Kwanini bidhaa nyingi zinazoagizwa kuja barani Afrika zinatokea China isipokuwa magari ambayo yanatokea Japan?

Labda wa sababu barabara nyingi za Afrika zinafadhiliwa na pesa za Wajapani ndio maana wanataka magari yao pekee ndio yapite katika barabara hizo.

Sina uhakika lakini nimeotea tu.

Nina hiyo pia kama kuna makubaliano fulani kati ya serekali na Japan maana gari za Japan zina ushuru mdogo ukilinganisha na gari kutoka ulaya au USA. China wanatumia stealing kushoto pengine ndiyo maana magari yaliyotumika hayaji TZ
 
Nina hiyo pia kama kuna makubaliano fulani kati ya serekali na Japan maana gari za Japan zina ushuru mdogo ukilinganisha na gari kutoka ulaya au USA.
Mkuu, sio kwamba ushuru unategemea na uchakavu pamoja na ukubwa wa engine ya gari husika?...
 
Nina hiyo pia kama kuna makubaliano fulani kati ya serekali na Japan maana gari za Japan zina ushuru mdogo ukilinganisha na gari kutoka ulaya au USA. China wanatumia stealing kushoto pengine ndiyo maana magari yaliyotumika hayaji TZ
Sidhana kama mfumo wa barabara za China ni LHS
 
Mta- MATAGS mkuu , na wengine wote wanaosema tunaweza kujitegemea kwa maneno huku kila siku wakipokea misaada tena bila kutuambia , kama ile bilioni 70 ya kupambana na korona
Huyu MATAGS ndio nani tena mzee baba?...
 
napmva kampuni moja ya magar toka china
 
Una maana China wanashindwa kutengeneza gari mpya za 4,000-USD?
Mkuu gari mpya Kwa hiyo bei, mchina akikutengenezea utawekewa injini za power tiller au zile pikipiki gari Baw. Hiyo gari ukinunua utadai urudishiwe pesa. Mchina injini anazotengeneza za Weichai bado zipo juu na zina teknolojia ya zamani.
Ndio maana kwenye Haval na Great Wall kaweka injini za Isuzu.

Cheap is Cost.
 
Hapana. mchina hatengenezi bidhaa feki kwa ajili ya china na hakuna bidhaa feki inauzwa china kwa ajili wachina bali ni kwa ajili ya aftica

Ndio maana hakuna mchina aliyepo china anaye tumia TECNO , INFINIX au ITEL
Hili nakubaliana na wewe. Ukienda soko la wageni pale Beijing, bidhaa zao zote magumashi matupu, lakini wenyewe wanatumia simu za Apple na bidhaa Original za Europe. Wakitumia za kwao kwa mfano simu ni Xiaomi(REDI MI), ambazo ni za quality.
 
Hili nakubaliana na wewe. Ukienda soko la wageni pale Beijing, bidhaa zao zote magumashi matupu, lakini wenyewe wanatumia simu za Apple na bidhaa Original za Europe.
Wanatumia bidhaa za europe wakati wao wanatuuzia sisi midosho...
 
Hili nakubaliana na wewe. Ukienda soko la wageni pale Beijing, bidhaa zao zote magumashi matupu, lakini wenyewe wanatumia simu za Apple na bidhaa Original za Europe. Wakitumia za kwao kwa mfano simu ni Xiaomi(REDI MI), ambazo ni za quality.
Mkuu, hizi simu za Xiaomi(REDI MI) zinapatikana hapa Tanzania?
 
Mkuu gari mpya Kwa hiyo bei, mchina akikutengenezea utawekewa injini za power tiller au zile pikipiki gari Baw. Hiyo gari ukinunua utadai urudishiwe pesa. Mchina injini anazotengeneza za Weichai bado zipo juu na zina teknolojia ya zamani.
Mkuu, hakika upo vizuri sana katika mambo haya...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…