Kwanini baadhi ya watu wenye dini zao hufikiri kila mtu anapaswa kuendana nao?

Kwanini baadhi ya watu wenye dini zao hufikiri kila mtu anapaswa kuendana nao?

Dini HUSAIDIA katika kuweka maadili sawa kama vile tu katiba/sheria ya nchi ilivyo, tofauti ni kwamba dini hutumia guilt (hatia) kuweka watu katika maadili wakati sheria ya nchi hushurutisha.
Mafisadi, wezi, watukanaji, wabakaji, walawiti na wengine wengi waovu wengi wao zaidi ya 99% huwa ni watu wenye dini.
 
Katika hoja zako 3 iko hivi,

1. Asalaam Aleykum siyo salam ya kidini ni salam ya watu wa middle East, Yesu pia alikuwa akisalimia hivi pia ambapo tafsiri yake kwa kiswahili ni Amani iwe juu yako, na wewe unaitikia na kwako pia, je kuna shida hapo? Shida ni lugha tu huelewi, ni kama Wakristo wanashindana salamu ya bwana asifiwe na tumsifu Yesu kristu ipi sahihi? Huwezi kuona hawa wote ni vichaa? Kuna tofauti gani hapo katika hizo mbili?

2. Hizo refference siyo lazima uzikubali unaweza kuzikataa au kuzikubali kwa sababu vyote ni vitabu vimeandikwa na binadamu havijaandikwa na Mungu.

3. Nakubaliana na wewe mia kwa mia kwenye hoja namba 3.
Sasa kwanini unisalimie salam ya watu wa kati huko inanisaidia nini si bora unisalimie kwa kisukuma asee MKOME
 
Ingetokea nikawa Rais hata kwa mwez tu...ningeweka kodi kubwa sana kwa hawa watu..yaani sio msikitini wala makanisani...wangeyafunga wenyewe bila kupenda..kwa nn hawalipi kodi??
 
Unafikiri hayo maneno uliyoandika hamna kiarabu ??
Kiswahili kimekopa maneno kutoka lugha mbalimbali ikiwemo kiarabu. Kama kiarabu kipo hapo ni sawa maana ndipo tulipokopa maneno mengi
 
Katika hoja zako 3 iko hivi,

1. Asalaam Aleykum siyo salam ya kidini ni salam ya watu wa middle East, Yesu pia alikuwa akisalimia hivi pia ambapo tafsiri yake kwa kiswahili ni Amani iwe juu yako, na wewe unaitikia na kwako pia, je kuna shida hapo? Shida ni lugha tu huelewi, ni kama Wakristo wanashindana salamu ya bwana asifiwe na tumsifu Yesu kristu ipi sahihi? Huwezi kuona hawa wote ni vichaa? Kuna tofauti gani hapo katika hizo mbili?

2. Hizo refference siyo lazima uzikubali unaweza kuzikataa au kuzikubali kwa sababu vyote ni vitabu vimeandikwa na binadamu havijaandikwa na Mungu.

3. Nakubaliana na wewe mia kwa mia kwenye hoja namba 3.
Shalom.......
 
Mimi mtu akinisalimia hivyo nasemaga mimi sijui kiarabu na yeye nikimsalimia kihindi atanijibu?😃😃
Kama wewe ni mhindi ukisalimia kihindi haina noma sana, tatizo litaanza wewe ni Mwafrika tena labda mweusi tii kama chungu halafu unasalimia Waafrika wenzako wabantu kihindi.
 
Inabidi uende mbali zaidi ili ujue siasa inahusiana vipi na dini na kwa namna gani zimeathili tamaduni za watu.
 
Ila mtu akinukuu akina Aristotle,Mwalimu Nyerere unapenda ? Hekima ipo kwenye vitabu vitakatifu.acha upoyoyo.pia Salamu kama haikuhusu/huijui itika unavyojua. Kwenye vituo vya mabasi kukiwa na miziki ya Koffi,Matangazo ya Dawa, Biashara hakuna shida! Ila akihubiriwa Muumba wa vyote,ni shida! Umekamatwa na ibilisi wewe,yakupasa toba.mfano injili ni habari njema,unakasilikia vipi habari njema?
Maandiko ya Aristotle na Nyerere ni maandiko ya ki-secular yanayoweza kutumika na watu wa dini zote na wasio na dini pia.
 
Ila mtu akinukuu akina Aristotle,Mwalimu Nyerere unapenda ? Hekima ipo kwenye vitabu vitakatifu.acha upoyoyo.pia Salamu kama haikuhusu/huijui itika unavyojua. Kwenye vituo vya mabasi kukiwa na miziki ya Koffi,Matangazo ya Dawa, Biashara hakuna shida! Ila akihubiriwa Muumba wa vyote,ni shida! Umekamatwa na ibilisi wewe,yakupasa toba.mfano injili ni habari njema,unakasilikia vipi habari njema?
Ni habari njema kwako sio kwa kila mtu.
 
Back
Top Bottom