Kwanini ardhi ya Mbagala haina thamani?

Ahaa hiyo list sasa,gurumo alihamia ubungo makubuli,hapo ukimtoa fella waliobaki siwezi kushangaa hata ungeniambia wanakaa tandali kwa bi nyau,chegge,mh temba na inspector walihama huko kitambo
 
Usijali, acha tuendelee na mada husika mezani.
 
Kama ungezaliwa Kurasini usingekuwa mshamba.

Hapo Kurasini upo hostel ukiwa ni mwanafunzi wa ualimu hapo DUCE.
Duce imeanza kuitwa hivyo nikiwa nimeshabarehe,kilikuwa chuo cha ualimu chang'ombe zamani kama hujui
 
Ahaa hiyo list sasa,gurumo alihamia ubungo makubuli,hapo ukimtoa fella waliobaki siwezi kushangaa hata ungeniambia wanakaa tandali kwa bi nyau,chegge,mh temba na inspector walihama huko kitambo
Temba kwao na alipojenga ni hapo Chang'ombe Ununio, nyuma ya Breweries.
Unawakumbuka spider

Chege ni mtoto wa Kurasini toka kitambo, unakumbuka kundi la Manyani camp

Inspector karudi mikoroshini, kumbuka alizaliwa na kukulia mtaa wa Wailes Temeke.

Hapo sijaweka wasomi na watu wengine mashuhuri pamoja na mabalozi waliojenga chamazi na wanaishi huko[emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38]
 
Duce imeanza kuitwa hivyo nikiwa nimeshabarehe,kilikuwa chuo cha ualimu chang'ombe zamani kama hujui
Mbagala pia imejaa, ukanunue Mkuranga huko[emoji38][emoji38][emoji38][emoji38][emoji38]
 
Kwan Diamond anasemaje?
Diamond amezaliwa na kukulia Tandale huko.

Aliimba Mbagala ikiwa ni sehemu maarufu ila uchafu Tandale ni kuchafu zaidi, paovyo zaidi.

Ni sawasawa na hapo Mbeya Watoto wa Iyunga kupasifia Iyunga na Nzovye ila maeneo ya kisasa, ya kishua ni Iwambi, New forest, Uzunguni na kidogo Isyesye
 
Chamazi imejaa wachezaji wa azam ,na mzee mmoja alikuwa RC dodoma enzi za jiwe jordan rugimbana mbagala inabebwa na kijichi tu
 
Kwa hiyo wewe unataka Wazaramo wasifie?

Ila Wandengereko, Wamatumbi, Wanyagatwa na watu kutoka kusini ndio hawafai?
 
Kwa hiyo wewe unataka Wazaramo wasifie?

Ila Wandengereko, Wamatumbi, Wanyagatwa na watu kutoka kusini ndio hawafai?
Mkuu mimi naongelea kabila langu tu. Hao wengine siwezi kuwajua na sijui utamaduni wao kiundani.
Mtu anayeongelea kitu asichokijua na bila ya uhakika ni mjinga asiyejitambua.
 
Sawasawa
 
Chamazi imejaa wachezaji wa azam ,na mzee mmoja alikuwa RC dodoma enzi za jiwe jordan rugimbana mbagala inabebwa na kijichi tu
Nipe sababu tatu, kwa nini inabebwa na kijichi?

Wakati eneo la kuanzia kizuiani mpaka Torori ndilo lenye shughuli nyingi za kiuchumi?

Vikunai unaifahamu?

Mgeni nani?

Maji matitu? Nayo ipo hovyo.

N.B Mbagala Misheni, Mbagala Mwanamtoti pia ni sehemu ya kijichi ikiwa kijichi ni sehemu ya kata kwenye Tarafa ya Mbagala
 
Kwa mtazamo wangu thamani hutokana na
1. Ugumu wa wenye ardhi kuuza au urahisi, utashangaa kiwanja ni ghali arusha kuliko dar japo dar kuna maendeleo zaidi sababu watu wa kaskazini hawana utamaduni wa kuuza ardhi.

2. Jamii iliyopo - mbagala imejaa jamii ya chini na pengine watu wenye asili ya kusini hivyo hata anaeuza na kununua wanaendana na hali halisi ya jamii husika. Pia kwao ardhi haina thamani sana ukizingatia hata huko kusini ardhi haitumiki sana kwenye uzalishaji kama kilimo.

3. Huduma muhimu kama usafiri, barabara, maji, umeme, shopping centers, mabaa, migahawa, mashule, mahospitali na miundo mbinu kwa ujumla. Mbagala inakosa baadhi ya hii miundo mbinu muhimu kuvutia wakazi.

4. Usalama

5. Mtazamo/brand au haiba - mbagala inasifa ya kuwa sehemu ya hali ya chini hata diamond aliimba "tatizo kwetu mbagala". Hii imewaaminisha watu wenye kipato kuona mbagala sio eneo la kuishi, kwa kuwa liko "branded" kama eneo.la kimaskini na hali ya chini.

6. Mipango miji....sijui kama kumepimwa na kupangwa au ni "squata" japo hili tatizo la karibia tanzania yote.

-
 
Huo ukanda wote sijawahi kuuelewa bara nikaishi mlandizi au kibaha
Sikiliza wewe wakuja, ni vizuri ukinunua njia ya kwenda kwenu.

Huo ndio Utamaduni, ila kutokuuelewa hakukufanyi kudunisha eneo.

Fananisha Mbagala na maeneo kama Bunju, Mbezi mwisho au Kibamba, Gongo la Mboto halafu tuone wapi Kuna maendeleo kuzidi
 
Umeona hata tukianza kuichambua Kimara utagundua Dar es salaam inafanana tu.
 
Sikiliza wewe wakuja, ni vizuri ukinunua njia ya kwenda kwenu.

Huo ndio Utamaduni, ila kutokuuelewa hakukufanyi kudunisha eneo.

Fananisha Mbagala na maeneo kama Bunju, Mbezi mwisho au Kibamba, Gongo la Mboto halafu tuone wapi Kuna maendeleo kuzidi
Sikiliza wewe wakuja, ni vizuri ukinunua njia ya kwenda kwenu.

Huo ndio Utamaduni, ila kutokuuelewa hakukufanyi kudunisha eneo.

Fananisha Mbagala na maeneo kama Bunju, Mbezi mwisho au Kibamba, Gongo la Mboto halafu tuone wapi Kuna maendeleo kuzidi
Njia ya kwetu unaijua,?usinipangie mi sina kwetu zaidi ya Dar
 
Mbona masanja kagongewa ni muislam
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…