Waumini wengi katika ukristu waliishi, wanaishi, na wataendelea kuishi katika upotevu na ujinga usio na kikomo.Qur'an imeelezea na kutoa hukmu juu ya mavazi kwa wanawake, hio haifichiki, ukiona mwanamke ameenda kinyume na maamrisho, huo ni ujinga wake tu.Bali hata katika Biblia kuna andiko linalo toa msingi mzima wa aina ya mavazi anayotakiwa kuvaa mwanamke (mavazi ya kujistiri) na sio agano la kale lililosema,hapana, ni agano jipya na 1:Timotheo 2:9-12ndo anazungumza hivyo. Sasa kimini ni stara,sketi ndefu lakini inabana makalio mpaka michirizi ya chupi inaonekana ni stara?, au kuvaa gauni refu lakini shepu la mwili kuanzia kifuani mpaka kwenye hips lingonekana ni stara hiyo?. Na jee! nini maana ya stara katika istilahi?ukishajua nini maana ya stara basi utafahamu kwamba 90% ya wakristu wanawake hawanastara au hawajui nini maana ya STARA. Na je? unataka kuniambia viongozi katika ukristu hawajawahi kusoma au hawajui maandiko haya katika Biblia ili wa wafundishe waumini wao? nini kinafichwa hapo? na kwa nini wakitoa mabango kuhimiza mavazi ya stara hawatoi hizo reference katika Biblia?. Andiko moja katika Biblia linasema Watu wangu wataangamia kwa kukosa maarifa.