Kwanini amechagua Kigoma?

Kwanini amechagua Kigoma?

Keynez

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2007
Posts
2,428
Reaction score
3,937
Siku ya leo kwa hali inayoonyesha ni makusudi kabisa, timu ya kampeni ya Magufuli imegonganisha shughuli zake za kiserikali na ujio wa Tundu Lissu mkoani Kigoma.

Ni kwa muda sasa Lissu amejaribu kukutana uso kwa uso na Magufuli huku watu wa Magufuli wakitumia kila njia kukwepa hilo lisitokee.

Kumekuwa pia na minong’ono ya uwezo wa pande hizi mbili kukusanya idadi ya watu katika mikutano yao.

Kwenye mapambano wanasema, chagua eneo sahihi la kufanya shambulizi. Eneo hilo inabidi uwe na nguvu kumshinda adui yako.

Sasa najiuliza, kwa nini timu ya Magufuli imeamua Kigoma ndiyo sehemu sahihi ya kupimana makali na timu Lissu? Huku akijua Lissu anaweza kupata backup ya Zitto, kwa nini bado aliona afanye hili alilofanya leo? Kwa nini wamemuita Rais wa Burundi, tena labda kwa short notice katika lengo hili? Nini wanategemea kukifanikisha siku ya leo?
 
Bora ungesema Lissu, Zitto Kigoma hana chake tunamuona snitch tu
 
Yaani maswali meeengiii kuliko majibu. Kwaio unatuuliza sisi au CCM?
 
Kule--------, alimwita mu7, huko anamwita huyo, hao waliohitwawote ni marafiki zake na wanamfumu unaofanana.Pia wanapitia mashambulizi yanayo fanana.
 
Magufuli ataikimbia Kigoma mara tu baada ya ufunguzi wa jengo la mahakama. Hana uwezo wa kukabiliana na Lissu. Lissu is another level.
 
Yaami mna mawazo ya kijinga sana ! Kwanini mnapenda kimlinganisha jpm na huyo Tundu wenu! Mtambue kuwa Jpm bado ni Rais , hivyo tusiaminishane eti amapimanana lissu !.
 

Attachments

  • 2523669_Subpost_4_-_Mgombea_Urais_wa_Jamuhuri_ya_Muungano_wa_Tanzania_kupitia_Chadema_Mh__360_...jpg
    2523669_Subpost_4_-_Mgombea_Urais_wa_Jamuhuri_ya_Muungano_wa_Tanzania_kupitia_Chadema_Mh__360_...jpg
    44.1 KB · Views: 2
Uzuri mkiwa kwenye keyboard mnaandika kweli kweli ila matokeo huwa mnyajua
 
Kule--------, alimwita mu7, huko anamwita huyo, hao waliohitwawote ni marafiki zake na wanamfumu unaofanana.Pia wanapitia mashambulizi yanayo fanana.
Unataka kusema akienda Arusha atamwita Uhuru??
 
Kule--------, alimwita mu7, huko anamwita huyo, hao waliohitwawote ni marafiki zake na wanamfumu unaofanana.Pia wanapitia mashambulizi yanayo fanana.
Machadema akili zenu sawa na za ng'ombe tu, sasa hapo sijui ndio umeandika nini!!? we unataka kumlinganisha mhe Rais na tapeli toka ubelgiji!!
 
Back
Top Bottom