Huwa nikipiga simu huduma kwa wateja akipokea mwanamke nakata napiga tena hadi apokee mwanaume.
Nilicho gundua akipokea wanamke majibu yake asilimia ndogo yakatatua tatizo nilopigia simu(Wanaonekana wengi sio watalamu wa hiyo fani )
Mambo mengi hawayajui na hawana kauli nzuri.
Kwenye NIDA huko ndo usiseme yaani uko foleni unaona mwenzako unavyofokewa kwa jambo la kawaida nawe unasubiria kuangalia zamu yako unafokewa kwa lipi.
Wanakua na viburi mana watu wa juu yao ndo wanaowapa kichwa na ni sisi wanaume.
Jichanganye ujitie una msemea kumbe unaongeza kaa la moto.
Ila nakumbuka kipindi nasoma UDSM kuna Madam mmoja alikuwa msaidizi wa Principle wa CONAS yule madam Mungu Amlaze mahali pema , maana katika hudumiwa na wanawake katika maofisi sijawa hudumia kwa bashasha ns kauli nzuri kama ile tena sio mara moja ni kila nilipowahi fila ofinisi pale na sio mimi tuu ilikuwa kila mtu alohudumiwaga nae hakuacha kusifia.
Wako wachache sana wenye roho za kujua anapaswa kuwaje.
Niliumia siku moja natembea pale naambiwa alifariki R.I.P madam