DR SANTOS
JF-Expert Member
- Mar 11, 2019
- 12,846
- 28,106
Kwenye app crdb wanakata 300 kila ukiangalia salioKaa ukijua ukichukua risiti wanakata 400/=tshs mi salio huwa naangalia bure kwenye app ila ATM sitoi risiti
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kwenye app crdb wanakata 300 kila ukiangalia salioKaa ukijua ukichukua risiti wanakata 400/=tshs mi salio huwa naangalia bure kwenye app ila ATM sitoi risiti
Naiomba TRA ishughulikie hili, hivi ni kwanini mashine za ATM mfano NMB, CRDB n.k hazitoi risiti pasipo kuuliza? Ilihali akifanya hivyo mfanya biashara kariakoo anakamatwa .
Kwanini risiti za ATM kuzipata kunamakato ilihali kudai risiti ni haki ya mteja?
Naiomba TRA ishughulikie hili, hivi ni kwanini mashine za ATM mfano NMB, CRDB n.k hazitoi risiti pasipo kuuliza? Ilihali akifanya hivyo mfanya biashara kariakoo anakamatwa .
Kwanini risiti za ATM kuzipata kunamakato ilihali kudai risiti ni haki ya mteja?
Benki ya kijani kwa makato ni hatari kila mmoja anajua hilo NMB ni bure kuangalia salio kupitia appKwenye app crdb wanakata 300 kila ukiangalia salio
Mbona Mimi naangalia Bure au wanakata mda gani ?Kwenye app crdb wanakata 300 kila ukiangalia salio
Angalia kwa makini labda huoni kwa sababu una figure nyingiMbona Mimi naangalia Bure au wanakata mda gani ?
Hakuna Cha kuokoa mbona kwenye Mafuta zinatoka automatically?Sababu ni kuokoa mazingira, inawezekana huitaji risiti. Hawana nia mbaya.
Risiti ya benki sio bure.Naiomba TRA ishughulikie hili, hivi ni kwanini mashine za ATM mfano NMB, CRDB n.k hazitoi risiti pasipo kuuliza? Ilihali akifanya hivyo mfanya biashara kariakoo anakamatwa .
Kwanini risiti za ATM kuzipata kunamakato ilihali kudai risiti ni haki ya mteja?
Wazo zuri. Hapo kuna double standard huyu mfanya biashara wa Kariakoo analazimishwa kutoa risiti alafu huwa wafanya biayara ya fedha wao risiti ni hadi uangalie kwenye App.Teknolojia imekuwa risiti unaweza kuzipata kiganjani muda wowote kwenye app za benki, tunapunguza kujaza karatasi
Poor Brain Huyo....Ukitoa pesa yako manunuzi gani umefanya?
HapanaWanatakiwa waiweke kwenye gharama za uendeshaji wa account ili kutimiza takwa la kisheria.
Nia yao mbaya ni kuuza lisitiSababu ni kuokoa mazingira, inawezekana huitaji risiti. Hawana nia mbaya.
Sio hivyo mkuu. Kuomba risiti ni sawa na KUULIZA SALIO. Na kuuliza salio sio bure. Mteja hukatwa pesa kiasi cha Tsh 1500 anapouliza salio. Kwa hiyo, ukiomba risiti unakatwa Tsh 1500. Benki wanakuuliza ili kuomba ridhaa yako kama upo tayari kukatwa kiasi hicho ili wakuchapie salio kwenye risiti. Ndio maana ukiwa na pesa pungufu kwenye akaunti unapotoa pesa na kuomba risiti, ,unaambiwa salio lako halitoshi. Lakini ukitoa bila risiti, pesa zinatoka bila shida. Hii ndio sababu ya kuulizwa kama unahitaji risiti.Sababu ni kuokoa mazingira, inawezekana huitaji risiti. Hawana nia mbaya.
Sheria za usimamizi wa huduma za kifedha ni tofauti.Ila nisheria kuto risti bila gharama za ziada kwa kila biashara inayo fanyika sindio?
Mkuu ristii haitolewi bure. Unaulizwa kama unahitaji risiti ili benki ijue kama upo tayari kukatwa pesa za kuuliza salio unapomba risiti. Elewa kuomba risiti ni sawa na kuuliza salio.ATM za mabenki zinauliza kama unataka risiti kwa sababu ya sababu kadhaa muhimu:
1. Haki ya Mteja: Ni haki ya kila mteja kupata risiti ili kuthibitisha muamala uliofanyika. Risiti inasaidia katika kudhibitisha kwamba umefanya malipo au umechukua fedha.
2. Usalama wa Kifedha: Risiti inaweza kusaidia katika kufuatilia matumizi na kusaidia katika kuzuia udanganyifu. Ikiwa kuna tatizo na muamala, risiti inatoa ushahidi wa kile kilichotokea.
3. Urahisi wa Kufuatilia: Kwa kutoa chaguo la kupokea risiti, ATM inawapa wateja uwezo wa kuzingatia matumizi yao ya kila siku na kurahisisha hesabu za kifedha.
4. Kuhakikisha Faragha: Baadhi ya wateja wanaweza kutaka kutopewa risiti kwa sababu ya faragha au kwa sababu wanataka kuepuka kuandika taarifa zao za kifedha.
5. Sera za Benki: Mabenki yanaweza kuwa na sera tofauti kuhusu kutoa risiti, na hivyo ni muhimu kwao kutoa chaguo kwa wateja ili waweza kuchagua.
Kwa hiyo, ingawa ni haki ya mteja kupata risiti, chaguo la kupokea risiti linawapa wateja udhibiti zaidi juu ya taarifa zao za kifedha.