Kwanini CHADEMA mmetunga na mnasambaza uzushi wa ukabila wa Hayati Magufuli?

Mwenye ukweli ndiye huyo Mbowe kwanini humuulizi unachafua page bure humu?
 
Daaah wakati mwingine tuwe tunabishana kwa sababu maanake unalazimisha vitu ili mradi tu kutaki kuamini njenya kile.unachoamini. Kwanza Wasubi asili yao ni wakazi wa Biharamulo na sii Wilaya nzima kama unavyochukuliwa.

Na Wazinza waliishi kando ya ziwa vijiji vya Chato kuelekea Geita ambayo iko mbali kabisa na ziwa. Kwa hiyo tuweke vitu sawa hapa kuwa kuna Chato mji na Chato wilaya. Kuna Geita Mji na Geita Mkoa. Huu mkoa wa Geita umechukua sehemu za Mwanza, Shinyanga na Kagera hivyo Wasukuma wapo kutokana na kiografia ya mikoa ilounda Geita.

Na Hata Mwanza hutasema ni Mkoa wa Wasukuma maana kumejaa watu wa Makabila tofauti ktk maeneo madogo sana wengine wahamiaji japokuwa Kabila kubwa linajulikana. Aidha chukulia Mara inajulikana kama Mkoa wa Wajita lkn kuna makabila mengi inategemea na eneo tunalozungumzia.

Chato sii ya Wasukuma, hata wao ni wahamiaji, Wasubi na Wazinza ni majirani wote waliishi Wilaya ya Biharamulo katika.maeneo tofauti. Hizi habari za Wasukuma gang sijui Sukumaland ni Siasa za Ukanda ziloanzishwa na Chadema na hatari yake tunaiona sasa hivi.

Na pengine hii ndio hofu alokuwa nayo Nyerere juu ya Wakaskazini maanake kizazi hiki wamerithi fikra za wazee wao kuhofia yasokuwepo. Kuna Usemi usemao - Who ever steal you past control your future. Kuna watu wanahofia kupoteza Ukabila wao maana Tanzania hatuna Ukabila labda kuna Prejudice!
 
Kampeni za Magufuli alisema wazi yeye sii Mwanasiasa, Maendeleo hayana Chama, hayana Kabila wala dini.[/QUOTE]

Na wewe unaamini kabisa kuwa JPM alimaanisha hayo maneno? Kwa nini wakati wa kampeni alikuwa anasema wasipomchagua mtu wa CCM hatajenga barabara katika hilo jimbo? Hatapeleka maji na huduma nyingine kama afya etc.

Kwa nini alibomoa nyumba Kimara na akazuia nyumba zisibomolewe Mwanza kwamba hao ni wapiga kura wake??

Kwa nini alipendelea kujenga miundombinu mbalimbali kijijini kwake Chato?? Kulikuwa na umuhimu wa kujenga uwanja wa ndege Chato? Hospital kubwa kama ile? Pamoja na vitu vingine vyote alivyojenga kwa upendeleo. Sidhani kama kuna ndege yoyote imetua kwenye huo uwanja baada ya mazishi yake.
 
Sio asilimia 15 tu,wasukuma mpk sasa wako milioni 21 kwa watu milioni 60,utawakwepaje hao kina ngosha?
Sensa ya lini hii? Usije ukawa umeangalia idadi ya watu kwenye mikoa ya Kanda ya Ziwa Nyanza ukadhani WOTE ni wasukuma. Mfano Mkoa wa Mwanza kuna watu wengi tu kutoka makabila mengine
 
Kanda ya ziwa. Tunasubiri 2025 CHADEMA mje kanda ya ziwa tuwanyooshe
Kanda ya ziwa mmejaa ushamba na ulimbukeni ndio maana msukuma mmoja alipo pewa nchi akadhani yeye yupo juu ya kila kitu lakini mungu akamwambia HAPANA CORONA IPO JUU YAKO na akamnyamazisha hadi sasa.
 
Mkuu kuzungumzia uchaguzi wa 2020 kwa mtu kama wewe ni kujishushia heshima uliyonayo tu.

Ule haukuwa uchaguzi ulikuwa ni ushenzi tu.

Unawezaje kusema fulani kamshinda fulani wakati huyo fulani katangazwa bila kura kuhesabiwa?

Umesema tutumie common sense hivi kwa common sense yako tu uchaguzi wa 2020 ulikuwa wa haki ?
 
Mkuu ulitazama matokeo au unazungumza tu kufurahisha baraza?! Lissu tena heee! hivi bado anazungumziwa humu?
Unless kama unazungumza kishabiki. Magufuli hakuwa na uwezo wa kumshinda Lissu kama uwanja ungekuwa sawa.

Huko Chato kwenyewe alilazimika kukodi watu wa kumpiga mawe Lissu.

Alifunga vyombo vyote vya habari visimtangaze Lissu lakini aliteswa mpaka kuamua kupora uchaguzi ingekuwaje kama Lissu angepata airtime walau theluthi ya airtime aliyopata Magufuli ?
 
Na hakuwa na utu
 
Nadhani uko sahihi ila bahati mbaya huelewi historia ya makabila haya ya kanda ya ziwa. Wakati wa ukoloni eneo ambalo lilijulikana kama uzinza ni yale ambayo yalikuwa ni utemi wa Karumo, Buchosa na Busambilo ambayo yalikuwa katika Wilaya ya Geita kabla ya Sengerema kuwa Wilaya hapo mwaka 1975. Ndio maana nikasema wazinza si wenyeji wa asili wa Chato kama unavyotaka kulazimisha. Hiyo Chato ilikuwa ni katika utemi ulioitwa Usubi ambayo ilikuwa wilaya yote ya Biharamulo. Na mpaka wa Biharamulo na Geita ni hapo kwenye mji mdogo wa Katoro ambayo iko Geita na Buselesele (usubi) ambayo iko Biharamulo kabla ya kuzaliwa wilaya ya Chato mwaka mwaka 2002. Nimekwambia Wasukuma na Wazinza walianza kuhamia Usubi(Chato) mwanzoni mwa miaka ya hamsini kwa ajili ya fursa ya kilimo cha pamba na kuanza kuwameza wasubi ambao ni wachache, pamoja na wasukuma kuhamia usubi hata wajita nao wengi walianza kuhamia mwambao huo wa Chato lakini wao hasa ni kwa ajili ya uvuvi. Pamoja na hayo hata huko wilaya ya Biharamulo ya sasa wasukuma wamejaa na kuwafanya wenyeji wa asili (wasubi) kuwa kama visiwa vidogo kwenye bahari kuu (wasukuma). Kwa hiyo narudia kusema kwamba wenyeji wa asili wa Chato siyo wazinza bali wasubi.
 
Na wewe iko siku utakufa.
Kanda ya ziwa mmejaa ushamba na ulimbukeni ndio maana msukuma mmoja alipo pewa nchi akadhani yeye yupo juu ya kila kitu lakini mungu akamwambia HAPANA CORONA IPO JUU YAKO na akamnyamazisha hadi sasa.
 
Mnamkosea sana mwendazake! Kutwa kucha mnalia lia, au mnapinga ile sala inayosema raha ya milele umpe ee Bwana?! Mnamsumbua, mwacheni apumzike!
 
Hivi aliyeanzisha uzushi kuwa CDM ni chama cha kanda ya kaskazini, CUF cha waislamu alipata kukemewa? Aliyesema vyama tofauti na CCM vikishika dola kutakuwa na vita kama Rwanda, Libya au Iraq alikanywa? Je...? Je....?
Ikiwa yale watu waliaminishwa hili linawakera nini au ni kweli?
 
Wakishika dola hao itakuwa hivyo.
 
Kuvunjia nyumba watu walioko Dar,kisha Mwanza akaamuru wasivunjiwe kwa kuwa mdio waliompa kura hiyo tu ni upendeleo wa kiwango cha SGR.
Ni kama ilivyokuwa utaifishaji majumba na viwanda wakati wa Azimio la Arusha au Uhujumu uchumi wa miaka ya themanini achilia mbali yaliyoendelea 2015-2020 yanayofanana na yale ya nyuma...
UNAFIKI MTUPU..
 
Yani akabomolea watu wa kimara bila fidia Ila alipofika mwanza kwenye ubomoaji kupisha ujenzi/upanuzi wa barabara ya furahisha pamoja na upanuzi wa airport akasema msiwasumbue hao no wapiga kura wangu. Sijui kama unaona hii double standard???
 

..pia kulikuwa na UDP ambayo mwenyekiti wake ni John Cheyo " bwana mapesa " chama hicho kilikuwa kinapigwa vita ya kikabila kuwa ni chama cha Wasukuma.

..hizi huwa ni PROPAGANDA za CCM dhidi ya chama chochote kinachoonekana kuwa ni tishio. Lazima chama hicho kichafuliwe kwa kashfa za ukabila au udini.

..kwa hapa Tanzania hakuna chama cha upinzani kinachoweza kuanzisha vita. Wenye uwezo huo ni CCM kwani wao ndio wenye silaha na wameshaonyesha mfano wa wanachoweza kufanya kupitia kundi la " WATU WASIOJULIKANA."

Cc Mkandara
 
Hivi kuna watu huwa wanamsikiliza huyu mfanya biashara ya madanguro? Eti wao huita night clubs! Huyu mwenyekiti wa chadema ndo biashara zake!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…