Kwanini Bosi wa TAKUKURU anavaa sare za Jeshi? Nini taswira ya Utawala wa Kiraia?

Kwani hakuna watz wenye uwezo wa hizi nafasi mpaka sinia officer wa jeshi watake over hayo majukum
Logically wao wamekuwa trained kuenforce zaidi badala ya logic implementation

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
Nani alikuambia....
Jeshini wanasoma uongozi tena hutoa viongozi wazuri sana.
Wametuletea Kikwete,kinana
 
Yule Kamishna General wa Megereza hivi hiwa anavaa nguo za JW?
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Thobias Andengenye hivi huwa anavaa sare za Polisi?
Mkurugenzi wa Usalama wa taifa hivi bado anavaa sare za Polisi?
Yule Mkuu wa Magereza huwa anavaa ndio kulingana na tukio, wkati anaenda kuvaa cheo kipya cha JWTZ alivaa gwanda za JWTZ ndio kvs. lkn pia akiwa ktk shughuli zake huko Magereza havai kwa kuwa Magereza kuna uniform, ila TAKUKURU hamna uniform hivyo Brigedia akivaa gwanda zake za Jeshi n sahihi tu. na Hao wengine uliowataja kutokuvaa kwao hakuhalalishi kuwa wengine wasivae
 
Huyu ni mwanajeshi bado hajastaafu utumishi wa jeshi ila ni utashi wake kuvaa sare, ilitakiwa avae sare kama za TAKUKURU ambapo ndo idala yake mpya
 
Nani alikuambia....
Jeshini wanasoma uongozi tena hutoa viongozi wazuri sana.
Wametuletea Kikwete,kinana
Hujanielewa mkuu kusomea uongozi na kuimplement ni vitu viwili tofauti
.
Kana mwalimu wangu ni mtunzi mzuri wavitabu vya ethics lakini yye hana ethics even a single one
Sihitaji kumtaja hapa wenye kujua wanamjua

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Yule Mkuu wa Magereza huwa anavaa ndio kulingana na tukio, wkati anaenda kuvaa cheo kipya cha JWTZ alivaa gwanda za JWTZ ndio kvs. lkn pia akiwa ktk shughuli zake huko Magereza havai kwa kuwa Magereza kuna uniform, ila TAKUKURU hamna uniform hivyo Brigedia akivaa gwanda zake za Jeshi n sahihi tu. na Hao wengine uliowataja kutokuvaa kwao hakuhalalishi kuwa wengine wasivae
Hayo magwanda wakavae huko jeshini na sio kwa ofisi za umma wao waliteuliwa kuwa wajeda Basi wafanye yanayo wahusu wasiingilie shughuli za raia, tunahitaji taasisi imara na sio individual people wanaovaa magwanda, pia nchi yetu haiongozwi na jeshi Una utawala halali wa kiraia
 
kwani, kuna sehemu katika Katiba inakataza Mwanajeshi kuwa Boss wa T

Wajibu wa JWTZ​

  • Kulinda Katiba na Uhuru wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
  • Ulinzi wa mipaka ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
  • Kufanya mafunzo na mazoezi ili kujiweka tayari kivita wakati wote.
  • Kufundisha umma shughuli za ulinzi wa Taifa.
  • Kushirikiana na mamlaka za kiraia katika kutoa misaada ya kibinadamu na uokoaji wakati wa maafa
  • Kutoa huduma mbalimbali za kijamii.
  • Kukuza elimu ya kujitegemea na uzalishaji mali kupitia Jeshi la Kujenga Taifa.
  • Kushiriki ulinzi wa amani kimataifa.
 
View attachment 1739305
Brigedia John Mbungo, Mkurugenzi Takukuru.

Teuzi za wanajeshi zilishamirishwa na hulka ya Mtawala aliyepita , Hayati John P. Magufuli ambaye aliamini katika matumizi ya vitisho, nguvu na mabavu katika uendeshaji wa shughuli za Serikali.

Je bado CCM na Mh. Samia Suluhu Hassan wanaona fahari kwa Viongozi wa kiserikali kuendelea kuvaa kombati katika shughuli za kiraia ?

Kwani akivalia hivyo Kijeshi anazuia nini katika Ustawi wako mzima wa Kimaisha unaouhisha Wewe Kula, Kufurahia, Kujipatia Pesa na hadi Kumbandua ( Kumtia ) Mkeo / Hawara?
 
Wewe unatumia Logic??
  • Kulinda Katiba na Uhuru wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
  • Ulinzi wa mipaka ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
  • Kufanya mafunzo na mazoezi ili kujiweka tayari kivita wakati wote.
  • Kufundisha umma shughuli za ulinzi wa Taifa.
  • Kushirikiana na mamlaka za kiraia katika kutoa misaada ya kibinadamu na uokoaji wakati wa maafa
  • Kutoa huduma mbalimbali za kijamii.
  • Kukuza elimu ya kujitegemea na uzalishaji mali kupitia Jeshi la Kujenga Taifa.
  • Kushiriki ulinzi wa amani kimataifa.
 
View attachment 1739305
Brigedia John Mbungo, Mkurugenzi Takukuru.

Teuzi za wanajeshi zilishamirishwa na hulka ya Mtawala aliyepita , Hayati John P. Magufuli ambaye aliamini katika matumizi ya vitisho, nguvu na mabavu katika uendeshaji wa shughuli za Serikali.

Je bado CCM na Mh. Samia Suluhu Hassan wanaona fahari kwa Viongozi wa kiserikali kuendelea kuvaa kombati katika shughuli za kiraia ?
Nilishangazwa na Kuchukizwa MWANAJESHI JWTZ kuteuliwa kuwa Mkuu wa Magereza

Hii ni dharau kubwa sana kwa jeshi la Magereza na walilalamika ila Jiwe alifunga masikio
 
Mbona magwanda yenu makamanda mnayavaa Hadi kwenye misiba na hujawahi kumhoji Mbowe?

Sent from my TECNO RA7 using JamiiForums mobile app
 
Yule Kamishna General wa Megereza hivi hiwa anavaa nguo za JW?
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Thobias Andengenye hivi huwa anavaa sare za Polisi?
Mkurugenzi wa Usalama wa taifa hivi bado anavaa sare za Polisi?
Umesahau hapo na RC wa Kagera Brigadia Gaguti .Labda huwafuatilii,ila wanavaa sana tu. Diwani ndiye huwa havai.ila hao wengine huwa wanavaa.Huyo wa magereza huwa anavaa zote,kuna siku avaa za magereza na kuna siku anavaa bakabaka
 
Je kulikuwa na sababu gani kuanza kuwatumia wanajeshi katika kazi za kiraia ? Kwamba Jeshi ndio lina uzalendo ? Au wasio wanajeshi sio Wazalendo ? Nahitaji kufahamu tija hasa ni ipi ?
Mh. alijibu iwe rahisi anapotaka kumkamata mwanajeshi anayekabiliwa na tuhuma za rushwa kwanza anapiga saluti halafu anakamatwa. Simple.

Sent from my TECNO RA7 using JamiiForums mobile app
 
huo wajibu je kuna sehem inakataza wao kuwa viongozi ktk Taasisi zingine? lakini pia je akichukuliwa mtumishi mfano wa halmashauri kwenda kuwa Boss wa TAKUKURU ndio sawa kuliko akitoka Jeshini?
 
Nilishangazwa na Kuchukizwa MWANAJESHI JWTZ kuteuliwa kuwa Mkuu wa Magereza

Hii ni dharau kubwa sana kwa jeshi la Magereza na walilalamika ila Jiwe alifunga masikio
Na afisa wa magereza alivoteuliwa kuwa mkuu wa jeshi la Zimamoto vp walilalamika napo?.

Magereza kulikuwa na madudu sana ambayo walikuwa wanalindana wenyewe kwa wenyewe.Ndio maana mzee kaamua kuleta mtu kutoka kabila lingine. Ingekuwa ameletwa Raia sawa.
 
Back
Top Bottom