Kwanini baadhi ya makanisa yanaweka mabango kuwaasa waumini wavae kwa heshima wakati kinachoangaliwa ni roho na sio mavazi?

Kwanini baadhi ya makanisa yanaweka mabango kuwaasa waumini wavae kwa heshima wakati kinachoangaliwa ni roho na sio mavazi?

Hiyo nguo haina tatizo. Hata akiingia kanisa lolote hakuna atakae mshangaa wala kumrudisha.
Makanisani wapo wanaume wanaojitambua sio wale wengine kule hata akiona kidole anadinda, maana muda wote wanawaza ngono.
Mavazi ya kuuchora mwili hayafai uchochea tamaa
 
Hata unapoingia club kupota starehe za mule ndani kwanini waanze kukagua mlangoni kama una silaha au kitu cha kudhuru na wakati kule unaenda kumwagilia moyo.

Kila kitu kina nafasi yake usitafute excuse kwa sababu fulanifulani.
 
Kwani Yesu Kristo na Bikira Maria na wengine wakati wa Yesu waliofuata mafundisho yake walikuwa wanavaaje?
Walivaa mavazi ya kuusitiri mwili mfano kanzu hijabu kama wanavyovaa masister
 
Mavazi ya kuuchora mwili hayafai uchochea tamaa
Inawezekana hivyo kwa upande wako. Ndo maana kuna sehemu mbali mbali za kuabudu unajichagulia unayoona inafaa unaishi nayo. Wengine unawaacha na mambo yao waendelee kusisimuana kama inawapendeza.
 
kuna hii fasheni imejizolea umaarufu makanisani kuvaa magauni / sketi zinachoresha makalio, mapaja na hips, haya ni mavazi ya heshima ?


View attachment 2832956
kama umeona umbo lake katika gauni hili,hata angevaa mkeka bado ungeona tu.

mtu ana jicho la ndani na la nje,la ndani huanza kuona kitu kisha la nje huthibitisha tu,ndio sababu unaweza geuka tu nyuma ukashangaa kapita mwanamke mzuri sana,unajiuliza nilijuaje kama ndio anapita nigeuke!

tunapambania kulificha jicho la nje,wakati la ndani linamuona mwanamke akiwa uchi kabisa na linamjua vyema hata avae mabati.



Sent from my Redmi Note 8 using JamiiForums mobile app
 
Waumini wengi katika ukristu waliishi, wanaishi, na wataendelea kuishi katika upotevu na ujinga usio na kikomo.Qur'an imeelezea na kutoa hukmu juu ya mavazi kwa wanawake, hio haifichiki, ukiona mwanamke ameenda kinyume na maamrisho, huo ni ujinga wake tu.Bali hata katika Biblia kuna andiko linalo toa msingi mzima wa aina ya mavazi anayotakiwa kuvaa mwanamke (mavazi ya kujistiri) na sio agano la kale lililosema,hapana, ni agano jipya na 1:Timotheo 2:9-12ndo anazungumza hivyo. Sasa kimini ni stara,sketi ndefu lakini inabana makalio mpaka michirizi ya chupi inaonekana ni stara?, au kuvaa gauni refu lakini shepu la mwili kuanzia kifuani mpaka kwenye hips lingonekana ni stara hiyo?. Na jee! nini maana ya stara katika istilahi?ukishajua nini maana ya stara basi utafahamu kwamba 90% ya wakristu wanawake hawanastara au hawajui nini maana ya STARA. Na je? unataka kuniambia viongozi katika ukristu hawajawahi kusoma au hawajui maandiko haya katika Biblia ili wa wafundishe waumini wao? nini kinafichwa hapo? na kwa nini wakitoa mabango kuhimiza mavazi ya stara hawatoi hizo reference katika Biblia?. Andiko moja katika Biblia linasema Watu wangu wataangamia kwa kukosa maarifa.
 
Mavazi ueleza kuhusu tabia ya mtu,kipimo Cha roho mwili.
Alivyo nje mtu ndivyo alivyo ndani
 
Sasa pameshaitwa mahali patakatifu unataka watu wavae nusu utupu?ndio maana ibada hulazimishwi we ukiona huwez kuvaa kiheshima unajifukiza tu kwako
 
Back
Top Bottom