Kwanini baadhi ya kesi hupelekwa Mahakama za chini ambazo hazina mamlaka ya kusikiliza kesi za aina hiyo?

mwanamwana

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2011
Posts
1,309
Reaction score
4,798
Salaam wakuu,

Mara nyingi tumekuwa tukisikia kuwa watuhumiwa fulani wamesomewa Mashtaka lakini hawakupaswa kujibu CHOCHOTE kwa kuwa Mahakama waliyopelekwa haina uwezo/mamlaka ya kusikiliza kesi husika.

Kwa mifano hai wengi tunatambua kuwa Mahakama Kuu ndio imepewa nguvu, uwezo/mamlaka ya kusikiliza kesi ya Mauji, sawa Mahakama ya Hakimu Mkazi na Mahakama ya Wilaya inaweza kupewa nguvu lakini kwasababu ambazo itaonekana zinafaa.

Kesi ya hivi karibuni inayowakabili watu Tisa kwa mauaji ya mtoto Asimwe Novath, watuhumiwa walifikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Bukoba ambayo ilisema Mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo, hivyo watuhumiwa hawapaswi kujibu chochote.

Nachohitaji kufahamu ni
  • Pamoja na sheria kuwa wazi, kwanini mtuhumiwa wa mauaji apelekwe Mahakama za chini zisizo na uwezo wa kusikiliza shauri hilo? au Ni sahihi mtuhumiwa wa mauaji kushtakiwa mahakama za chini?
  • Nini Faida na hasara za mchakato wa kesi hiyo kuanzia mahakama za chini?
  • Mchakato huu hauwezi kusababishwa kukiukwa kwa haki za msingi za mtuhumiwa?
  • Mchakato huu hauwezi kusababisha kesi kuchukua muda mrefu kutamatika?
  • Mahakama ya chini inaweza kupewa nguvu ya kusikiliza kesi ambayo haina mamlaka ya kesi hiyo? Kama ndiyo, vigezo vipo kwa mujibu wa sheria gani?

Pia soma
Maelezo kutoka kwa Wakili Yakubu
 
Attachments

Naona hakuna aliyekujibu ila iko hivi iyo ipo kisheria inaitwa commital proceding, na sababu kuu ya kesi kupelekwa kuanzia mahakama ya chini ni kuipa nafasi jamhuri kukusanya ushahidi ili kesi ikifika mahakama yenye mamlaka isije kugota tena kwa kusosekana ushahidi
 
Kuna kesi ya kikatiba inaendela huko mahakamani ikanikumbusha jinsi ambavyo huwa tunaona taarifa mtuhumiwa mfano wa mauaji kafikishwa mahakamani kasomewa mashitaka halafu inasemwa hakutakiwa kujibu chochote kwa sababu mahakama haina uwezo wa kusikiliza kesi yake!

Sasa maana ya waendesha mashitaka kuipeleka hiyo kesi katika hiyo mahakama isiyo na uwezo wa kusikiliza kesi huwa ni nini hasa?!

Screenshot_20240729-145701_X.jpg
 
Naona hakuna aliyekujibu ila iko hivi iyo ipo kisheria inaitwa commital proceding, na sababu kuu ya kesi kupelekwa kuanzia mahakama ya chini ni kuipa nafasi jamhuri kukusanya ushahidi ili kesi ikifika mahakama yenye mamlaka isije kugota tena kwa kusosekana ushahidi
Hapa sijaelewa, kwani kumfikisha mtuhumiwa hiyo mahakama ya mwanzo kunawasaidiaje polisi kukusanya ushahidi??
 
Sababu ya makosa ya jinai ambayo yanatakiwa kusikilizwa Mahakama Kuu kupitia kwanza kwenye Mahakama ya chini ni utaratibu wa kisheria unaitwa COMMITTAL PROCEEDINGS (MWENENDO KABIDHI).

Inafanyika kwa makosa yote ambayo yanatakiwa kusikilizwa na Mahakama Kuu.
Ukitaka kuyajua hayo makosa soma Jedwali (schedule) nyuma ya sheria inaitwa Criminal Procedure Act, au kwa kifupi “CPA” CHAPTER 20. (Kwa kiswahili inaitwa, sheria ya Mwenendo wa makosa ya Jinai, Sura ya 20). Ipo hata google unaweza ku download.

Mfano kesi ya mauaji inatakiwa kusikilizwa Mahakama Kuu, lakini haitafunguliwa
Mahakama Kuu moja kwa moja, mpaka kwanza ipitie Mahakama ya Wilaya au
Mahakama ya Hakimu Mkazi kwa ajili ya committal proceedings.

Wala haifanyiki bahati mbaya ni utaratibu kabisa umewekwa kwenye sheria. Kwamba makosa ambayo yanapaswa kusikilizwa na Mahakama Kuu, lazima mtuhumiwa apelekwe kwanza Mahakama ya chini (Mahakama ya Wilaya au Mahakama ya Hakimu Mkazi) ili kufanyiwa committal proceedings.

Baada ya upelelezi kukamilika watakuja kumsomea mshtakiwa maelezo ya ushahidi. Baada ya hapo ile Mahakama ya chini itamkabidhi au kumpeleka (inam-commit) yule mshtakiwa Mahakama Kuu kwenda kuanza kusikiliza kesi yake.
 
Ikitokea mtuhumiwa katika mahakama ambayo hatakiwi kujibu chochote kama sheria inavyotaka na mtuhumiwa huyo akajibu chochote labda akasema "sio kweli Mheshimiwa", kisheria imekaaje hiyo?
 
Ikitokea mtuhumiwa katika mahakama ambayo hatakiwi kujibu chochote kama sheria inavyotaka na mtuhumiwa huyo akajibu chochote labda akasema "sio kweli Mheshimiwa", kisheria imekaaje
Atajibuje sasa na hajaulizwa

Unajibu ukiulizwa "Mshtakiwa kweli si kweli?"

Ukijibu nje ya utaratibu hawa record (hawaandiki)
 
Sababu ya makosa ya jinai ambayo yanatakiwa kusikilizwa Mahakama Kuu kupitia kwanza kwenye Mahakama ya chini ni utaratibu wa kisheria unaitwa COMMITTAL PROCEEDINGS (MWENENDO KABIDHI).

Inafanyika kwa makosa yote ambayo yanatakiwa kusikilizwa na Mahakama Kuu.
Ukitaka kuyajua hayo makosa soma Jedwali (schedule) nyuma ya sheria inaitwa Criminal Procedure Act, au kwa kifupi “CPA” CHAPTER 20. (Kwa kiswahili inaitwa, sheria ya Mwenendo wa makosa ya Jinai, Sura ya 20). Ipo hata google unaweza ku download.

Mfano kesi ya mauaji inatakiwa kusikilizwa Mahakama Kuu, lakini haitafunguliwa
Mahakama Kuu moja kwa moja, mpaka kwanza ipitie Mahakama ya Wilaya au
Mahakama ya Hakimu Mkazi kwa ajili ya committal proceedings.

Wala haifanyiki bahati mbaya ni utaratibu kabisa umewekwa kwenye sheria. Kwamba makosa ambayo yanapaswa kusikilizwa na Mahakama Kuu, lazima mtuhumiwa apelekwe kwanza Mahakama ya chini (Mahakama ya Wilaya au Mahakama ya Hakimu Mkazi) ili kufanyiwa committal proceedings.

Baada ya upelelezi kukamilika watakuja kumsomea mshtakiwa maelezo ya ushahidi. Baada ya hapo ile Mahakama ya chini itamkabidhi au kumpeleka (inam-commit) yule mshtakiwa Mahakama Kuu kwenda kuanza kusikiliza kesi yake.
Committal proceedings ni nini??
 
Usizunguke sana
Sema hivi, hizi ni sheria za jinai za United Kingdom tumezikopi wakati tunapewa uhuru, na ndio zinafata huu utaratibu

Sababu ya makosa ya jinai ambayo yanatakiwa kusikilizwa Mahakama Kuu kupitia kwanza kwenye Mahakama ya chini ni utaratibu wa kisheria unaitwa COMMITTAL PROCEEDINGS (MWENENDO KABIDHI).

Inafanyika kwa makosa yote ambayo yanatakiwa kusikilizwa na Mahakama Kuu.
Ukitaka kuyajua hayo makosa soma Jedwali (schedule) nyuma ya sheria inaitwa Criminal Procedure Act, au kwa kifupi “CPA” CHAPTER 20. (Kwa kiswahili inaitwa, sheria ya Mwenendo wa makosa ya Jinai, Sura ya 20). Ipo hata google unaweza ku download.

Mfano kesi ya mauaji inatakiwa kusikilizwa Mahakama Kuu, lakini haitafunguliwa
Mahakama Kuu moja kwa moja, mpaka kwanza ipitie Mahakama ya Wilaya au
Mahakama ya Hakimu Mkazi kwa ajili ya committal proceedings.

Wala haifanyiki bahati mbaya ni utaratibu kabisa umewekwa kwenye sheria. Kwamba makosa ambayo yanapaswa kusikilizwa na Mahakama Kuu, lazima mtuhumiwa apelekwe kwanza Mahakama ya chini (Mahakama ya Wilaya au Mahakama ya Hakimu Mkazi) ili kufanyiwa committal proceedings.

Baada ya upelelezi kukamilika watakuja kumsomea mshtakiwa maelezo ya ushahidi. Baada ya hapo ile Mahakama ya chini itamkabidhi au kumpeleka (inam-commit) yule mshtakiwa Mahakama Kuu kwenda kuanza kusikiliza kesi yake.
Commit together with a committal bundle
 
Back
Top Bottom