jf user
JF-Expert Member
- Aug 22, 2018
- 777
- 623
Biblia ni kitabu kinachojumuisha vitabu mbalimbali vilivyoandikwa na watu mbalimbali katika nyakati tofauti na sehemu tofauti.
Biblia ni mkusanyiko wa hivi vitabu ambavyo viliandikwa na waandishi mbalimbali kisha vikapangwa katika mtiririko unaofaa kuanzia miaka ya mwanzo kabisa hadi ya mwisho (Mwanzo hadi ufunuo).
Kitabu cha kwanza kwenye biblia ni Mwanzo ambacho kinaelezea uumbaji wa hii dunia, binadamu wa kwanza na habari za awali kabisa za dunia na ulimwengu. Kitabu cha mwisho ni Ufunuo Kilichoandikwa na Yohane Mbatizaji.
Hivi vitabu viliandikwa katika lugha ya kiebrania eneo la mashariki ya kati na sehemu za kaskazini mwa Africa (Misri, Ethiopia, Libya n.k) kwa sababu ndipo MUNGU alipopachagua ili neno na habari zake zisambae sehemu nyingine za ulimwengu.
Biblia imeanza kutumika rasmi baada ya kuondoka kwa Yesu Kristo ila maandiko yalikua yamehifadhiwa hata kabla ya Kristo kuja duniani.
Shida yangu ni hii
1/Kwanini vitabu kadhaa vitolewe kwenye biblia kwa misingi ya mawazo ya watu? Kama maandiko yanaonya kuongeza au kupunguza neno la MUNGU kwanini binadamu wanatoa hivyo vitabu?
2/Kitabu cha Enoch kimeondolewa, vitabu vya deuteron kanoni vinatumiwa na Roman Catholic ila Protestant na makanisa mengine hayavitumii! Injili ya Thomas, Bikira Maria, Injili ya Yuda, Injili ya Barnabas, Injili ya Eva na vitabu vingine vingi?
Ni kwanini hivi vitabu vitolewe wahusika hawakuona wanakwenda kinyume na maandiko ya MUNGU?