tutafikatu
JF-Expert Member
- Dec 17, 2011
- 3,327
- 4,624
Wapiga kura wengi au sioMtaji wa wanasiasa huo
Wapiga Kura Wa Mzilankende Sasa Ni Wa Chifu Hangaya... hao ni wapiga kura chief; hata faini zao ni 10K kama sijakosea.
Kwa maoni yangu ili kukomesha vitendo vya uvunjaji wa sheria za barabarani kwa vyombo vyote vya moto, ikiwemo hizo Bajaj, bodaboda, daladala etc ingetakiwa uindwe mamlaka mpya kabisa ya ''USALAMA BARABARANI'' na polisi/trafiki watolewe kabisa kwenye jukumu hilo. Polisi/Trafiki warudi kuendelea na kazi yao kuu ya USALAMA WA RAIA NA MALI ZAO. Hii Mamlaka inaweza kuwa chini ya Wizara ya Miundombinu au Wizara ya Mambo ya Ndani, na ipewe mamlaka ya kusimamia usalama barabarani, leseni, kufunga taa za barabarani, kufunga camera barabarani kurikodi matukio mbaliimbali ya madereva nk. Utaratibu wa kupiga tochi ufutwe na mfumo mpya wa CCTV camera ndiyo utumike ,ambapo gari likirekodiwa linatumwa kwa namba ya gari ili muhusika akalipe faini ndani ya muda fulani. Pale ambapo Mamlaka itahitaji msaada wa polisi kwa special operation za kijinai wanaweza kuchukua polisi anytime.Bajaj zikipita traffic light bila ruhusa haina shida, wewe mwenye gari ukiunga ukidhani mmeruhusiwa imekula kwako.
Bajaj ikijaza watu, igeuze main road, ichukue abiria nje ya kituo, na dereva aendeshe kwa kuning'inia hakuna mtu atambugudhi. Daladala ifanye kosa mojawapo hapo utaumia.
Kama tumeamua bajaj ziwe njia yetu kuu ya usafiri, kwanini zisifuate sheria za barabarani?
Tumekuwa Taifa la hovyo.