Kwanini app za mikopo ya mtandaoni zinatumia picha za wanawake warembo kutangaza biashara zao?

mshamba_hachekwi

JF-Expert Member
Joined
Mar 3, 2023
Posts
20,704
Reaction score
66,337
Kama unatumia sana youtube utakuwa umekutana na matangazo ya mikopo mtandao.

Mimi sikuwa nayazingatia mpaka yakaanza kuwa ya ajabu ajabu kama hivi;



Basi nikaamua kufuatilia kidogo, nikatafuta makampuni yanayomiliki haya matangazo.

Cha kushangaza utakuta vikampuni vingi vingi viko chini ya kampuni moja kubwa.

Mfano Singularity Microfinance Limited ina matangazo ya PesaX na CashX.

Dexintec Global Limited inamiliki kwanzaloan, hewamkopo, twigaloan, finiloan, na jiachie cash.

Dexintec wamechapisha matangazo 40+ ndani ya huu mwezi mmoja tu kutoka April.


Dexintec ni kampuni ya kichina, wana fanya kazi kwenye nchi maskini kama Nigeria na Pakistan


Huko mitandaoni watu wanalalamika mikopo yao inawakandamiza.



Hawa majamaa ni loan sharks. Huu ni uhalifu kabisa, kunyonya maskini kupitia mikopo.

Nimesikia mwigulu alisema bungeni huduma za mobile money kama Airtel timiza, Vodacom songesha hazina leseni, kama hao hawana, hawa kausha damu vipi?

Na wakati huo huo BOT wanasema watoa mikopo mtandao wapo chini ya makampuni yenye leseni. Ingekuwa hivyo, wangenyonya watu?

Nimewaza tu, nakaribisha wenye mawazo/maoni mbalimbali.
 
Sijui kwa nini naamini Makonda anaweza kupambana na hawa walaghai. Yaani hii nchi viongozi wengi hawana uwezo wa kutatua kero za wananchi badala yake wao ndio wamekuwa wazalisha kero inafika wakati unahisi kuna kundi katika utawala lipo kwa ajili ya kuhakikisha masikini wanaendelea na umasikini kwa kuwatwika makodi, mikopo na kupandisha bei bidhaa.
 
Sasa mkuu wa mkoa anahusika vipi hapo aisee??
Jamaa kawalisha sumu mbaya sana.
 
Kweli mkuu
 
Natamani sana tuwe na taifa la kutafiti na kuhoji Kama hivi, vijana kwa wingi wao wakihoji mambo kama haya, nchi itabadilika hii...Kumbuka wafanya maamuzi wengi ni wazee wanaozidiwa ujanja na kundi la vijana mafisadi.
 
Trust me, huwezi kuwa timamu ukakopa kwenye hayo makampuni. Yaani na utimamu wako usome terms and conditions zao za mkopo zilivyo za hovyo alafu ukubali kutoa taarifa zako na kuchukua mkopo?

Watu wanataka wenyewe kudhalilishwa. Cha ajabu wengi wanajua riba zao ni kubwa lakini bado wanaendelea kukopa kinachonishangaza wanavyolalamika utadhani walilazimishwa kuchukua hiyo mikopo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…