Kwanini Bosi wa TAKUKURU anavaa sare za Jeshi? Nini taswira ya Utawala wa Kiraia?

..wakati wa Mwalimu tulikuwa na kikosi maalum cha kuzuia rushwa. Baadae ndiyo kikabadilishwa jina na kuwa Takukuru.

..Nakumbuka Colonel Ali Maftaha ndio alikuwa muasisi lakini hakuwa akivaa uniform za jeshi.

..baadae alikuwepo Major General Kamazima, naye hakuwa akivaa uniform za jeshi.

..hata mimi sikubaliani na utaratibu wa maafande wanaoongoza taasisi za kiraia kuvalia kijeshi.

..huu ni utaratibu ambao umeibuka ktk awamu ya 5. Awamu zilizopita maafande walikuwa wakiteuliwa kuongoza idara / taasisi za kiraia lakini hawakuwa wakivaa sare za jeshi.
 
..kuna wakati tulikuwa na Jaji Mkuu[ Znz na Tz] ana cheo cha Brigedia Jenerali. Je, angekuwa sahihi kuvaa kombati ktk majukumu yake mahakama kuu?

..Hakuna anayepinga askari kuteuliwa kuongoza taasisi za huku uraiani.

..Tatizo ni uvaaji wao wa sare za kijeshi ktk taasisi hizo.

..Nadhani yakitokea matatizo ktk taasisi hizo tutaanza kulilaumu jeshi.

..kuna kipindi bosi wa Takukuru alikuwa anaenenda kisiasa-siasa huku amevalia combat fatigues za Jwtz. Kitendo kile hakikuwa sahihi.
 
Huyo sio raia ni mwanajeshi tena senior officer na hajastaafu sasa ulitaka aende kazini kavaa msuli?? Kwani mavazi yana athiri nn?? Na pia si mwanajeshi wa nchi hii hii sasa shida iko?? Haya sema ww ulitaka avae nn??
 
Kwa taharifa yako hakuna mtu wanaomkubali kama huyo alieteuliwa (m JWTZ) kua mkuu wa magereza amewarekibishia mambo yao mengi tu,in fact wanajeshi wakipewa sehemu kusimamia hua hawapindishi japo katiba ya nchi hairuhusu hilo.
We ndo msemaji wao??
 
Huyo sio raia ni mwanajeshi tena senior officer na hajastaafu sasa ulitaka aende kazini kavaa msuli?? Kwani mavazi yana athiri nn?? Na pia si mwanajeshi wa nchi hii hii sasa shida iko?? Haya sema ww ulitaka avae nn??

..anavaa sare za jeshi halafu anafanya siasa ktk nafasi aliyoteuliwa.

..mnakumbuka alivyokuwa analumbana na viongozi wa cdm wakati tunakaribia kampeni za uchaguzi 2020?

..sasa kule siyo kuchafua taswira nzuri ya Jwtz?
 
Kama anafanya siasa hili siwezi ingilia maana sijaona..ila kama ni kuvaa tu kwenda kazini kwake ofisi za pccb sidhani kama ina maana mbaya mkuu
 
Kama anafanya siasa hili siwezi ingilia maana sijaona..ila kama ni kuvaa tu kwenda kazini kwake ofisi za pccb sidhani kama ina maana mbaya mkuu

..Augustino Ramadhani alikuwa na cheo cha Brig.Gen wa Jwtz, na Jaji Mkuu wa Znz.

..Je, angekuwa anavaa kijeshi mahakamani ingeleta tafsiri nzuri?
 
Je, kulikuwa na sababu gani kuanza kuwatumia wanajeshi katika kazi za kiraia? Kwamba Jeshi ndio lina uzalendo? Au wasio wanajeshi sio Wazalendo ? Nahitaji kufahamu tija hasa ni ipi?
Haikuanza jana. Muhidin Kimario aliwahi kuwa mkuu wa mkoa Tabora, Mwanza.
Kanali Isdory Shirima ( Mara Mtwara)
Yusuph Makamba ( Kigoma)
Zellothe Steven ( mbeya)
Nsa Kaisii ( Mara)
Wapo wengi Sarakikya balozi Nigeria ( Nyerere)
 
Je, kulikuwa na sababu gani kuanza kuwatumia wanajeshi katika kazi za kiraia? Kwamba Jeshi ndio lina uzalendo? Au wasio wanajeshi sio Wazalendo ? Nahitaji kufahamu tija hasa ni ipi?
Wanajeshi ni watiifu, wakipewa order wanatekeleza ipasavyo...wapo hivyo siku zote. Kufanya kazi kwa weledi na kwa uzalendo. Naona mzee aliamua kuwatumia hao ili kujiepusha na sisi wengine wavivu.

Sent from my Infinix X5515 using JamiiForums mobile app
 
Huyu John Mbungo ni mtu wa wapi? Ila akipiga kombati anatokelezea kweli
 
Hili halina muda... Kuna mabadiliko mengi makubwa yanakuja... Jeshi litatengwa na shughuli na siasa na utawala libaki na dhima yake ya ulinzi na usalama
Kina kandoro na kiwhelu walikuwa raia wa kawaida? Rais ana uwezo wa kumteua yeyote anayeona anafaa hata wewe kwa nafasi fulani, teuzi za jeshi zilikuwepo tu
 
Takukuru ina historia ya kuwa na viongozi ambao ni Major Generals.
 
Watanzania ni washamba sana hata Viongozi wetu maana hawajui Uniform ni vazi la utambulisho wa kazi ya anayevaa ili aweze kukimbiliwa wakati wa dharura kwa msaada. Majeshi, Hospitali, Shule nk ni kati ya Taasisi za Serikali zinazovaa Uniform kazini au nje ya maeneo ya kazi kama lazima lakini kwenye nchi za wenzetu tulikoiga, ni Polisi tu ndo wanavaa Uniform popote hata mitaani. Mwanajeshi au Polisi akiteuliwa kwa kazi ya kiraia haruhusiwi kuvaa vazi lolote la kijeshi kazini hata mitaani ingawa atakuwa bado ana Uniform nyumbani na kama kazi yake mpya ina vazi lake basi atapewa. Tanzania utakuta . Mkuu wa Mkoa utakuta amevaa Combat ofisini!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…