Travelogue_tz
JF-Expert Member
- Sep 28, 2010
- 855
- 1,224
Brigedia John Mbungo, Mkurugenzi Takukuru
Teuzi za wanajeshi zilishamirishwa na hulka ya Mtawala aliyepita, Hayati John P. Magufuli ambaye aliamini katika matumizi ya vitisho, nguvu na mabavu katika uendeshaji wa shughuli za Serikali.
Je, bado CCM na Mh. Samia Suluhu Hassan wanaona fahari kwa Viongozi wa kiserikali kuendelea kuvaa kombati katika shughuli za kiraia?
Fahamu wajibu wa kikatiba wa Jeshi
- Kulinda Katiba na Uhuru wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
- Ulinzi wa mipaka ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
- Kufanya mafunzo na mazoezi ili kujiweka tayari kivita wakati wote.
- Kufundisha umma shughuli za ulinzi wa Taifa.
- Kushirikiana na mamlaka za kiraia katika kutoa misaada ya kibinadamu na uokoaji wakati wa maafa
- Kutoa huduma mbalimbali za kijamii.
- Kukuza elimu ya kujitegemea na uzalishaji mali kupitia Jeshi la Kujenga Taifa.
- Kushiriki ulinzi wa amani kimataifa