RRONDO
JF-Expert Member
- Jan 3, 2010
- 55,727
- 123,094
Kwa wateja aina yako ku-survive lazima wawe kausha damu. Watanzania wengi si waaminifu wanakopa halafu wanaingia mitini halafu vijana wanalalamika hatuna mitaji. Mitaji ni mikopo ambayo mkikopa hamtaki kulipa.Hawa jamaa ni kausha damu kweli kweli, nilikopa nikarudisha kwa wakati zaidi ya mara tano sikupandishiwa kiwango zaidi ya wao kuwa na riba kubwa...nikaona ngoja na mimi niwatese nikakopa karibu aplication nne na zote sikulipa ....kilichotokea wakaanza kuwasumbua watu wangu wa jirani.. aisee niliwapandia hewani nikawaambia siwalipi kwa demage mlionifanyia ....wanajua kusumbua aiseee nilichofanya nikablock incoming unknown call zote na msg at the end waliacha kunisumbua zaidi ya kutuma msg za kunipa offer kwamba wameniongezea kiwango cha kukopa nilipe deni nipate double hahaha nabaki nacheka tu wanajua me mjinga labda nitalipa🤣🤣🤣