Kwa mtazamo wangu thamani hutokana na
1. Ugumu wa wenye ardhi kuuza au urahisi, utashangaa kiwanja ni ghali arusha kuliko dar japo dar kuna maendeleo zaidi sababu watu wa kaskazini hawana utamaduni wa kuuza ardhi.
2. Jamii iliyopo - mbagala imejaa jamii ya chini na pengine watu wenye asili ya kusini hivyo hata anaeuza na kununua wanaendana na hali halisi ya jamii husika. Pia kwao ardhi haina thamani sana ukizingatia hata huko kusini ardhi haitumiki sana kwenye uzalishaji kama kilimo.
3. Huduma muhimu kama usafiri, barabara, maji, umeme, shopping centers, mabaa, migahawa, mashule, mahospitali na miundo mbinu kwa ujumla. Mbagala inakosa baadhi ya hii miundo mbinu muhimu kuvutia wakazi.
4. Usalama
5. Mtazamo/brand au haiba - mbagala inasifa ya kuwa sehemu ya hali ya chini hata diamond aliimba "tatizo kwetu mbagala". Hii imewaaminisha watu wenye kipato kuona mbagala sio eneo la kuishi, kwa kuwa liko "branded" kama eneo.la kimaskini na hali ya chini.
6. Mipango miji....sijui kama kumepimwa na kupangwa au ni "squata" japo hili tatizo la karibia tanzania yote.
-