sky soldier
JF-Expert Member
- Mar 30, 2020
- 5,407
- 19,264
Kama pombe tuijuavyo, inaweza kumfanya mtu ajinyee (mnisamehe kwa luga kali ila imebidi), atapike, azimie (kuzima), kuropoka, kushindwa kujitambua kabisa, hupunguza umakini (rejea mheshimiwa Kitwanga), n.k. licha ya haya yote lakini pombe hii ni halali.
Ni utumwa wa fikra huu, tulirithishwa sheria za kilo;oni ikiwemp sheria ya kufanya bangi iwe haramu nayo tukaipokea hivyo hivyo mpaka leo.
Haya mambo ya kufata fata sheria tulizorithishwa na wakoloni yawe na limit yake, kisa wakoloni waliona bangi ni mbaya basi sheria walizoziacha nasi tunazifata hivyo hivyo .... Hata makombo na matapishi ya sheria za utesajii zilizotumika kwenye jela enzi za ukoloni kwa wafungwa watumwa hasa waliotetea uhuru na kuwachukiza wakoloni ndizo zinatumika mpaka leo, si ajabu kukuta wafungwa wakifanyishwa makazi mazito lakini mlo ni moja tu siku nzima na watu walivyo wajinga wanatoa sababu zile zile za kikoloni eti ili wafungwa wasipate nguvu.
bangi mtu ataitumia lakini bado anaweza kujitambua tofauti na pombe.
Bangi ambayo hufanya watu wawe machizi ni sababu ya ivi vitu ambavyo vitaisha ikiwa halali:
1. Baadhi ya mapusha wanaouza bangi mtaani huwa wanachanganya bangi na madawa ya kulevya yanayotindua akili si kidogo, wateja wanadhani kwamba bangi ya pusha huyo ni "mzigo wenyewe" kumbe wanachobuta ni madawa kama methamphetamine na maunga, hapa si ajabu kukuta mtu anavua hata nguo anatembea uchi mtaani. ndivyo kina Ray C walivyopatwa na masaibu yaliyowahi kuwakuta hivi, mtu unadhani unavuta bangi kumbe mhuni kakuchanganyia madude, yeye anachotaka uwe mteja wa kudumu tu awe anapiga pesa yako, hajali hata uwe kichaa.
2. Watumiaji wa bangi kutokuwa na elimu ya wazi ya matumizi sahihi, wapo watumiji wanavuta bangi mbichi miaka nenda rudi kumbe haya si matumizi sahihi, wapo watumiaji hawajui kuichambua kuyatenganisha maua ya bangi yasiwe na vijiti na mbegu, wao wanachanganya na haya si matumizi sahihi ... n.k.