Kwanini bado usipuuze Maombi?

Kwanini bado usipuuze Maombi?

Amani hailetwi na maombi wewe, kwani huko Lebanon , Ukraine, Urusi, Syria hakuna wanaofanya maombi?
Mungu anaweza kuleta amani. Yeye ni mfalme wa amani.
Lakini kaa ukijua kuwa, Mungu ni Mungu mwenye Hasira, na ghadhabu yake inapomwagwa juu ya nchi dunia lazima itikisike, Kabla ya kuleta maangamivu yoyote, Jua kabisa, Maonyo hutangulia.

Ezekiel 22:30
Nami nikatafuta mtu miongoni mwao, atakayelitengeneza boma, na kusimama mbele zangu mahali palipobomoka, kwa ajili ya nchi, nisije nikaiharibu, lakini sikuona mtu.
 
Unaleta maandiko ambayo hukuwepo, rudi sasa kwenye dunia ya sasa watu wana amani hata huyo Mungu mwenyewe hawamjui,nchi zina maendeleo hata huyo Mungu wako hawamjui
Hao akina Aristotle na Caesar waliobuni democracy pamoja na hao akina eistein wamekuachia maandiko kibao ambayo unajihangaisha nayo mpaka leo kutafuta maarifa wewe ULIKUWEPO WALIPOKUWEPO????
 
Mungu anaweza kuleta amani. Yeye ni mfalme wa amani.
Lakini kaa ukijua kuwa, Mungu ni Mungu mwenye Hasira, na ghadhabu yake inapomwagwa juu ya nchi dunia lazima itikisike, Kabla ya kuleta maangamivu yoyote, Jua kabisa, Maonyo hutangulia.

Ezekiel 22:30
Nami nikatafuta mtu miongoni mwao, atakayelitengeneza boma, na kusimama mbele zangu mahali palipobomoka, kwa ajili ya nchi, nisije nikaiharibu, lakini sikuona mtu.
Hakuna kitu hapo huko Lebanon kuna wakristo kama wewe wanaomba amani hakuna kitu wanapata, Mungu sio wa hivyo wewe
 
Hao akina Aristotle na Caesar waliobuni democracy pamoja na hao akina eistein wamekuachia maandiko kibao ambayo unajihangaisha nayo mpaka leo kutafuta maarifa wewe ULIKUWEPO WALIPOKUWEPO????
Democracy tunaiona inafanya kazi watu wanaishi nayo, mpaka viongozi wa dini wanatuambia tukapige kura, sio maombi ambayo hakuna uhalisia
 
Bado maombi yana nguvu. Puuza wanaopuuza maombi.

Maombi Yanaweza kugeuza maamuzi ya Serikali na viongozi wakubwa wa nchi. Mfalme wa Iran Koreshi, Altashasta na Dario walijikuta wanaendeshwa na maombi ya wakina Danieli, Nehemia, Ezra licha ya ukatili wao.

Maombi yalimtoa Petro Gerezani.

Maombi yalizuia mvua miaka 3, na kuileta kwa neno la Eliya.

Maombi yalimfanya mtu mmoja Ibrahim aishi kama jeshi, na hakuna aliyemuweza.

Maombi yalimfanya Yakobo apite katikati ya maadui zake bila kuguswa.

Maombi yanaangusha ngome

Maombi yana nguvu ya kupasua bahari.

Maombi maombi maombi

Usipuuze maombi.

Ni hayo tu

Mtumishi Matunduizi
Sisi walutheri tunasema Ora et Labora maana yake kazi na sala.
Yaani unapoomba, ukimaliza amka nenda kakipambanie ulichokuwa unakiomba.
 
Hakuna kitu hapo huko Lebanon kuna wakristo kama wewe wanaomba amani hakuna kitu wanapata, Mungu sio wa hivyo wewe
Lebanoni umeenda mbali sana ndugu, anzia jirani tu hapo Congo na hata hapo kusin tu mtwara kwa chini, wapo wakristo.

Kuna jambo unapaswa Kujua, the only standard of God. HOLLINESS.
MUNGU always husikia maombi ya watakatifu. Read betwewn the lines
 
Kwahiyo huko kwenye machafuko HAKUNA WATAKATIFU wa kuomba amani?😂😂😂
 
Kwahiyo huko kwenye machafuko HAKUNA WATAKATIFU?😂😂😂
HAkuna siasa wala kuuma maneno inapokuja kwel ya Mungu kaka.
Watakatifu wapo, na maadamu wapo, uwe na uhakika wana mkono wa Mungu uko juu yao na hakuna baya baya litawapata
"Haijalishi mamia wataanguka mkono wa kulia na mamia mkono wa kushoto, tauni haitakukaribia wewe"

Why?kwasababu
"Bwana ndiye mchungaji wao, wajapopita kwenye bonde la uvuli wa Mauti, hawataogopa mabaya, gongo lake na fimbo yake vyawafariji"

Nikuuloze swali.
Unaweza nipa list ya watakatifu unaowajua huko waliokufa?
Ahsante.
 
Democracy tunaiona inafanya kazi watu wanaishi nayo, mpaka viongozi wa dini wanatuambia tukapige kura, sio maombi ambayo hakuna uhalisia
Basi jua na maombi yanafanya kazi, Njoo tukuonyeshe matendo makuu ya Mungu, .ujue tatizo ni kwamba faith is not a public office , things happen na waliotendewa wanamtukuza Mungu kwa shuhuda halisi kwenye maisha yao.

Mungu wa kwel yupo, na matendo yake makuu bado tunayaona. Sema ndio hivyo, unataka uone wanyama wa mikumi wakati umepitia njia ya Bagamoyo na safari yako ni arusha

Je wewe ninwa njia hii????
Come and see!.
 
HAkuna siasa wala kuuma maneno inapokuja kwel ya Mungu kaka.
Watakatifu wapo, na maadamu wapo, uwe na uhakika wana mkono wa Mungu uko juu yao na hakuna baya baya litawapata
"Haijalishi mamia wataanguka mkono wa kulia na mamia mkono wa kushoto, tauni haitakukaribia wewe"

Why?kwasababu
"Bwana ndiye mchungaji wao, wajapopita kwenye bonde la uvuli wa Mauti, hawataogopa mabaya, gongo lake na fimbo yake vyawafariji"

Nikuuloze swali.
Unaweza nipa list ya watakatifu unaowajua huko waliokufa?
Ahsante.
Unajua na sisi tunasoma hayo maandiko!!! wale wanafunzi wa Yesu walikuwa watakatifu lakini kwa taarifa yako wote waliuwawa kwa namna tofauti na utakatifu wao, mwanafunzi pekee aliekufa kifo cha kawaida ni mtume Yohana pale Uturuki, kwahiyo utakatifu wako HAUKUZUII kukutwa na mabaya , Swali langu hao watakatifu wa Lebanon maombi yao Mungu hawasikii ?
 
HAkuna siasa wala kuuma maneno inapokuja kwel ya Mungu kaka.
Watakatifu wapo, na maadamu wapo, uwe na uhakika wana mkono wa Mungu uko juu yao na hakuna baya baya litawapata
"Haijalishi mamia wataanguka mkono wa kulia na mamia mkono wa kushoto, tauni haitakukaribia wewe"

Why?kwasababu
"Bwana ndiye mchungaji wao, wajapopita kwenye bonde la uvuli wa Mauti, hawataogopa mabaya, gongo lake na fimbo yake vyawafariji"

Nikuuloze swali.
Unaweza nipa list ya watakatifu unaowajua huko waliokufa?
Ahsante.
Ezekieli 14:13
Mwanadamu, nchi itakapofanya dhambi na kuniasi, kwa kukosa, nikaunyosha mkono wangu juu yake, na kulivunja tegemeo la chakula chake, na kuipelekea njaa, na kukatilia mbali mwanadamu na mnyama;
Ezekieli 14:14
wajapokuwa watu hawa watatu, Nuhu, na Danieli, na Ayubu, kuwamo ndani yake, wangejiokoa nafsi zao wenyewe tu kwa haki yao, asema Bwana MUNGU.

Mambo ya Mungu ni kanuni.
 
Basi jua na maombi yanafanya kazi, Njoo tukuonyeshe matendo makuu ya Mungu, .ujue tatizo ni kwamba faith is not a public office , things happen na waliotendewa wanamtukuza Mungu kwa shuhuda halisi kwenye maisha yao.

Mungu wa kwel yupo, na matendo yake makuu bado tunayaona. Sema ndio hivyo, unataka uone wanyama wa mikumi wakati umepitia njia ya Bagamoyo na safari yako ni arusha

Je wewe ninwa njia hii????
Come and see!.
Hayana kazi ndio maana watu wanavamia mpaka makanisa CONGO na kwengineko hakuna wa kuwazuia, ndio maana hata zile sehemu ambazo watu wanakutana kwa ajili ya kuabudu Mungu zinalindwa na watu
 
Watu wote wanaweza kukubaliana kwa jambo moja?
Unaweza kuomba watu wote wakubaliane?
MOja ya zawad Mungu alimpa mwanadamu, ni Free will. Ndio maana anakuumba na bado anakuachia uhuru wa kumkataa.

Makubaliano yoyote baina ya watu, Mungu huyaheshimu.
Na katika kukubaliana, wala huhitaji kundi kuuuubwa la Watu ili Mungu afanye jambo.

"Walipo wawili au watatu kwaajili ya neno langu, NAMI NIPO KATIKATI YAO"
 
Hayana kazi ndio maana watu wanavamia mpaka makanisa CONGO na kwengineko hakuna wa kuwazuia, ndio maana hata zile sehemu ambazo watu wanakutana kwa ajili ya kuabudu Mungu zinalindwa na watu
Sawa..Hata wewe unaweza mbona vamia kanisa hata saa hii ukitaka.
 
MOja ya zawad Mungu alimpa mwanadamu, ni Free will. Ndio maana anakuumba na bado anakuachia uhuru wa kumkataa.

Makubaliano yoyote baina ya watu, Mungu huyaheshimu.
Na katika kukubaliana, wala huhitaji kundi kuuuubwa la Watu ili Mungu afanye jambo.

"Walipo wawili au watatu kwaajili ya neno langu, NAMI NIPO KATIKATI YAO"
1.KANISA
2.MSIKITI
3.HEKALU
Haya majengo yote watu wanakwenda kumuabudu Mungu LAKINI yote haya walinzi ni WATU
 
Back
Top Bottom