Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 23,526
- 34,057
Allen...Angalau wewe umesema ukweli.... Kuna wanahistoria uchwara hawataki kuonesha kuwa kabla ya Karume "kuitwa" aliyekuwa kiongozi wa yale Mapinduzi alikuwa ni John Okello!!
Yaani hujibu swali langu. Hao watu wa kipumbwi au huyo aliyekuwa Dar, walimweka nani kule Zanzibar asimamie yale Mapinduzi?Allen...
Kiongozi wa mapinduzi alikuwa Dar es Salaam.
Allen...Yaani hujibu swali langu. Hao watu wa kipumbwi au huyo aliyekuwa Dar, walimweka nani kule Zanzibar asimamie yale Mapinduzi?
Mambo ya kuweka picha za mtu kavaa kofia ya chuma bila kuwa na Ithibati kuwa huyo mtu alikuwepo siku ya mapinduzi pale Zanzibar ni porojo tu.
Kina Natepe, Mfarinyaki na Washoto hawakuwa na kofia za chuma lakini walikuwepo mbele kabisa na Okello siku ya mapinduzi.
Yaani Okello zichukuliwe hatua na watu wa Afrika Mashariki nzima kumdhibiti halafu mtake kufanya alikuwa ni mtu wa kawaida tu kwenye Mapinduzi yale?Naamini umepata kusikia Kamati ya Watu 14.
John Okello hakuwa mjumbe wa Kamati hii.
Allen...Yaani Okello zichukuliwe hatua na watu wa Afrika Mashariki nzima kumdhibiti halafu mtake kufanya alikuwa ni mtu wa kawaida tu kwenye Mapinduzi yale?
Hizi harakati za kuudogosha mchango wa Okello kwenye Mapinduzi yale lengo lake ni nini hasa?
Kama kulikuwa hakuna mpangilio wa kufanya yale Mapinduzi, hizo saa sita za kuuangusha utawala wa Sultan Zanzibar zilisimamiwa na nani?
Unataka kusema kuwa bila ya sababu maalum Okello aliingia kwenye studio za redio Zanzibar na kutangaza Mapinduzi yale bila ya yeye kuwa na mamlaka yoyote Kwa wanamapinduzi?
Hoja dhaifu kabisa hii bwana mtafiti. Kwa ivo kina Natepe walimtii kwa kuwa alikuwa ana sauti ya kutishia?Okello alipewa radio na sababu Kuu ilikuwa kutisha Wazanzibari kwa lafidhi yake atakapokuwa anatangaza kuanguka kwa serikali ya Mohammed Shamte.
Allen...Hoja dhaifu kabisa hii bwana mtafiti. Kwa ivo kina Natepe walimtii kwa kuwa alikuwa ana sauti ya kutishia?
Wakati wa Mapinduzi hao wajumbe wa Kamati ya watu 14 walikuwa field? Hivi Okello aliondokaje Zanzibar?
John Okello si swala tano si miongoni mwa Wazee wake wa Kipata usitarajie atamweka sehemu inayomstahili.Mzee utamkandia sana John Okello kwa kuwa hakuwa mmoja wa "wazee wako" ila historia yake adhimu katika mapinduzi ya Zanzibar kuundoa utawala dhalimu wa mwarabu haitafutika bali itaendelea kuenziwa daima.