Kwanini app za mikopo ya mtandaoni zinatumia picha za wanawake warembo kutangaza biashara zao?

Kwanini app za mikopo ya mtandaoni zinatumia picha za wanawake warembo kutangaza biashara zao?

Nadhani branch watakuwa wamenisamehe 150k yao maana kwa riba zile tumelipana juu kwa juu
Mimi Kuna kipindi branch walinipa offer kwamba nilipe nusu . nusu nyingine wanisamehe nikawaambia haya, Mara Ile offer haipo Tena Ni matusi. Mimi nafanya kazi bandarini, wanategemea Kuna tusi sijawahi kulisikia? Hivi Hawa branch wako kihalali au wanatutukana matusi mazito wakati hawajasajiliwa na vyombo vya serikali?
 
Yaani mwanamko ana kope na kucha bandia kisha kavaa tako la bandia halafu wewe unamuona mrembo?

Mchina kapita na akili yako bwashee 😂😂
Hiyo ndio tafsiri ya urembo rafiki,inaweza isikuvutie wewe lakini ikawavutia wengine .

Fahamu kwanza urembo ni nini rafiki
 
Sababu zinafanikiwa ndio maana zinaendelea..., On top of my head bila kufanya research yoyote naweza kuja na majibu kama matano:-

Moja: kama katika demographic hio wakopaji wengi ni wanaume na ukizingatia sex sells na opposite attract basi mwanaume atavutiwa kumuangalia huyo mwanamke mrembo na akishavutiwa basi atapata na muda wa kusoma kilichoandikwa...

Mbili: wanawake wamekuwa portrayed kwamba ni wapole wenye huruma na sio matapeli (ni kina mama na dada zetu) hivyo wanachosema huenda ikawa rahisi kukubaliana nacho

Tatu: portray ya weakness ya mwanamke kwa mwanaume kwamba hata huyu nikimdhulumu au kutokulipa kwa wakati huenda nisipokee kibano (physicality)

Naweza kuendelea na nyingine ila hizo ndio nimewaza kwa haraka haraka..., Motive behind ni kukuvuta tunduni ila kwa algorithm za sasa kila ukitembelea mtandaoni unaweza kulengwa na mtu kulingana na taste yako au umri au sex..., kwahio utalishwa kile unachotaka kula ili mradi tu uweze kuuziwa wanachotaka...., kama unapenda soka ulengwa na mwanasoka, kama unapenda kina dada, hali kadhalika....
 
Wanataka ujichange ukope ila kudai yatakuja majibaba yenye mikwara
 
Nafahamu urembo ni nini, Ila kuhusu mwanamke mrembo nahitaji msaada wako kujua muonekano wake ulivyo.
kama unafahamu urembo ni nini unahitaji kujua muonekano kivipi? Mwanamke hata akichukua udongo apake kwenye macho akiwa na dhamira kuwa atapendeza au kuonekana ana mvuto wa nje huo ni urembo

Urembo haujalishi unatumia product za mchina au kwetu huku kijijini,urembo hujumuisha mavazi,kujipamba n.k so kujipendezesha kwa namna yeyote ile ni urembo hata kama haikuvutii wewe..si kila urembo utatuvutia...kuweka hizo kope zimechomoka kama wiper za gari ni urembo,kuweka kucha,matako,kujaza unyonyo ni urembo.
 
Kama unatumia sana youtube utakuwa umekutana na matangazo ya mikopo mtandao.

Mimi sikuwa nayazingatia mpaka yakaanza kuwa ya ajabu ajabu kama hivi;

Basi nikaamua kufuatilia kidogo, nikatafuta makampuni yanayomiliki haya matangazo.

Cha kushangaza utakuta vikampuni vingi vingi viko chini ya kampuni moja kubwa.

Mfano Singularity Microfinance Limited ina matangazo ya PesaX na CashX.

Dexintec Global Limited inamiliki kwanzaloan, hewamkopo, twigaloan, finiloan, na jiachie cash.

Dexintec wamechapisha matangazo 40+ ndani ya huu mwezi mmoja tu kutoka April.

Dexintec ni kampuni ya kichina, wana fanya kazi kwenye nchi maskini kama Nigeria na Pakistan

Huko mitandaoni watu wanalalamika mikopo yao inawakandamiza.

Hawa majamaa ni loan sharks. Huu ni uhalifu kabisa, kunyonya maskini kupitia mikopo.

Nimesikia mwigulu alisema bungeni huduma za mobile money kama Airtel timiza, Vodacom songesha hazina leseni, kama hao hawana, hawa kausha damu vipi?

Na wakati huo huo BOT wanasema watoa mikopo mtandao wapo chini ya makampuni yenye leseni. Ingekuwa hivyo, wangenyonya watu?

Nimewaza tu, nakaribisha wenye mawazo/maoni mbalimbali.
Ile Tulia na Jokate foundation jichanganye ndio utajua nchi inamatapeli
 
utatuvutia...kuweka hizo kope zimechomoka kama wiper za gari ni urembo,kuweka kucha,matako,kujaza unyonyo ni urembo.
Ikiwa kwako ni urembo sawa, Ila kwangu huo sio urembo.

Msimamo wangu ni kwamba uumbaji wa Mungu unajitosheleza.
 
Kuna mda watu wanakuwa kwenye tight angle mkuu, ukipiga kwa ndugu nae yupo tight. Kama kuna namna unaweza kupata mkopo wa nafuu namna hii mtu aliyebanwa hajiulizi twice.

Lakini pia hawa jamaa, business model yao ni ya udhalilishaji, unatakiwa kufanya marejesho kesho, wanaanza usumbufu leo.
Kuna kutingwa sikatai hata mimi kuna muda inakuwa hivyo lakini siwezi opt hii mikopo kama njia sahihi ya kupata msaada. Yani najua fika riba ni kubwa na marejesho ni baada ya siku 6-7 na usiporejesha unaanikwa kama nguo kambani asee hapana siwezi.
 
Mkuu mimi nimekaa na mkopo wao muda ka.a wiki 3 ila hawajatuma msg kwa ndg zangu. Unadhani wamenionea huruma??
Wezi Hawa,
Na ukisahau kurejesha hata nusu siku tu watatuma meseji Kwa ukoo wako wote kuwaambia kua eti wewe ni tapeli.
 
E
Upo sahihi kabisa mkuu hii ndio dawa yao.hawa jamaa sina huruma nao kabisa..niliwatumia mpaka email tcra ...hawa kausha damu mtu unalipa zaidi ya mara tano tena kwa wakati lakini hupandishiwi kiwango wakati sera zao zinasema ukilipa kwa wakati kiwango kinapanda.kuna siku walinipigia nikawauliza maswali hadi yule dada akanishauri nisepe tu na hiyo pesa coz ni utapeli wanafanya...haiwezekani ukope 33000 urudishe 63000 .na ukilipa hiyo 63000 bado ukikopa utapewa 33000 huu ni utapelii pia wana hiden fees ambazo hazijulikani zinapatikanaje...
Eti wanaita platform fee
 
Mkuu mimi nimekaa na mkopo wao muda ka.a wiki 3 ila hawajatuma msg kwa ndg zangu. Unadhani wamenionea huruma??
Uko app gani labda?
Pengine sio wote lakin kila mara napokea meseji za app mbali mbali watu walionisevu wamekopa
 
Juzi nimewaliza wanajiita sijui cash poa...wana majina ya ajabu ajabu mara sijui hewa mkopo
 
Matangazo yao yanaonyesha matako ya wanawake......na tunao ona mbali tunafahamu kwamba matako ni mlango wa umasikini....Sasa kwanini mtu mzima unafanya nao biashara?
 
Kama unatumia sana youtube utakuwa umekutana na matangazo ya mikopo mtandao.

Mimi sikuwa nayazingatia mpaka yakaanza kuwa ya ajabu ajabu kama hivi;

Basi nikaamua kufuatilia kidogo, nikatafuta makampuni yanayomiliki haya matangazo.

Cha kushangaza utakuta vikampuni vingi vingi viko chini ya kampuni moja kubwa.

Mfano Singularity Microfinance Limited ina matangazo ya PesaX na CashX.

Dexintec Global Limited inamiliki kwanzaloan, hewamkopo, twigaloan, finiloan, na jiachie cash.

Dexintec wamechapisha matangazo 40+ ndani ya huu mwezi mmoja tu kutoka April.

Dexintec ni kampuni ya kichina, wana fanya kazi kwenye nchi maskini kama Nigeria na Pakistan

Huko mitandaoni watu wanalalamika mikopo yao inawakandamiza.

Hawa majamaa ni loan sharks. Huu ni uhalifu kabisa, kunyonya maskini kupitia mikopo.

Nimesikia mwigulu alisema bungeni huduma za mobile money kama Airtel timiza, Vodacom songesha hazina leseni, kama hao hawana, hawa kausha damu vipi?

Na wakati huo huo BOT wanasema watoa mikopo mtandao wapo chini ya makampuni yenye leseni. Ingekuwa hivyo, wangenyonya watu?

Nimewaza tu, nakaribisha wenye mawazo/maoni mbalimbali.
Hata wewe ukishaupata huo mkopo utaanza kutafuta pisi kali ukajifariji kwanza kabla ya kutimiza lengo lako.
 
Kuna rafiki yangu huwa anafanya hii biashara ya kausha damu , aliwahi niambia kuwa hajawahi kuona biashara inayolipa na kutajirisha haraka kama hii ya kukopesha . Na kodi nadhani huwa hawalipi pamoja kuwa na riba kubwa .
 
Back
Top Bottom