Kwanini baadhi ya makanisa yanaweka mabango kuwaasa waumini wavae kwa heshima wakati kinachoangaliwa ni roho na sio mavazi?

Huko ni kukosa mafunzo sahihi ya sheria ya mavazi ndio maana wanalazimika kuweka matangazo juu ya mavazi, sisi wakristo inajulikana wazi kwamba kinachoangaliwa ni roho sio mavazi, kuna haja ipi ya kuweka haya mabandgo, uliona wapi misikitini wanaweka matangazo ya aina hiyo?

Nijuavyo kinachoangaliwa ni roho na sio mavazi, haya makatazo yalishapitwa na muda ni mambo ya agano la kale lililokataza kula wanyama kama mbwa na nguruwe, kunywa pombe, kuvaa mavazi yanyositiri, kukataza kuchonga nywele na ndevu, n.k.

Kwani Yesu Kristo na Bikira Maria na wengine wakati wa Yesu waliofuata mafundisho yake walikuwa wanavaaje?
 
Huko ni kukosa mafunzo sahihi ya sheria ya mavazi ndio maana wanalazimika kuweka matangazo juu ya mavazi, sisi wakristo inajulikana wazi kwamba kinachoangaliwa ni roho sio mavazi, kuna haja ipi ya kuweka haya mabandgo, uliona wapi misikitini wanaweka matangazo ya aina hiyo?

Nijuavyo kinachoangaliwa ni roho na sio mavazi, haya makatazo yalishapitwa na muda ni mambo ya agano la kale lililokataza kula wanyama kama mbwa na nguruwe, kunywa pombe, kuvaa mavazi yanyositiri, kukataza kuchonga nywele na ndevu, n.k.

'Nyumba yangu ni Nyumba ya Sala.'
 
Hiyo nguo haina tatizo. Hata akiingia kanisa lolote hakuna atakae mshangaa wala kumrudisha.
Makanisani wapo wanaume wanaojitambua sio wale wengine kule hata akiona kidole anadinda, maana muda wote wanawaza ngono.
Nikuelimishe ya kwamba vazi hilo halisitiri umbile la mwanamke kwa kuwa linachoresha makalio, hips na mapaja, halina utofauti na kuvaa skin tight inayochoresha makalio, mapaja na hips.

Ndio maana zamani ukivaa hivi kanisani unatimuliwa ama kuvishwa kanga.
 
Unanielimisha kama nani? Fungua huduma yako ukaelimishe huko..
Sisi makanisani kwetu watu wanavaa na huwezi kuwafanya lolote.
 
Mavazi na kusali ni vitu vinanyoendana kbsa
Huwez kusali wakat uwo jiran yako paja liko njee
Huwez sali kwa aman km mtu anaingia kanisan na kiatu cha mchuchumio na mini sket flan iv
 
Unanielimisha kama nani? Fungua huduma yako ukaelimishe huko..
Sisi makanisani kwetu watu wanavaa na huwezi kuwafanya lolote.
Ni kwanini hapo zamani watu waliovaa hivyo walitimuliwa makanisani warudi wavae mavazi ya kiheshima ama kuvishwa kanga ?
 
Itabidi uwatafute watu wa zamani uwaulize.
Sisi ndo tupo na tunavaa bila bughudha yoyote.
 
Huko ni kukosa mafunzo sahihi ya sheria ya mavazi ndio maana wanalazimika kuweka matangazo juu ya mavazi, sisi wakristo inajulikana wazi kwamba kinachoangaliwa ni roho sio mavazi, kuna haja ipi ya kuweka haya mabandgo ? uliona wapi misikitini wanaweka matangazo ya aina hiyo ?

Nijuavyo kinachoangaliwa ni roho na sio mavazi, haya makatazo yalishapitwa na muda ni mambo ya agano la kale lililokataza kula wanyama kama mbwa na nguruwe, kunywa pombe, kuvaa mavazi yanyositiri, kukataza kuchonga nywele na ndevu, n.k.

Soma hili Neno upate ufahamu zaidi: Mwanzo 3:7, 21
 
Mambo ya agano la kale yalishapitwa na muda, Hata zile sheria za kukataza wanyama wa kula zilishapitwa na wakati, sikuhizi ruksa kula mbwa, nguruwe, punda, pweza, n.k.
 
Nina wasiwasi kama umesoma yaliyomo kwenye Mwanzo 3:7, 21, kwani hayaendani na unachosisitiza. Kama haukubaliani na taratibu hizo, nenda sehemu wanapozikubali usali huko, vinginevyo ni kuwafanyia fujo wahusika.

View: https://youtu.be/vGYdJ-uVvGI?si=v4lnW_x_IBfd_zcN
 
Huku ni kukosa mafunzo sahihi ya sheria ya mavazi kwa viongozi wetu wa makanisa ndio maana wanalazimika kuweka matangazo juu ya mavazi, sisi wakristo inajulikana wazi kwamba kinachoangaliwa ni roho sio mavazi, kuna haja ipi ya kuweka haya mabandiko ? uliona wapi misikitini wanaweka matangazo ya aina hiyo ?

Nijuavyo kinachoangaliwa ni roho na sio mavazi, haya makatazo yalishapitwa na muda ni mambo ya agano la kale lililokataza kula wanyama kama mbwa na nguruwe, kunywa pombe, kuvaa mavazi yanyositiri, kukataza kuchonga nywele na ndevu, n.k.

Mipasuo hupunguza umaskini kwa anayetazama kwenye Ibada!vaa kiungwana.
 
Kinachoangaliwa ni roho na sio mavazi, inakuwaje tena wanaweka sheria za mavazi ya kuvaa ?
KANISANI sio Disco Mzee sio unaenda na nguo zako za Club chupi nje nje au wengine hawavai chupi kabisa alafu wanavaa nguo nyepesi mchana nguo ya kuvaa usiku Sasa mtu km huyo bila kumzuia ataingia nayo kanisani na kuharibu ibada
 
hii ni nini ??

Photo by MOCU KCMC MWENGE MWEKA IAA TUMA on August 12, 2023. May be an image of 1 person and d...jpg
 
Roho inakaa katika mwili mkuu...

"Roho i radhi lakini mwili u dhaifu"...Alilia mwana wa Mariamu pale Golgotha. Hata Mtume Paulo alifafanua vizuri sana kuhusu mtanziko uliopo kati ya roho na mwili...ndiyo maana silaha mojawapo kuu iliyopo katika kuyashinda majaribu ni kutojiweka katika mazingira ambayo mwili utajaribiwa...

Sasa mwanaume rijali aone mwanamke pisi kali amejiachia mipaja nje nje, kigauni kimebana mpaka michoro ya chupi ilivyokaa inaonekana. Ndiyo anaweza kuwa imara kiroho lakini mwili unaweza pia kumpinga. Ndiyo maana ni vyema kuzuia vishawishi hivi hasa mahali patakatifu kama kanisani.

Kule kwingine mpaka wakaamua kutenganisha kabisa wanawake na wanaume wasali sehemu tofauti na wasionane. Unafikiri hawana akili? Imagine mtu unajaribu kufokasi na swala halafu mbele yako mwanamke aliyefungasha kabong'oa eti anaswali. Utafokasi na swala kweli?

By the way. Mfalme Daudi (mteule wa Mungu) angeweza kuepukana na dhambi ya kumla Bethsheba kama asingekuwa anazurura zurura katika ghorofa lake wakati alipaswa kuwa vitani na wanajeshi wake. Mwili ulimwangusha pamoja na kwamba kiroho alikuwa vizuri sana!

Hata mwamba Samsoni angejiendea zake nyumbani tu baada ya kugundua kuwa ulaghai wa Delilah hatimaye ungeweza kumwingiza matatizoni!

Mwili...ni dhaifu! 📌📌📌
 
kuna hii fasheni imejizolea umaarufu makanisani kuvaa magauni / sketi zinachoresha makalio, mapaja na hips, haya ni mavazi ya heshima ?

View attachment 2832956
Ndugu mleta mada!

Sasa Kanisa likiweka tangazo kusisitiza watu wavae nguo za heshima linakosea wapi?unalalamika nini unakubali nini,wewe mwenyewe umeshaona siyo nguo ya heshima lakini unasema uangaliwe moyo moyo gani unauzungumzia wewe ikiwa unajua kabisa kuna mavazi yasiyokuwa na heshima?
 
Mwanamke mmoja aliyevaa mavazi ya kikahaba anaweza tamanisha wanaume 300 kwa siku wakazini nae kiroho.
Kuzini kunaanzia mawazoni kukutana kimwili ni hitimisho tu
 
Huku ni kukosa mafunzo sahihi ya sheria ya mavazi kwa viongozi wetu wa makanisa ndio maana wanalazimika kuweka matangazo juu ya mavazi, sisi wakristo inajulikana wazi kwamba kinachoangaliwa ni roho sio mavazi, kuna haja ipi ya kuweka haya mabandiko ? uliona wapi misikitini wanaweka matangazo ya aina hiyo ?

Nijuavyo kinachoangaliwa ni roho na sio mavazi, haya makatazo yalishapitwa na muda ni mambo ya agano la kale lililokataza kula wanyama kama mbwa na nguruwe, kunywa pombe, kuvaa mavazi yanyositiri, kukataza kuchonga nywele na ndevu, n.k.

Unaujua Ukristo na sheria zake ya dunia ni ya dunia na ya Muñgu ni ya Mungu michanganyo haitakiwi
 
Back
Top Bottom