Kwanini CHADEMA inaanzia Mikutano Kanda ya ziwa?

Kwanini CHADEMA inaanzia Mikutano Kanda ya ziwa?

kanda ya ziwa imebeba mikoa hii.
👇
Mwanza,Mara,Shinyanga,Geita,Simiyu,Kagera.,,lakini pia mikoa ya jirani ambayo inamuingiliano na kanda ya ziwa hususan Mwanza ambayo ndo kitovu cha kanda ya ziwa ni Tabora,Kigoma,Singida.

kanda ya ziwa ndo ukanda wenye mikoa mingi na wabunge wake wameonyesha kuwa na kauli zenye ushawishi kwa kuisimamia serikali wakiwa Bungeni.
 
Najaribu kufikiri na kuwaza kwanini Chadema inaanzia mikutano yake Mwanza? Kwanini siyo makao makuu ya nchi Dodoma? Kwanini siyo Dar Mbako viongozi wengi Wa Chadema wanaishi? Kwanini siyo Moshi Arusha Mbako mawazo ya kuzaliwa Chadema yalianzia.swali kwanini iwe Mwanza? Aliye majibu anijibu naomba.
Hii nayo ni post? Mod huyu anajaza servet tu , hakuna kitu hapa
 
Najaribu kufikiri na kuwaza kwanini Chadema inaanzia mikutano yake Mwanza? Kwanini siyo makao makuu ya nchi Dodoma? Kwanini siyo Dar Mbako viongozi wengi Wa Chadema wanaishi? Kwanini siyo Moshi Arusha Mbako mawazo ya kuzaliwa Chadema yalianzia.swali kwanini iwe Mwanza? Aliye majibu anijibu naomba.

Ni uamuzi tu, kama vile royal tour ilivyoanzia kuonyeshwa Marekani. Kwani unaumia boss?
 
Najaribu kufikiri na kuwaza kwanini Chadema inaanzia mikutano yake Mwanza? Kwanini siyo makao makuu ya nchi Dodoma? Kwanini siyo Dar Mbako viongozi wengi Wa Chadema wanaishi? Kwanini siyo Moshi Arusha Mbako mawazo ya kuzaliwa Chadema yalianzia.swali kwanini iwe Mwanza? Aliye majibu anijibu naomba.
Sababu ni hii....
Jee Watanzania hawana kanda zao?. JK Nyerere alitoka kanda ya Ziwa, Mwinyi akatoka Zanzibar, Ben akatoka kanda ya Kusini, JK ametoka kanda ya Mashariki, Kanda ya Kati by now bado haina mtu mwenye caliber na uwezo wa kuwa rais wa JMT kwa sasa (sorry), hivyo kanda zilizobakia ambazo bado hazijatoa rais ni Kanda ya Ziwa na Kanda ya Kaskazini!, hivyo rais wa 2015 lazima atoke ama Kanda ya Ziwa, ama Kanda ya Kaskazini!. Kwa vile Kanda ya Kaskazi inaelezwa kulaaniwa na Nyerere kufuatia kisa cha Mangi Mkuu Thomas Marealle kumkwamisha Nyerere kwa kutaka Kanda hiyo ndio ipewe uhuru kwanza kwa hoja Tanganyika as a whole bado haijawa tayari, hivyo sasa rais wa 2015 lazima atoke Kanda ya Ziwa!.

Paskali

Rejea
Tupende, tusipende: Tanzania inanyemelewa na udini! | Page 42 ...
Jinamizi la Udini Tanzania: Utabiri wa Sheikh Suleiman Takadir ...
Mkuu wa Mkoa wa Arusha na ukabila; Ukemewe na kila mmoja wetu ...
Ni upuuzi kuwagawa watanzania kikanda,kikabila na kidini ...
Ni kweli kuna makabila yasiyotakiwa kutoa rais wa nchi? | Page 7 ...
Hatimaye kile kitendawili cha Mikutano ya hadhara sasa rasmi kimeteguliwa , hii ni baada ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo kutoa Ratiba yake .

Taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Itifaki wa Chama hicho John Mrema imedai kwamba , Jiji la Mwanza limeteuliwa kuwa la Kwanza kwa Chadema kufanya mkutano wake wa Hadhara , Mkutano huo unaotarajiwa kuvunja rekodi ya Kitaifa ya Mikutano ya hadhara tangu kuvumbuliwa kwa Tanzania utafanyika tarehe 21/01/2023 .

Mungu ibariki Chadema
Kwa kweli nawapongeza sana kuanzia Mwanza, kwasababu sasa hatimaye Chadema imejitambua na kujua kanda determinant za ushindi kwa uchaguzi wa urais Tanzania ni kanda gani, hivyo wameanzia hapa.
Ushauri huu ulitolewa siku nyingi nyuma!. Mwaka 2010 nilipandisha bandiko hili, CCM Imechokwa, CHADEMA Haijajipanga! humo nikasema
Wanabodi,

Hakuna ubishi, Chadema imenyanyuka, toka wabunge 5 mpaka 22 wa kuchaguliwa tena majimbo ya haja yenye impact ikiwemo kuyashika majiji makubwa katika mikoa the big five!, huku sio kukua bali ni kupaa, tatizo kubwa la Chadema, bado hawajipanga mkao wa kichama tawala, ili kikabidhiwe nchi, kitawale, Chadema bado kimekaa kichama harakati, hivyo kuna wengi wanakiona kama bado hakijakomaa kiasi cha kukabidhiwa ikulu yetu!.

Kichama, wanachadema mkubali msikubali, chama chenu kwa sasa japo kipo juu, lakini bado hamjakomaa kufikia kiwango cha kukabidhiwa nchi, bado mko kiuana harakati zaidi kuliko ki chama tawala, na hamjajipanga kwa sura ya kitaifa na utayari wa kutawala nchi.

Kwa vile CCM imechokwa na imekaa mkao wa kifo, hii ndio opportunity yenu Chadema kuongeza offensive ili kuisindikiza CCM kaburini, kwa kujipanga kimkakati ili muwe na sura ya kitaifa, kwa kuonyesha Watanzania kuwa mmekomaa na mko tayari kutawala, hivyo Watanzania watawamini watawakabidhi nchi mwaka 2015.

Sehemu muhimu kabisa kwa Chadema to keep watch kuhakikisha hamuiachii ni hiyo Kanda ya Ziwa ambayo imeipokonya CCM na kuishika, hii ndio Kanda determinant ya nani anakuwa rais wa nchi hii. Aliyeishika Kanda ya Ziwa ndio rais wa Tanzania. Hivyo CCM imeumia sana kupoteza Kanda ya Ziwa na wataelekeza all it might powers to reclaim what it has lost, hivyo Chadema itumie uwezo wake wote kulinda what it has!.

Kwa upande wa Chadema, lazima kibadilike, first and foremost, anzeni na Mwenyekiti wenu Freeman Mbowe, he should go!. Ajiuzulu uenyekiti, ampishe more able person kama Dr. Slaa kwenye usukani wa chama, Katibu Mkuu mpeni Zitto strategically, hii itaifuta ile dhana ya nepotisim kwenye chama chenu, na kulivua lile koti la ukanda na ukabila ili walioichoka CCM wawafungulie mikono kwa kujitokeza kwa wingi kuwapigia kura 2015 kwa kujionyesha Chadema ni chama cha wote, dini zote na kanda zote.

Kupumzishwa kwa Freeman Mbowe sio kuwa hafai no, anafaa sana lakini kwa background yake na nature ya kazi zake, as a businessman, hapo alipoifikisha Chadema amaishafanya kazi kubwa na kufikia mwisho wa uwezo wake. Kwa background yake ya a former DJ na sasa ni mfanyabiashara, focus ya wafanyabiashara kote dunia nzima ni maximisation of profits, hivyo Mbowe atahitaji ruzuku ya Chadema itumike kuivest kwenye assets, kwenye vitu vya kuonekanika yaani assets kama magari, mavazi, etc

Ili Chadema kiweze kushika nchi 2015, it has to invest on people na sio ku invest kwenye vitu. Chadema must invest kwenye mass mobilisation na sio kutegemea mikutano ya hadhara na maandamano. Chadema needs to have able people kuiwezesha kushika dola five years to come kwa kutumia reaching out mechanism kuwafikia the mases kwa kumiliki media yake yenyewe. Chadema lazima ifanye recruitment ya able people, watakaokuja kuendesha serikali ya Chadema. Mbowe hawezi kukubali ruzuku ya Chadema itumike to invest on people, it's a loss making venture kwa mfanyabiashara na kuivest kwenye mass media sio profitable investment kwa business man ambaye ni in for profit making. Dr.Slaa na Zitto sio wafanyabiashara hawa ni ma technocrats. Chama kishikwe na wanasiasa watendaji sio wanasiasa wafanyabiashara. Chadema iwekeze kwenye watu na kupanua mtandao wake hadi vijijini, ili kwenda kuiongoa CCM kuanzia kule chini kabisa kwenye mizizi yake ambako ni kule kwenye mashina. Chadema imiliki media yake yenyeshe for mass mobilization na sio kutegemea mikutano na maandamano, huko ni kuendeleza uanaharakati, Chadema inatakiwa kukaa mkao wa kutawala, ikitangaza kitu, kinafika Tanzania nzima!.
Paskali
Mwaka 2012, nikapandisha uzi huu
Mtazamo: Kanda ya Kaskazini, CCM imechokwa mpaka basi! humo nilisema
Wanabodi,
Determinant ya Rais wa Tanzania ni Kanda ya Ziwa.
Determinant ya nani anakuwa rais wa nchi hii, ni wapiga kura wa Kanda ya Ziwa ambayo ndiyo inayoongoza kwa idadi kubwa ya watu!. Kati ya watu milioni 40 wa sensa ya mwaka 2002 kwa Tanzania yenye makabila 120, Wasukuma peke yao wako milioni 10!. Sasa ukiwajumlisha na Kanda ya Kaskazini, hata kama mikoa yote iliyobakia wataipigia kura CCM, bado kwa kanda hizo mbili pekee, zinatosha kabisa kuipiga chini CCM!, hivyo CCM kwa kulitambua hili, itatumia nguvu yake yote, all its mighty powers by all means, by hooks and crooks kuyakomboa majimbo haya matatu ya Kanda ya Ziwa, na naomba mshishangae, kama ili kujiokoa, CCM inaweza kabisa kutafuta mgombea wa urais kutoka kanda hii ya Ziwa ili kujiokoa kwa kuwahonga watu wa kanda ya Ziwa kwa hongo kubwa kabisa ya mgombea urais, hiyo watu kama John Pombe Magufuli, Andrew Chenge, Laurent Masha, Ngeleja, Kitwanga, are men to watch very closely, hata kama mgombea huyo atakuwa hana sifa za kutosha kuwa rais bora, kwa CCM iko tayari kutupatia bora rais as long as atatoka Kanda ya Ziwa kuliko kuanguka huku inajiangalia!, kwa CCM kinachotakiwa ni ushindi na sio sifa za mgombea!, the end justifies the means.

Mwelekeo huu ni uthibitisho kuwa ule ukombozi wa pili wa kweli wa Mtanzania, sio ndoto tena, ni kitu ambacho kinawezekana kabisa kutokea kama upinzani utajitambua kwa kushikilia kwa makini kile kilicho mkononi na kuongeza juhudi za kuimililki kanda ya Ziwa, hivyo vita kuu ya kisiasa nchini Tanzania kuelekea 2015 ni nani ataimiliki Kanda ya Ziwa. Chadema ikifanikiwa, CCM inapigwa chini, ila CCM ikifanikiwa kuikomboa Kanda ya Ziwa, then 2015 ni CCM tena, na kitakacho fuatia kwa CCM ya 2015 ni kuikomboa Kanda ya Kaskazini na kusema ukweli hii ndio itakuwa kazi ngumu kweli kweli, ila kama itatumika ile 'universal language', kuna msemo "hakuna mkate mgumu mbele ya chai", mkate hata uwe mgumu vipi ukiuchovya ndani ya chai, unalainika!

Tuache Siasa za Ukanda na Ukabila, au Tuzidumishe Ili Mtu wa Kanda/Kabila Yetu Ndie Ashinde?.
Natoa mwito kwa Watanzania wenye mapenzi mema na nchi yetu, tusiendekeze hizi siasa za Ukanda, zitajenga chuki za kukichukia chama fulani bila sababu za msingi ya chuki hiyo, au kukipenda na kikishabikia chama fulani kwa upenzi tuu, matokeo ya mwisho ya siasa hizi ni kujengeana chuki zisizo na sababu!. Tupingane bila kupigana, tutofautiane kisiasa bila kuchukiana bali tupingane kwa hoja huku tukipendana!.

Hata mimi uchaguzi wa Arumeru, nilisimama na Sioi, tumekutana na Nasari pale Bungeni Dodoma, tumekumbatiana, na kiukweli kutoka moyoni mwangu, sina chuki na Nasari, namkubali sana tuu kwa dhati na kupongeza kwa ushindi, huku nikiendelea kushikamana na Sioi kwa sababu ni rafiki!.

Wito Kwa Watu wa Kanda ya Kaskazini
Wito wangu kwa nyie watu wa Kanda ya Kaskazini, Kanda yenu ndio imependelewa sana, inaongoza kwa mashule na wasomi, inaongoza kwa mahospitali!, KCMC, Mawenzi, Kibongoto, Mt. Meru, Seliani, Dareda, etc, Inaongoza kwa vivutio vya utalii, Mt. Kilimanjaro, Mt. Meru, Serengeti, Ngorongoro, Seronera, Manyara, Inaongoza kwa barabara za lami hadi vijijini, inaongoza kwa umeme vijijini, inaongoza kwa maendeleo, inaongoza kwa kutoa wanawake wife material, ukioa mchagga umeoa maendeleo, hivyo msiichukie hivyo CCM, kwani pamoja na mabaya yake yote ya CCM, kulea rushwa na ufisadi na kutuletea umasikini na kulea ujinga kwa kuutumia kama mtaji wake wa ushindi, pia kuna mema na mazuri yake mengi ambayo CCM imelifanyia taifa hili ikiwemo kutuletea maendeleo japo kiduchu, lakini pia imetuletea hazina ya amani na utulivu ambazo ni tunu kubwa kuliko maendeleo, hivyo tuichukie CCM kwa mabaya yake na kupenda kwa mema na mazuri yake!.

Wito Kwa Wa Kanda ya Ziwa.
Tusikubali kutumiwa kama ngazi ya wengine kupandia kisiasa, kwa vile na mimi ni mtu wa Kanda hii na sisi ndio determinant ya nani anashinda na kukikalia kile kiti cha ikulu yetu, tusikubali kuendelea kutumika tuu kama ngazi kwa wengine kupandia, au kuendelea kuwa na upendo wa mshumaa kumulikia wengine huku kwetu kunateketea, Kanda hii ndio Kanda yenye watu wengi, ndio Kanda yenye mijitu yenye nguvu inayokula na kushiba, ndio Kanda tajiri kuliko Kanda zote, ndio yenye madini ya dhahabu na almasi, ndio wenye Ziwa Victoria lenye samaki watamu Sato, tusikubali kutumiwa kama dodoki kuwasafishia wengine au dekio baada ya deki linatupwa kule, sisi tuna kila aina ya utajiri lakini very unfortunately watu wetu ni masikini wa kutupwa!. Angalia wenzetu wa Kaskazini mbona wameweza kulibwaga hili lidubwana na wanapata maendeleo, na sisi tuamue kulibwaga unless kama 2015 atakuwa ni mmoja wetu!.

Namalizia kwa kusisitiza, huu ni mtazamo tuu!

Wasalaam.

Paskali
Sasa Chadema ndio wanaamka kujua nguvu ielekezwe wapi, huu ni mwanzo mzuri!, tatizo la tonge hilo, waliolishika tonge mdomoni wanajua, jee watakubali kunyang'anywa tonge mdomoni?
P.
 
Najaribu kufikiri na kuwaza kwanini Chadema inaanzia mikutano yake Mwanza? Kwanini siyo makao makuu ya nchi Dodoma? Kwanini siyo Dar Mbako viongozi wengi Wa Chadema wanaishi? Kwanini siyo Moshi Arusha Mbako mawazo ya kuzaliwa Chadema yalianzia.swali kwanini iwe Mwanza? Aliye majibu anijibu naomba.
Endelea kujiuliza ni tafakuri nzuri
 
Najaribu kufikiri na kuwaza kwanini Chadema inaanzia mikutano yake Mwanza? Kwanini siyo makao makuu ya nchi Dodoma? Kwanini siyo Dar Mbako viongozi wengi Wa Chadema wanaishi? Kwanini siyo Moshi Arusha Mbako mawazo ya kuzaliwa Chadema yalianzia.swali kwanini iwe Mwanza? Aliye majibu anijibu naomba.
FB_IMG_1673884194538.jpg
 
Sababu ni hii....


Kwa kweli nawapongeza sana kuanzia Mwanza, kwasababu sasa hatimaye Chadema imejitambua na kujua kanda determinant za ushindi kwa uchaguzi wa urais Tanzania ni kanda gani, hivyo wameanzia hapa.
Ushauri huu ulitolewa siku nyingi nyuma!. Mwaka 2010 nilipandisha bandiko hili, CCM Imechokwa, CHADEMA Haijajipanga! humo nikasema

Mwaka 2012, nikapandisha uzi huu
Mtazamo: Kanda ya Kaskazini, CCM imechokwa mpaka basi! humo nilisema

Sasa Chadema ndio wanaamka kujua nguvu ielekezwe wapi, huu ni mwanzo mzuri!, tatizo la tonge hilo, waliolishika tonge mdomoni wanajua, jee watakubali kunyang'anywa tonge mdomoni?
P.
Kanda determinant ya ushindi kwani Tanzania kuna uchaguzi, au kuna maonesho ya ujinga wa mtu mweusi kwenye box la kura? Uchaguzi upo Kenya boss.
 
Najaribu kufikiri na kuwaza kwanini Chadema inaanzia mikutano yake Mwanza? Kwanini siyo makao makuu ya nchi Dodoma? Kwanini siyo Dar Mbako viongozi wengi Wa Chadema wanaishi? Kwanini siyo Moshi Arusha Mbako mawazo ya kuzaliwa Chadema yalianzia.swali kwanini iwe Mwanza? Aliye majibu anijibu naomba.

Kwa sababu ndio jiji la pili kwa ukubwa na ni eneo ambalo CHADEMA waliwahi kulicontrol huko nyuma. Kwa kuchukua majimbo mawili na Manispaa ya nyamagana kabla CCM haijaanzisha jiji.
 
Sababu wasukuma ni kama ng'ombe wakiambiwa hivi wanakubali kesho wakiambiwa vile wanakubali. Awamu ya Magufuli walikuwa supporters wa CCM sasa Chadema wanaenda kuwalubuni fasta watageuka.

Jiji la mwanza ni mvhanganyiko sio wasukuma wote. Kuna kipindi majimbo yote yaliongozwa na wasio wasukuma kipindi Cha CHADEMA.
 
Kanda determinant ya ushindi kwani Tanzania kuna uchaguzi, au kuna maonesho ya ujinga wa mtu mweusi kwenye box la kura? Uchaguzi upo Kenya boss.
Hili la kufanya igizo la uchaguzi, tumelizungumza sana humu https://www.jamiiforums.com/threads...na-haja-kufanya-uchaguzi-wa-rais-2020.980346/ nilisema
Wanabodi.
Kwa maoni yangu, uchaguzi wa 2020, utakuwa sio uchaguzi bali utakuwa ni igizo tuu la uchaguzi, sasa badala ya kufanya igizo la uchaguzi , si ni bora tumwache tu Magufuli aendelee mpaka pale tutakaapoona tumetosheka?, na badala yake hizo fedha za uchaguzi zikaelekezwa kwenye maendeleo ?

10. Na baada ya katiba kukanyagwa, kwa mikutano ya siasa kuzuiwa, jee kuna ubaya wowote kama wapinzani wa Tanzania mkiamua kwa kauli moja msisimamishe tena mgombea urais, haswa kwa kuzingatia the playing field is not level, na badala yake CCM tuu ndio iwe pekee inatoa mgombea urais siku zote kufuatia long eksipirience ya uzoefu wa muda mrefu wa CCM kutoa rais wa JMT tangu nchi hii imepata uhuru, ambaye siku zote huchaguliwa kwa ushindi wa kishindo kwenye uchaguzi huru na wa haki?

11. Na kufuatia somo la demokrasia ya Kiafrika, na mfano hai wa matokeo ya urais wa Zanzibar, na kilichofanyika kwenye urais wa JMT, kweli wapinzani makini bado kweli watahitaji kusimamisha mgombea urais wa kushindana na mgombea wa chama dola, CCM, kwa Tume hii hii, na mazingira haya haya ukategemea kuna ushindani?, yaani by now tumeishajua mgombea wa CCM kwa 2020 ni Magufuli, bado kuna chama kiko tayari kumteua mgombea wake kushindana na Magufuli ambaye ni a sitting president, huku kutakuwa ni kugombea urais au kugombea ili kujifurahisha tuu?, ni kama kugombea kisu cha makali kuwili huku mmoja ameshika mpini, wengine kwenye makali kuwili, unategemea nini?, au hata ikitokea Mungu akafanya muujiza, huyo mgombea wa upinzani akashinda kwa muujiza wa Mungu, jee atatangazwa?.

Kwa maoni yangu, 2020 hakutakuwa na uchaguzi wa rais 2020, kutakuwa tuu na igizo la uchaguzi, na kwenye ubunge na udiwani , kwa udikiteta huu, sijui kama kuna mpinzani atatoka!, uchaguzi wa 2020 itakuwa ni uchaguzi wa CCM only and only CCM!. Uchaguzi mwingine wa rais na uchaguzi wa vyama vingi ni uchaguzi wa 2025 only if ...(Mungu hatafanya yake hapa katikati)

Hayo ni maswali tu nimeanza kujiuliza aloud.

Je, wewe una maoni gani kuhusu hoja zangu hizi?

Paskali
Hivyo sasa uchaguzi wa kweli wa rais ni 2030 https://www.jamiiforums.com/threads...ga-karibu-wote-watakuwa-wamemalizika.1401652/
P
 
Hili la kufanya igizo la uchaguzi, tumelizungumza sana humu https://www.jamiiforums.com/threads...na-haja-kufanya-uchaguzi-wa-rais-2020.980346/ nilisema

Hivyo sasa uchaguzi wa kweli wa rais ni 2030
P

Hata 2030 kwa katiba hii, bado utakuwa upuuzi kama upuuzi mwingine. Machafuko tu ndio yatarejesha chaguzi za kweli hapa Tanzania.
 
Hata 2030 kwa katiba hii, bado utakuwa upuuzi kama upuuzi mwingine. Machafuko tu ndio yatarejesha chaguzi za kweli hapa Tanzania.
Duh...!, kama hii ndio misimamo, basi tuna kazi kubwa mbele yetu!. Yaani una anticipates machafuko?!. Naomba endelea to anticipate that kimya kimya, ukihamasisha ni uchochezi!.

P
 
Back
Top Bottom