sky soldier
JF-Expert Member
- Mar 30, 2020
- 5,407
- 19,264
Nashangaa kuona bado hizi fikra za kale zinaendelea "kila mtu ajitafutie cha kwake", mtoto wa mfanyabiashara anafika miaka 23 hana utofauti na watoto wa mwalimu, yani hajui kitu kuhusu biashara kiasi kwamba hata akimaliza chuo anafikiria mshahara, hata akikosa ajira mzazi kwenye account ana milioni 500 lakini atampa kimtaji cha milioni 10 nae aende kupambana kivyake "ajitafutie kivyake", Mzazi hamuamini mtoto wake aendeleze biashara zake.
Wazazi Watanzania ambao wamefanikiwa ni waoga sana kuwatumia watoto wao kuendeleza miradi yao ya kibiashara iliyofanya wafanikiwe tofauti na wenzetu wenye asili ya Asia (Waarabu na Wahindi)
Nikupe mfano utakuta baba alikuwa na maduka ya hardware na mashamba, biashara hizi zimempa mafanikio hata watoto wake kawasomesha kupitia maokoto ya huku.
Cha ajabu
-watoto mpaka wanakuwa wakubwa hawashirikishwi kwenye biashara walau wajifunze hata machimbo ya kujumulia mzigo,
-haukuti anawasomesha waje waendeleze biashara hiyo ya familia waje na idea mpya,
matokeo yake baba umri ukienda (uzee) au kifo na biashara zinakufa maana watoto hawajui chochote kuhusu hizo biashara, wajanja wanafagia.
Watanzania tunakosa kujiamini sana kuendeleza biashara za kifamilia. Tunapenda sana kuajiriwa. Wenzetu wanatengeneza brands