Ili kupata jibu la swali lako, lazima ujiulize je ni kipi kilianza kati imani au vitabu, yaani ilianza imani na baadaye watu wakaandika hayo mafundisho na kuwa vitabu au vitabu ndio vilianzisha imani?
Waprotestant wana imani yao inaitwa imani ya mitume, na ili kuwa protestant lazima ukili hiyo iman yao ya mitume. Sasa mafundisho yoyote yanayoenda kinyume na imani hai, hayo mafundisho ni ubatili.
Sasa kama vitabu ndio vilianzisha imani je ni vitabu vipi hivyo ambavyo vilianzisha hiyo imani na vimeolozeswa wapi ili sasa kujua kama kuna vitabu fulani vimeondolewa na kupelekea kukosa mafundisho fulani, maana kama kuna vitabu vimekosekana lazima kutakiwa na mapungufu katika imani hiyo iliyo ainishwa katika vitabu hivyo. Mfano kanisa la RC wao wanamisa ya kuombea wafu na ili kusupport hili jambo wanavitabu vyao wanavyotumia kama mwongozo, kwa hiyo mtu akihoji mnapata wapi hayo mafundisho basi anaonyeshwa hayo mafundisho kwenye vitabu vyao. Protestant hawana mafundisho ya kuombea wafu sababu wao hawana vitabu vyenye mafundisho hayo.
Kama imani ndio ilianza na baadaye yale mafundisho yakawekwa katika vitabu, maanayake ni kwamba imani na mafundisho yaliyo katika kitabu lazima yaendane kinyume na hapo yote yanakuwa ni ubatili.
Sasa kwa issue nibble, kilichoanza ni imani ndio ikapelekea vitabu vyenye mafundisho yake, utasema umejiaje, ni kwamba kabla musa kuwapo hakukuwa na torati na kabla ya Yesu kuwapo hapakuwa na injiri, kwa hiyo imani ndio ilizaa vitabu vyenye mafundisho yake
Sasa kuna hoja kwamba mbona bibilia hiyo hiyo imetaja baadhi ya vitabu lakini hivyo vitabu havipo hivyo kwa msingi huo kuna vitu baadhi ya wakristo wanaficha. mfano ndugu zetu Islam wao wanasema injiri ya Barbara, Henoc, pia Qur'an maana Islam kwa mujibu wa mafundisho yao ni kuwa mtume wao ni ndio nabii wa mwisho.
Kama nilivyosema kuwa bible ni mafundosho yalitokana na imani na kupolekea kuandikwa kwa hiko kitabu na sio bible ndio ilizaa imani ya ukristo, hivyo basi vitabu vyote vinavyopingana na imani ya ukristo ni ubatili na havifai kwa mafundisho ya ukristo, hata kama hicho kitabu kina jina linalo fanana na jina la kitabu kikichotajwa katika bible na kutokuwa compiled katika bible ya sasa.
Sasa kwanini kuna baadhi ya vitabu vimetajwa katika bible lakini havijawa compiled katika bible ya sasa.kitendo cha bible kutaja baadhi ya vitabu, kwanza ni uthibitisho kwamba enzi hizo kulikuwa na waandishi wengi walikuwa wanaandika maandiko ya mafundisho mbalimbali including vitabu vya bible.
Na ukisoma hiyo bible inasema kuna waandishi walikuwa wanafanya upotoshaji katika maandiko yao, hivyo swala la kupotosha kupitia maandiko halijaanza leo wala jana. Na huu upotoshaji ndio sababu mojawapo ya baadhi ya vitabu kuwachwa maana vinapingana na msingi wa imani ya ukristo, mfano Qur'an inasema Yesu hakusulubiwa wala hakufa, wakati msingi wa imani ya ukristo unajengwa katika kusulubiwa na kufariki msalabani kwa Yesu wa Nazareth kwa hiyo ilo fundisho la quaran ni ubatili kwa mkristo, lakini ujiulize tuseme kweli kuna vitabu vipo vina mafundisho kama imani ya Kristo inavyosema je ni rahisi kuvi compile na kuwa kitabu kimoja hataka vipo labda elfu moja, hapana na ndio maana vipo hivyo lakini vineeleza kwa upana wake imani ya ukristo.
Nimalizie kwa kusema tu imani ya kikristo ipo wazi haina cha kuficha nai kwamba vitabu vingine vinakosa sifa au vigezo ya kutumia kama mafundisho kuhusu ukristo.