Kwanini bado usipuuze Maombi?

Kwanini bado usipuuze Maombi?

Wakikubaliana wote inakuja.

ikiwa watu wangu, walioitwa kwa jina langu, watajinyenyekesha, na kuomba, na kunitafuta uso, na kuziacha njia zao mbaya; basi, nitasikia toka mbinguni, na kuwasamehe dhambi yao, na kuiponya nchi yao.

2Nyakati 7:14
Watu wote wanaweza kukubaliana kwa jambo moja?
Unaweza kuomba watu wote wakubaliane?
 
Wao sio chama cha maombi, ni chama cha siasa. Waje na kitu bora ambacho kama mbadala wa hiki tunachokiona.

Pia sio lazima mbadala wa CCM iwe chadema. Inaweza pia kuwa CCM iliyobadilika au Mungu akafumua wote wawili akaleta kitu kipya.
Unaweza kuomba CCM ikabadilika?
 
Watu wote wanaweza kukubaliana kwa jambo moja?
Unaweza kuomba watu wote wakubaliane?
Ninawi walikubaliana wote, kuanzia mfalme. Inawezekana kama litakuwepo jambo linalowafanya wakubaliane.
 
Wakikubaliana wote inakuja.

ikiwa watu wangu, walioitwa kwa jina langu, watajinyenyekesha, na kuomba, na kunitafuta uso, na kuziacha njia zao mbaya; basi, nitasikia toka mbinguni, na kuwasamehe dhambi yao, na kuiponya nchi yao.

2Nyakati 7:14
Hujui hata unasimamia kitu gani, kwani hapa Tanzania unaposema kuna amani tumekubaliana wote?
 
Tanzania tunaweza kuomba umaskini ukaisha?
Yes.
KWa maombi Mungu hutoa maelekezo juu ya kutatua changamoto yoyote ile.
Mungu akitoa maelekezo, kinafuata hatua ya namna ya kutekeleza maelekezo hayo kwa uaminifu.
 
Hujui hata unasimamia kitu gani, kwani hapa Tanzania unaposema kuna amani tumekubaliana wote?
Hiyo niliyokupa ni kanuni. Ukitaka amani mahala ambapo haipo sio tu nch8 hata familia maombi ya pamoja wote mkikubaliana inakuja.

Zipo exceptions. Ndio maana Mungu anaachilia amani hata kwa nchi ambazo hazimtambui kwa makusudi yake yeye kama Mungu. Ila hili halibatilishi kanuni hapo juu.
 
😂😂😂atakwambia NDIO
Hakuna linaloshindikana kwa Mungu. Halipo.
Jeremiah 32:26,27
"Tazama mimi ni Bwana, Mungu wa wote wenye mwili, Je kuna jambo lolote nisiloliweza?"

Hao chadema kama watautafuta utakatifu, wakaamua kumtegemea Mungu kwa moyo wote pasipo kujichanganya, wakamlilia Mungu juu ya uasi na madhira ya ccm juu ya watanzania, Mungu atasikia toka Mbinguni na ataiondoa Ccm madarakani.

"ikiwa watu wangu, walioitwa kwa jina langu, wakinyenyekesha na kuomba na kuutafuta uso wangu na kuziacha njia zao mbaya, mimi Mungu, nitasikia toka Mbinguni na kuwatoa katika tabubyao"
 
Kuna wanaobeza thread hii ya maombi msichanganye mambo ya ulimwengu wa roho na ulimwengu wa mwili chanzo cha mambo mengi ni ulimwengu wa roho tatzo wengi hamna elimu na haya mambo
Wasikuumize kichwa
2wakorintho 4:4
mngu wa dunia hii (ibilisi) amewapofusha fikra zao isiwazukie nuru.

They have a pre determined mind of unbelief.
 
Maombi huenda na vitendo. Bila kuwa na ari ya kutaka kukamilisha jambo huwezi toboa.

Yani ni sawa na uwe na software bila kuwa na hardwares. Huwezi kufanikisha chochote.

Maombi + vitendo = Matokeo
Uko sahihi.
Iman pasipo matendo imekufa.
Neno la Mungu liko wazi kuhusu hili suala
 
Hiyo niliyokupa ni kanuni. Ukitaka amani mahala ambapo haipo sio tu nch8 hata familia maombi ya pamoja wote mkikubaliana inakuja.

Zipo exceptions. Ndio maana Mungu anaachilia amani hata kwa nchi ambazo hazimtambui kwa makusudi yake yeye kama Mungu. Ila hili halibatilishi kanuni hapo juu.
Sio anaachilia kwa nchi ambazo HAZIMTAMBUI, ukweli ni kwamba maombi hayaleti amani, wewe unasoma maandiko ya kale huko, lakini uhalisia wa sasa unakataa, HAKUNA nchi duniani kwasasa watu wanakubaliana wote HAKUNA
 
Neno la MWENYEZI MUNGU ni upanga waefeseo6:17

Shida ya vijana wa leo wametanguliza mzaha sana na kufuata mkumbo

Alafu wanataka waombe kwa siku moja na kufanikiwa
Sure. They dont mean on what they pray for.. and also dont pray while believing.
Kwa maana aombaye hupokea na atafutaye huona.

Mbaya zaid ni kwamba watu wengi sasa hivi suala la utakatifu na kuishi maisha ya kumpendeza Mungu imekua sio kipaumbele kwao.

Mungu anasema wazi. "Tazama, mkono wangu si mfupi hata ushindwe kuokoa wala sikio langu si zito hata nishindwe kusikia. Bali maovu yenu yamewafarikisha ninyi na Mungu hata ameficha uso wake msiouone wala sikio lake asisikie.
 
Hakuna linaloshindikana kwa Mungu. Halipo.
Jeremiah 32:26,27
"Tazama mimi ni Bwana, Mungu wa wote wenye mwili, Je kuna jambo lolote nisiloliweza?"

Hao chadema kama watautafuta utakatifu, wakaamua kumtegemea Mungu kwa moyo wote pasipo kujichanganya, wakamlilia Mungu juu ya uasi na madhira ya ccm juu ya watanzania, Mungu atasikia toka Mbinguni na ataiondoa Ccm madarakani.

"ikiwa watu wangu, walioitwa kwa jina langu, wakinyenyekesha na kuomba na kuutafuta uso wangu na kuziacha njia zao mbaya, mimi Mungu, nitasikia toka Mbinguni na kuwatoa katika tabubyao"
Unaleta maandiko ambayo hukuwepo, rudi sasa kwenye dunia ya sasa watu wana amani hata huyo Mungu mwenyewe hawamjui,nchi zina maendeleo hata huyo Mungu wako hawamjui
 
Back
Top Bottom