhabu ni kwa sababu gani.

Mimi si mtu wa kushindwa kujibu suala la utafiti ambao
mimi nilishiriki nikiwa Research Assistant wa Dr. Harith
Ghassany aliyeandika, ''Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru,''
(2010).

Naijua vyema historia ya Zanzibar na Maktaba yangu ina
mengi kuhusu historia hii.

Nimezungumza na washiriki wa mapinduzi na waliopinduliwa
na waliopindua na wasomi wa Kizanzibari uso kwa macho:
Abdulrahman Babu (London, 1991), Ali Muhsin Barwani, Issa
Nasser Ismaily (Muscat, 1999).

Nimealikwa Zanzibar mara kadhaa kufanya pitio la vitabu
vilivyoandikwa na wazalendo wasomi wa Kizanzibar kuhusu
mapinduzi: Hashil Seif Hashil, Khamis Abdulla Ameir na Ibrahim
Mohamed Hussein.

Achilia mbali makongamano niliyohudhuria ndani na nje ya
Tanzania.

Itawezekana vipi nishindwe na wewe ndugu yangu?

Tunaweza tukafanya mjadala na ukaniuliza chochote katika
historia ya Zanzibar.

Unachotakiwa kuzingatia ni tufanye mjadala wa heshima.
 
Allen...
Sijui hii ya Karume aliomba usaidizi wa Nyerere kumuondoa Karume umeipata wapi.

Okello alizuiwa na Hashil Seif Hashil asiingie Zanzibar akiwa ndani ya ndege.
Hiyo ndege ilikuwa inatoka wapi na Okello aliondokaje Zanzibar baada ya mapinduzi hadi akawa anarudi Zanzibar Kwa ndege?
 
Allen,
Alikwenda Dar es Salaam kuonana na Mwalimu Nyerere.
Aisee!!!

Sauti yake ndiyo iliyotakiwa...lakini picha za siku ya mapinduzi kuanzia kuvaa kwake na hata kukaa kwake alionekana yeye alikuwa ni kiongozi wa wenzake.
 
Aisee!!!

Sauti yake ndiyo iliyotakiwa...lakini picha za siku ya mapinduzi kuanzia kuvaa kwake na hata kukaa kwake alionekana yeye alikuwa ni kiongozi wa wenzake.
Allen...
Kukaa kwake ndiyo awe kiongozi wa Mapinduzi?

Katika hizo picha umewaona Mohamed Omari Mkwawa, Victor Mkello, Ali Mwinyi Tambwe, Jumanne Abdallah, Kassim Hanga, Oscar Kambona au Jimmy Ringo?

Hii ni timu ya Kipumbwi.

Unajua mchango wa Kipumbwi katika Mapinduzi?
 
Historia ya yale Mapinduzi na hao watu waliokuwa kipumbwi kama hakuna maelezo toshelevu ni kwa nini Okello aliongoza yale Mapinduzi basi yanabaki kuwa masimulizi tu.

Tunaojua Mapinduzi hufanyikaje, hawezi mtu asiyeaminika au asiye na nguvu ya ushawishi kwa wana Mapinduzi akapewa nafasi ya kuongoza Mapinduzi.
 
kwa hiyo okelo hakuongoza mapinduzi, ndo unavyomaanisha? kile alichokifanya ni nini sasa?
 
Inasemekana siku alizo kalia kiti zanzibar iliwaka moto
Angalau wewe umesema ukweli.... Kuna wanahistoria uchwara hawataki kuonesha kuwa kabla ya Karume "kuitwa" aliyekuwa kiongozi wa yale Mapinduzi alikuwa ni John Okello!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…