Kwanini Bunge linawakumbatia Wabunge wasio na sifa?

Kwanini Bunge linawakumbatia Wabunge wasio na sifa?

Kama wasingeingia huko bungeni ndio ingekuwa matokeo ya uchaguzi hamkuibiwa?

Au kitu gani kingebadilika?

Chadema wamesusa ila kila siku wako kwenye mitandao kushauri serikali, sasa wanashauri serikali ipi wakati uchunguzi hawautambui?
Bwana mdogo uelewa wako ni hafifu sana. unajua maana ya NENO kuhalalisha Lakini??
 
Ela inatoka wapi?
Suala la kuweka mambo Sawa ni kurudia uchaguzi. Wote ni wabunge haramu hawakupatikana Kwa njia Halali. Ikiwepo hata Rais mwenye. Wale COVID 19 wapo mle kuharalisha ule uchaguzi uliofanyika October mwaka Jana
 
Kimsingi hawajafukuzwa.... La sivyo wasingekuwa bungeni....

Hahahaaa.....
Watakuwa wamepewa taraka, wale wapo bungeni kwa sababu maalum, Spika na tume ya uchafuzi wanafahamu vizuri wanachokitenda..! Hata kesi ifunguliwe kwa bunge na tume kukiuka katiba ya nchi hawawezi kuondolewa maana kesi ikifungiliwa itapelekwa kwa FELESHI itapigwa dana dana mpaka miaka 5 iishe..
Nchi yetu kwa ujumla kuanzia wananchi wote, viongozi wake, watunga sera na viongozi wa dini hawajui umuhimu wa kulinda katiba wala kufuata katiba bali wengi tupo kwa hisani ya mtu fulani kuangalia anapenda nini na sisi tunageuka kufuata upepo na maelekezo yake hata anavunja katiba. Pia sisi wananchi, viongozi na watu muhimu wa taifa hili asilimia kubwa tumetawaliwa na njaa ya hela zaidi kuliko utu ama utii wa taifa wengi tunatanguliza uzalendo kwa chama zaidi kuliko uzalendo kwa taifa letu pendwa. Ndio maana watu wanaona Ndugai anavyochezea katiba yetu lakini tupo kimya nisije nikamkosea bwana mkubwa nikakosa teuzi either ndani ya chama au serikali.
 
Kama wasingeingia huko bungeni ndio ingekuwa matokeo ya uchaguzi hamkuibiwa?

Au kitu gani kingebadilika?

Chadema wamesusa ila kila siku wako kwenye mitandao kushauri serikali, sasa wanashauri serikali ipi wakati uchunguzi hawautambui?
Anayekudanganya serikali inatikana na uchaguzi pekee ni Nani We Kanjanja?
 
Suala la kuweka mambo Sawa ni kurudia uchaguzi. Wote ni wabunge haramu hawakupatikana Kwa njia Halali. Ikiwepo hata Rais mwenye. Wale COVID 19 wapo mle kuharalisha ule uchaguzi uliofanyika October mwaka Jana

Tukiwaendekeza chadema kwa staili hiyo tutakuwa tunafanya uchaguzi kila siku, kutaka kuwaridhisha chadema then inatakiwa mambo yote yasimame tufanye wanachotaka
 
Mwanasheria Mkuu wa Serikali yupo Bungeni Wabungeni Wasio na Vyama anashinda Nao Spika yumo Bungeni yeye ndiye Anawakumbatia kwanini?

Hamna hoja nyingine ya kuongea,
Wao wakitoka eh chadema ndio inakuwa imeshinda urais?

Coz wale wanaweza kutoka na rais akawateua kuwa wakurugenzi au mabalozi na ww ukaendelea kubaki hapo hapo na tekno yako

Tuache wivu jaman kuna mambo mengi ya kujadili
 
Wakuu pengine tujadili kidogo kua kwa nini Bunge kinawakumbatia wabunge wasio na sifa za ubunge.

Naibu spika wa bunge Dr. Tulia Ackson naona anawakumbatia wabunge hao.
Je, nini maoni yako? Tujadili hili.
Ili kutimiza ile sheria ya usimamizi ya mahesabu ya serikali za kitaa PAC na LAAC maana kule bungeni husimamiwa na upinzani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Coz sababu za kuwavua uanachama wao sio za msingi,

Hata wakina silinde walilindwa na spika wakati ule mbowe amepiga bia zake anaawambia wabunge wote watoke nje ya bunge kisa kuna corona

Viti maalum ni takwa la kikatiba, na wakina mdee wamefukuzwa just because wametii katiba
Hujui lolote
 
Hao wabunge wanachama na chama chao ni CCM subirini 2025 ndio mtawaona wakimeremeta na kijani na njano wakimfanyia kampeni mama yetu Samia.
 
Kwa sasa tutaendelea hivi hivi
Hakuna katiba mpya wala tume nyingine, hili la tume ni maalum kwa ajili ya kuwafurahisha chadema no way

As long as mambo yanakwenda basi acha twende
Sasa nchi ikiwa na wananchi sampuli ya huyu mtapigaJe hatua ?!. Never
 
Sasa nchi ikiwa na wananchi sampuli ya huyu mtapigaJe hatua ?!. Never

Kupiga hatua ni kuwa na tume mpya? Kupiga hatua ni kuwa na katiba mpya? Nyie mnataka tume mpya kwa manufaa yenu ya kichama, sisi kama wanainchi tume mpya ya uchaguzi ya nn
 
Kupiga hatua ni kuwa na tume mpya? Kupiga hatua ni kuwa na katiba mpya? Nyie mnataka tume mpya kwa manufaa yenu ya kichama, sisi kama wanainchi tume mpya ya uchaguzi ya nn
Hujui kuwa kuwa na democracy iliokomaa isiyo na uonevu nayo ni maendeleo ?![emoji174]. Twaweza hawakukosea
 
Back
Top Bottom