Wapo Wamakonde kibao kutoka Mtwara waliokuwa wanachanja chale aliyekudanganya sijui nani?
Kifupi enzi za milki ya Kilwa kulikuwa na Wamakonde wengi kutoka mji wa Mikindani walioenda kuomba katika mji wa Kilwa.
Baadae Mikindani ikakua na Wamakonde waliopo Mwambao mwa bahari kupokea dini ya kiislamu na kuacha tamaduni zao hasa kuchanja.
Hivyo kujulikana kama Wamakonde Marhaba ambao wanatofautiana na wale waliopo bara maeneo kama Masasi, Nangomba, Nanyumbu, Newala na Nanyamba.
Hali hii ilitokea hivyo hivyo na Mozambique kwa jamii za kimakonde zilizopo Pwani maeneo kama Jimbo la Pemba.
Hivyo kuweka ndonya na kuchanja ni Utamaduni wa Wamakonde wote ila kwa Sasa wameuacha.
N.B Lindi wenyeji ni Wamwera
Kilwa wenyeji ni Wamatumbi na Wangindo.
Tunduru wenyeji ni Wayao
N.B hii PHD ulikaa darasani au ulinunua?