Kwanini CHADEMA ina ushawishi Mkubwa katika Chama cha Wanasheria(TLS) nchini?

Kwanini CHADEMA ina ushawishi Mkubwa katika Chama cha Wanasheria(TLS) nchini?

Sabato Njema!

Kama swali linavyoeleza Hapo juu.
Kûna MTU anaweza kuniambia nini kinapelelea CHADEMA kuwa na ushawishi ndani ya Chama kikubwa cha TLS chenye Taaluma muhimu ndàni ya nchi?

Nakabidhi Maiki kwèñu wataalamu.



Kiufupi ni kuwa chadema ni cha watu walioenda shule na TLS all of them ni elites so ni rahisi kuwa na influence huko.

Kwanini labda Chadema haina ushawishi katika vyama vingine Kama CWT n.k

Kwanza wanachama asilimia kubwa ya CWT ni Watumishi wa serikali tofauti na TLS ambao ni watu huru waliojiajiri.


Kitendo cha kuwa huru umejiajiri haupo chini ya serikali maana yake unaweza kuwa logically na kuleta positive impact .
 
Kiufupi ni kuwa chadema ni cha watu walioenda shule na TLS all of them ni elites so ni rahisi kuwa na influence huko.
CCM ni chama cha watu wote. Walioenda na ambao hawajaenda shule. Inatusaidia sana kupata kura nyingi kwenye uchaguzi mkuu. CHADEMA iendelee kujikita kwa wasomi na iachane na makundi mengine wanayoona ni ya wajinga.
 
Lakini kutokuwa na ushawishi Kwa wanasheria siô dalili nzuri Kwa sababu Moja ya Kada nyeti naya lazima kwèñye siasa NI Sheria.

Kukosa uungwaji mkono na wanasheria haina maana nzuri kisiasa
Mkuu kwenye siasa kikubwa ni namba. CCM inaungwa mkono na makundi mengi mno yanayofanya ishinde uchaguzi kirahisi. Kura za wahadzabe peke yao ni nyingi kuliko za wanasheria wote nchini hali inayowafanya waahadzabe wawe wa muhimu kuliko wanasheria. Pia kada zote ni nyeti. Hakuna kada yenye umuhimu kuliko nyingine.
 
Wanasheria wanafundishwa kitu kinaitwa logic thinking!

Kuna kitu wanafundishwa kinaitwa to think as a reasonable person!

Hapa ndo ililo tofauti kati ya Wanasheria na professionals wengine. Wanasheria wanafikiri sana kwenye kufanya maamuzi!

Tuache uongo kwa mtu mwenye akili timamu na anayefikiri vizuri, ni ngumu sana kushawishiwa na CCM. Huo ndo ukweli.

Hata Duniani huko, mapinduzi makubwa yalisababishwa na Wanasheria!
 
Sabato Njema!

Kama swali linavyoeleza Hapo juu.
Kûna MTU anaweza kuniambia nini kinapelelea CHADEMA kuwa na ushawishi ndani ya Chama kikubwa cha TLS chenye Taaluma muhimu ndàni ya nchi?

Nakabidhi Maiki kwèñu wataalamu.
Siyo suala la ushawishi, Bali ni Kwa kuwa huko TLS ndiko Kwenye uchaguzi ulio huru na haki.

Hujawahi msikia Katibu Mwenezi wa CCM wa wakati wa Magufuli, Humphrey Polelpole, akieleza kuwa iwapo uchaguzi Mkuu wa nchi hii utakuwa huru na haki, basi CCM ijandae kukabidhi madaraka ya nchi??😚

Huo ndiyo ukweli mchungu, ambao hata wao wenyewe CCM wanaujua

Jiulize ni kwanini CCM hawataki hata kusikia suala la kuundwa Kwa Katiba mpya, itakayotuletea Tume huru ya uchaguzi??

Jibu utakalopata hapo, ndipo ujue kuwa chaguzi zote, hao CCM, huwa wanashinda Kwa goli la mkono😎
 
Back
Top Bottom