Wanabodi,
Determinant ya Rais wa Tanzania ni Kanda ya Ziwa.
Determinant ya nani anakuwa rais wa nchi hii, ni wapiga kura wa Kanda ya Ziwa ambayo ndiyo inayoongoza kwa idadi kubwa ya watu!. Kati ya watu milioni 40 wa sensa ya mwaka 2002 kwa Tanzania yenye makabila 120, Wasukuma peke yao wako milioni 10!. Sasa ukiwajumlisha na Kanda ya Kaskazini, hata kama mikoa yote iliyobakia wataipigia kura CCM, bado kwa kanda hizo mbili pekee, zinatosha kabisa kuipiga chini CCM!, hivyo CCM kwa kulitambua hili, itatumia nguvu yake yote, all its mighty powers by all means, by hooks and crooks kuyakomboa majimbo haya matatu ya Kanda ya Ziwa, na naomba mshishangae, kama ili kujiokoa, CCM inaweza kabisa kutafuta mgombea wa urais kutoka kanda hii ya Ziwa ili kujiokoa kwa kuwahonga watu wa kanda ya Ziwa kwa hongo kubwa kabisa ya mgombea urais, hiyo watu kama John Pombe Magufuli, Andrew Chenge, Laurent Masha, Ngeleja, Kitwanga, are men to watch very closely, hata kama mgombea huyo atakuwa hana sifa za kutosha kuwa rais bora, kwa CCM iko tayari kutupatia bora rais as long as atatoka Kanda ya Ziwa kuliko kuanguka huku inajiangalia!, kwa CCM kinachotakiwa ni ushindi na sio sifa za mgombea!, the end justifies the means.
Mwelekeo huu ni uthibitisho kuwa ule ukombozi wa pili wa kweli wa Mtanzania, sio ndoto tena, ni kitu ambacho kinawezekana kabisa kutokea kama upinzani utajitambua kwa kushikilia kwa makini kile kilicho mkononi na kuongeza juhudi za kuimililki kanda ya Ziwa, hivyo vita kuu ya kisiasa nchini Tanzania kuelekea 2015 ni nani ataimiliki Kanda ya Ziwa. Chadema ikifanikiwa, CCM inapigwa chini, ila CCM ikifanikiwa kuikomboa Kanda ya Ziwa, then 2015 ni CCM tena, na kitakacho fuatia kwa CCM ya 2015 ni kuikomboa Kanda ya Kaskazini na kusema ukweli hii ndio itakuwa kazi ngumu kweli kweli, ila kama itatumika ile 'universal language', kuna msemo "hakuna mkate mgumu mbele ya chai", mkate hata uwe mgumu vipi ukiuchovya ndani ya chai, unalainika!
Tuache Siasa za Ukanda na Ukabila, au Tuzidumishe Ili Mtu wa Kanda/Kabila Yetu Ndie Ashinde?.
Natoa mwito kwa Watanzania wenye mapenzi mema na nchi yetu, tusiendekeze hizi siasa za Ukanda, zitajenga chuki za kukichukia chama fulani bila sababu za msingi ya chuki hiyo, au kukipenda na kikishabikia chama fulani kwa upenzi tuu, matokeo ya mwisho ya siasa hizi ni kujengeana chuki zisizo na sababu!. Tupingane bila kupigana, tutofautiane kisiasa bila kuchukiana bali tupingane kwa hoja huku tukipendana!.
Hata mimi uchaguzi wa Arumeru, nilisimama na Sioi, tumekutana na Nasari pale Bungeni Dodoma, tumekumbatiana, na kiukweli kutoka moyoni mwangu, sina chuki na Nasari, namkubali sana tuu kwa dhati na kupongeza kwa ushindi, huku nikiendelea kushikamana na Sioi kwa sababu ni rafiki!.
Wito Kwa Watu wa Kanda ya Kaskazini
Wito wangu kwa nyie watu wa Kanda ya Kaskazini, Kanda yenu ndio imependelewa sana, inaongoza kwa mashule na wasomi, inaongoza kwa mahospitali!, KCMC, Mawenzi, Kibongoto, Mt. Meru, Seliani, Dareda, etc, Inaongoza kwa vivutio vya utalii, Mt. Kilimanjaro, Mt. Meru, Serengeti, Ngorongoro, Seronera, Manyara, Inaongoza kwa barabara za lami hadi vijijini, inaongoza kwa umeme vijijini, inaongoza kwa maendeleo, inaongoza kwa kutoa wanawake wife material, ukioa mchagga umeoa maendeleo, hivyo msiichukie hivyo CCM, kwani pamoja na mabaya yake yote ya CCM, kulea rushwa na ufisadi na kutuletea umasikini na kulea ujinga kwa kuutumia kama mtaji wake wa ushindi, pia kuna mema na mazuri yake mengi ambayo CCM imelifanyia taifa hili ikiwemo kutuletea maendeleo japo kiduchu, lakini pia imetuletea hazina ya amani na utulivu ambazo ni tunu kubwa kuliko maendeleo, hivyo tuichukie CCM kwa mabaya yake na kupenda kwa mema na mazuri yake!.
Wito Kwa Wa Kanda ya Ziwa.
Tusikubali kutumiwa kama ngazi ya wengine kupandia kisiasa, kwa vile na mimi ni mtu wa Kanda hii na sisi ndio determinant ya nani anashinda na kukikalia kile kiti cha ikulu yetu, tusikubali kuendelea kutumika tuu kama ngazi kwa wengine kupandia, au kuendelea kuwa na upendo wa mshumaa kumulikia wengine huku kwetu kunateketea, Kanda hii ndio Kanda yenye watu wengi, ndio Kanda yenye mijitu yenye nguvu inayokula na kushiba, ndio Kanda tajiri kuliko Kanda zote, ndio yenye madini ya dhahabu na almasi, ndio wenye Ziwa Victoria lenye samaki watamu Sato, tusikubali kutumiwa kama dodoki kuwasafishia wengine au dekio baada ya deki linatupwa kule, sisi tuna kila aina ya utajiri lakini very unfortunately watu wetu ni masikini wa kutupwa!. Angalia wenzetu wa Kaskazini mbona wameweza kulibwaga hili lidubwana na wanapata maendeleo, na sisi tuamue kulibwaga unless kama 2015 atakuwa ni mmoja wetu!.
Namalizia kwa kusisitiza, huu ni mtazamo tuu!
Wasalaam.
Paskali