Kwanini awamu hii ya 6 Muungano umekua hati hati kuvunjika?? kwanini hii hali haijawai kuwa moto hivi miaka ya nyuma

Kwanini awamu hii ya 6 Muungano umekua hati hati kuvunjika?? kwanini hii hali haijawai kuwa moto hivi miaka ya nyuma

Muungano wa kiwaki,, wazanzibar wanafaidi zaidi kuliko wabala,, lakini hawajielewi ni kama mtoto pendwa kwenye familia kila saa nyee nyee nyee,, mwishowe tumeichoka sasa,,
kuna vitu vya kurekebisha
 
Wale wapumbavu wenye vichwa visivyo na visogo kama redio za kichina wanaona dada yao yuko kwenye mpini ndio wanatikisa kibiriti lakini dada yao hawezi kubali hii keki imtoke mikononi kirahisi hivyo, lakini pia sisi Watanganyika wengi tuna chukizwa na utawala wa hovyo uliopo
Eti dada yao
 
Kwasababau mzanzibari kauza bandaru za tanganyika,kauza mapori ya tanganyika kwa wajomba zake waarabu.
 
Wakuu nauliza tu,,,,
Ishu za muungano imekua moto kuliko ishu yoyote ile kuna nn??
Nini kinachochea hii movement!!
Ule mwiko was Nyerere was mvaa kanzu akiwa namba moja lazima atokee visiwani kama Mzee mwinyi ulivunjwa baada ya watoto was mjini kushika hatamu!!

Sasa bas ndoto ya namba Moja kutoka visiwani ilikufa kibudu ,baada ya mzilankende kwenda halafu huyu kushika,Imeleta uchungu sana Kwa Yale anayofanya ambayo wanaccm wa bara wametema nyongo kupitia Lisu!!"Mzanzibari anauza Ardhi ya Tanganyika" Sasa watanganyika wanakiona Cha moto Toka Kwa was visiwani na wao wanaanza kuiona chungu ya Muungano!!

Sasa kisiwa kinapokea pesa nyingi za mkopo tofauti na zamani!nongwa imezidi ndio maana Muungano shakani!!

Sisi wengine tunatilia shaka kwamba yawezekana kwamba huyu Mama ni Aboud Jumbe aliechangamka na Bahati nzuri hakuna Maalim seif was Leo was kumsaliti Kwa Baba was taifa!!

Leo Ally Hapi anasisitiza eti "Nchi ipo salama" Hadi najiuliza kwani lini imekua hatarini !!!?

Nadhani walio jikoni wanajua zaidi yangu!!
 
Wanakuambia ni temper, wazanzibar wanaongea utumbo na watanganyika wanajibu maini ! Hali ni tete kwa kweli. Hakuna wa kukemea matamko hayo yanayotishia kuvunjika kwa muungano. Wanaharakati na wanasiasa wanaongea bila hofu kuhusu muungano, ni mbwambwa tu, wazee wako kimya hawakemei mtifuano huo
 
hii suala la muungano siyo Mtanganyika au Mzanzibar anayeridhika nayo, ni vyema serikali ikarekebisha vipengele kwenye huo muungano ili wananchi wa JMT waridhike.

mbona ni easy tu.!, kwani kuna siri gani?
Hakuna siri. Ila kuna uroho wa madaraka
 
Back
Top Bottom