Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 48,475
- 70,102
Waumini wengi wa zinazoitwa dini mbili kubwa za Tanzania kuna mambo kadhaa inabidi mbadilike kuendana na mabadiliko ya wakati.
1. Kusalimia kila mtu "salameleko"
Sijawahi kuelewa sababu za baadhi ya watu kumsalimia kila mtu anayeongea naye kwa hii salamu ya kidini ya salamaleko ukizingatia sio watu wote unaokutana nao ni wa hiyo dini yako.
2. Kujenga hoja kwa kurejea vitabu vya dini.
Unaweza kuwa unajadiliana na mtu au watu masuala mbalimbali ya maisha ambayo ni ya ki-secular kabisa mara unasikia anasema "hata vitabu vya vitakatifu dini vinatuambia blah blah...." Sikubaliani kabisa kujenga hoja za msingi kwa kurejea vitabu vya kidini tena kimoja au viwili tu hasa inapokuwa ni suala au jambo linalohusu mkusanyiko wa watu wenye dini au imani tofauti.
3. Tabia ya kufanya mahubiri kwenye vyombo vya usafiri vya umma
Hii tabia ndugu zetu Wakristo inabidi ifike mwisho sasa au mamlaka zifanye udhibiti wake. Sio sahihi hata kidogo kugeuza vyombo vya usafiri uwanja wa mahubiri, mtu anaposafiri safari ndefu kwanza mtu anachoka hivyo anahitaji utulivu. Pia kwenye hicho chombo kuna watu wa imani tofauti hivyo inakuwa usumbufu mkubwa kwao pia