Kwanini app za mikopo ya mtandaoni zinatumia picha za wanawake warembo kutangaza biashara zao?

Nadhani branch watakuwa wamenisamehe 150k yao maana kwa riba zile tumelipana juu kwa juu
Mimi Kuna kipindi branch walinipa offer kwamba nilipe nusu . nusu nyingine wanisamehe nikawaambia haya, Mara Ile offer haipo Tena Ni matusi. Mimi nafanya kazi bandarini, wanategemea Kuna tusi sijawahi kulisikia? Hivi Hawa branch wako kihalali au wanatutukana matusi mazito wakati hawajasajiliwa na vyombo vya serikali?
 
Tangazo la mkopo alafu wanaweka wadada wamegeukia nyuma inahusiana nini sasa
Kwamba ukiwakopa ukachelewa kuwalipa nikama wamekufumania na mkeo utajuta kuwafahamu.
 
Yaani mwanamko ana kope na kucha bandia kisha kavaa tako la bandia halafu wewe unamuona mrembo?

Mchina kapita na akili yako bwashee 😂😂
Hiyo ndio tafsiri ya urembo rafiki,inaweza isikuvutie wewe lakini ikawavutia wengine .

Fahamu kwanza urembo ni nini rafiki
 
Sababu zinafanikiwa ndio maana zinaendelea..., On top of my head bila kufanya research yoyote naweza kuja na majibu kama matano:-

Moja: kama katika demographic hio wakopaji wengi ni wanaume na ukizingatia sex sells na opposite attract basi mwanaume atavutiwa kumuangalia huyo mwanamke mrembo na akishavutiwa basi atapata na muda wa kusoma kilichoandikwa...

Mbili: wanawake wamekuwa portrayed kwamba ni wapole wenye huruma na sio matapeli (ni kina mama na dada zetu) hivyo wanachosema huenda ikawa rahisi kukubaliana nacho

Tatu: portray ya weakness ya mwanamke kwa mwanaume kwamba hata huyu nikimdhulumu au kutokulipa kwa wakati huenda nisipokee kibano (physicality)

Naweza kuendelea na nyingine ila hizo ndio nimewaza kwa haraka haraka..., Motive behind ni kukuvuta tunduni ila kwa algorithm za sasa kila ukitembelea mtandaoni unaweza kulengwa na mtu kulingana na taste yako au umri au sex..., kwahio utalishwa kile unachotaka kula ili mradi tu uweze kuuziwa wanachotaka...., kama unapenda soka ulengwa na mwanasoka, kama unapenda kina dada, hali kadhalika....
 
Wanataka ujichange ukope ila kudai yatakuja majibaba yenye mikwara
 
Nafahamu urembo ni nini, Ila kuhusu mwanamke mrembo nahitaji msaada wako kujua muonekano wake ulivyo.
kama unafahamu urembo ni nini unahitaji kujua muonekano kivipi? Mwanamke hata akichukua udongo apake kwenye macho akiwa na dhamira kuwa atapendeza au kuonekana ana mvuto wa nje huo ni urembo

Urembo haujalishi unatumia product za mchina au kwetu huku kijijini,urembo hujumuisha mavazi,kujipamba n.k so kujipendezesha kwa namna yeyote ile ni urembo hata kama haikuvutii wewe..si kila urembo utatuvutia...kuweka hizo kope zimechomoka kama wiper za gari ni urembo,kuweka kucha,matako,kujaza unyonyo ni urembo.
 
Ile Tulia na Jokate foundation jichanganye ndio utajua nchi inamatapeli
 
utatuvutia...kuweka hizo kope zimechomoka kama wiper za gari ni urembo,kuweka kucha,matako,kujaza unyonyo ni urembo.
Ikiwa kwako ni urembo sawa, Ila kwangu huo sio urembo.

Msimamo wangu ni kwamba uumbaji wa Mungu unajitosheleza.
 
Kuna kutingwa sikatai hata mimi kuna muda inakuwa hivyo lakini siwezi opt hii mikopo kama njia sahihi ya kupata msaada. Yani najua fika riba ni kubwa na marejesho ni baada ya siku 6-7 na usiporejesha unaanikwa kama nguo kambani asee hapana siwezi.
 
Mkuu mimi nimekaa na mkopo wao muda ka.a wiki 3 ila hawajatuma msg kwa ndg zangu. Unadhani wamenionea huruma??
Wezi Hawa,
Na ukisahau kurejesha hata nusu siku tu watatuma meseji Kwa ukoo wako wote kuwaambia kua eti wewe ni tapeli.
 
E
Eti wanaita platform fee
 
Mkuu mimi nimekaa na mkopo wao muda ka.a wiki 3 ila hawajatuma msg kwa ndg zangu. Unadhani wamenionea huruma??
Uko app gani labda?
Pengine sio wote lakin kila mara napokea meseji za app mbali mbali watu walionisevu wamekopa
 
Juzi nimewaliza wanajiita sijui cash poa...wana majina ya ajabu ajabu mara sijui hewa mkopo
 
Matangazo yao yanaonyesha matako ya wanawake......na tunao ona mbali tunafahamu kwamba matako ni mlango wa umasikini....Sasa kwanini mtu mzima unafanya nao biashara?
 
Hata wewe ukishaupata huo mkopo utaanza kutafuta pisi kali ukajifariji kwanza kabla ya kutimiza lengo lako.
 
Kuna rafiki yangu huwa anafanya hii biashara ya kausha damu , aliwahi niambia kuwa hajawahi kuona biashara inayolipa na kutajirisha haraka kama hii ya kukopesha . Na kodi nadhani huwa hawalipi pamoja kuwa na riba kubwa .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…