Kwanini ATM za Mabenki zinauliza kama tunataka Risiti wakati ni haki ya mteje kama kununua bidhaa?

Kwanini ATM za Mabenki zinauliza kama tunataka Risiti wakati ni haki ya mteje kama kununua bidhaa?

jodac

JF-Expert Member
Joined
Apr 9, 2014
Posts
339
Reaction score
371
Naiomba TRA ishughulikie hili, hivi ni kwanini mashine za ATM mfano NMB, CRDB n.k hazitoi risiti pasipo kuuliza? Ilihali akifanya hivyo mfanya biashara kariakoo anakamatwa .
Kwanini risiti za ATM kuzipata kunamakato ilihali kudai risiti ni haki ya mteja?
 
Ukiuza/Ukinunua Dai Risiti
TRA Haraka Waambieni Watoe Hizi Risiti Pia Zisiwe Na Makato
Huduma Nyingi Zimekaa Kula Pesa Ya Mteja Simbaking, Wakala

Siku Hizi Kujiunga Simbaking Banks Zote Wanalazimisha
Wafanye Huduma Zote Bure Tutajiunga Haraka
 
Zile risiti ni kwaajiri ya kumbukumbu tu. Kuna baadhi ya kadi huwezi jua salio bila hio risiti mf prepaid card, ndio maana wanakuuliza. Kama nina card ya kawaida nitapata kujua salio kwa simbanking au app.

Sioni sehemu ya TRA hapo.
 
Naiomba TRA ishughulikie hili, hivi ni kwanini mashine za ATM mfano NMB, CRDB n.k hazitoi risiti pasipo kuuliza? Ilihali akifanya hivyo mfanya biashara kariakoo anakamatwa .
Kwanini risiti za ATM kuzipata kunamakato ilihali kudai risiti ni haki ya mteja?
Mzee unachanganya mambo. Risiti za ATM siyo risiti za EFD ni kama bank slip tu, ikiwa unahitaji kwa ajili ya kumbukumbu zako. Lakini kama hau file kumbukumbu huna haja ya kuchukua risiti. Maana utaitupa kwenye dustbin tu.
 
Naiomba TRA ishughulikie hili, hivi ni kwanini mashine za ATM mfano NMB, CRDB n.k hazitoi risiti pasipo kuuliza? Ilihali akifanya hivyo mfanya biashara kariakoo anakamatwa .
Kwanini risiti za ATM kuzipata kunamakato ilihali kudai risiti ni haki ya mteja?
Kaa ukijua ukichukua risiti wanakata 400/=tshs mi salio huwa naangalia bure kwenye app ila ATM sitoi risiti
 
Nami niulize.
  • Unatoa fedha yako makato ya nini tena?
  • Unatoa mshahara wako benki, ambao tayari umekatwa kodi, ila unakatwa tena unapoutoa, makato ya nini tena?
Nchi imejaa double taxation kinoma ni wakati sasa hii miamala ya fedha tutunze kumbukumbu tuwe tunapeleka tra kudai return.

Mshahara unaingia benki unakatwa kodi(paye)
Unahamisha hiyo Pesa ambayo imeshakatwa kodi kutoka benki kwenda kwenye mtandao wako wa simu mfano Mpesa wanakata tena.
Unatuma Pesa ambayo imekatwa kodi Mara mbili kutoka mpesa kwenda kwa mke wanakata tena Mara ya tatu huyo mke anaenda kuwithdraw inakatwa tena Mara ya nne hapo ni miamala hakuna biashara unayofanya kuwa unapata faida Asa hapo unabakiwa na nini?
 
Naiomba TRA ishughulikie hili, hivi ni kwanini mashine za ATM mfano NMB, CRDB n.k hazitoi risiti pasipo kuuliza? Ilihali akifanya hivyo mfanya biashara kariakoo anakamatwa .
Kwanini risiti za ATM kuzipata kunamakato ilihali kudai risiti ni haki ya mteja?
Ukichukua risiti makato yanaongezeka
 
Back
Top Bottom