Kwanini Africa ukifikisha 35, 45, 55, tunasema ni mzee?

Mkuu umeelezea vizuri sana.
 
Kweli kabisa Mtu ana miaka 50 hapa Tanzania wanasema ni mzee, hata kidogo! Uzee ni miaka 76 na kuendelea.

1. 0-17 Mtoto
2. 18-50 Kijana
3. 51-75 Mtu mzima
4. 76> Mzee
Naelewa Africa watu wanawaona wenye miaka 50 kuwa wazee kwasababu ya age profile ya Africa ambapo watoto na vijana chini ya 35 ni wengi kuliko makundi mengine.
 
Sasa wewe kjana ana miaka 16 anaanza kupiga kamunyweso ka smart gin mixer na gongo, mo energy anashushia na ugoro . Bado pia pia zake kageuza ekzosi ya ist muda wote zinatoa Moshi wa bange, sigara na gozo, utegemee mpaka afike 20 atakua bado kjana. Saivi vijana wanaonekana wazee sababu ya mtindo mbovu wa maisha. Kjana unakuta kavimba mashavu na pia yamelegea sababu ya pombe Kali. Midomo imeunguzwa na sigara.
Wacha niishie hapa tu
 
Kwa mfano Finland old age sio 70 tena , sababu watu wenye miaka 70 wako ngangari haswa. Uzee unatokana na maisha mabovu.
 
Sifa kubwa ya uzee ni kitambi.Ukiwa na kitambi hata kama una 25 utaitwa mzee.Hao waliotajwa hapo kina Obama hawakuwa/hawana na vitambi
 
Uzee na ujana mara nyingine ni kitu relative ambacho kinaendana na life expectancy pamoja na demographics za nchi.

Katika nchi ambayo life expectancy ni miaka 50, na asilimia 90 ya watu wake wako chini ya miaka 40, ukiwa na miaka 40 wewe ni mzee.

Katika nchi ambayo life expectancy ni miaka 90, na 40% ya wananchi wake wana miaka chini ya 40, kuwa na miaka 40 si mzee.

Huko Afrika watu wanaonekana wazee mapema kwa sababu life expectancy ni ndogo halafu population zina watoto wengi.

Ukiwa wewe mtu mmoja una miaka 45 katika kundi la wengine watoto watoto 99 wenye miaka chini ya 18, utaitwa mzee tu.

Ukiwa wewe mmoja mwenye miaka 45 umekaa kundi la watu wengine 99 waliozidi miaka 70, utaitwa kijana tu.
 
Inategemea ujue kuna watu wanamiaka 20 Ila wanonekana Kama wana 40 yrs

Ukija katika Hoja yako kuwa watu wenye umri mkubwa wana akili zilizokomaa labda ulaya na sio Tanzania
 
What does it matter ni life Expectancy ya nchi husika au sehemu husika,, kwa Tanzania kuitwa mzee katika hiyo age ni kitu cha kawaida kabisa,, kwa sababu ukiangalia life Expectancy ya Tanzania ni below 70 kwa asilimia kubwa.

And the rest ni kwamba watoto na vijana wenye age below 40 ni wengi ukilinganisha na kundi lingine.
 
Mtoto ndio anaweza kumuita au kumuona mtu mwenye miaka 35/45/55 mzee.
Hata mimi nilipokuwa mdogo baba yangu wakati ana 40s nilkuwa namuona mzee.
[emoji3581][emoji3581][emoji3581]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…