Kwanini CHADEMA wanadhani Lissu ataleta mabadiliko ili hali kawepo kwenye chama miaka zaidi ya 30?

Tuo Tuo

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2013
Posts
678
Reaction score
1,202
Lissu kushika kijiti watu wamefurahi sana lakini pia CHADEMA wanaona kama ndo watashika nchi vile?

Nini wanadhan Lissu atakibadilisha kama yule mzee asiye na bla bla wala maneno maneno ameshindwa
 
Nashangaa sana mtu mzima au kijana mwenye akili timamu akishabikia CCM, wakati viongozi wake wakiogelea kwenye utajiri wakati yeye mshabiki anaendelea kuwa maskini, mtumishi wa serikali anamiliki timu na anataka kushindana na simba na yanga kwenye usajili, wengine wanashindana kununua Nyumba dubai, alafu wewe kajamba nani uko mpwimbe unashabikia CCM, mimi sina muda na siasa kwa sababu zinaniumiza tu, bora hata CHADEMA wanaongelea mabaya ya hao watendaji wa serikali.
 
Kitu cha kwanza kitendo cha kubadilisha Sura kwenye kiti hayo ni mafanikio tosha.

Vingine atabadilisha taratibu kwa sababu kama ni mti basi mzizi umekita chini kabisa. Miaka 20 sio mchezo.
 
Ili ufanye jambo ndani ya chama,kushika nafasi ya juu kabisa ni mhimu,utatekelezaje wakati huko chini!?,, mbona hiyo inaeleweka tu
 
jitahidi usiwe mtu wa hisia!!
changia maada afu endelea kushangaa kimoyo moyo
 
Ili ufanye jambo ndani ya chama,kushika nafasi ya juu kabisa ni mhimu,utatekelezaje wakati huko chini!?,, mbona hiyo inaeleweka tu
Lisu ni muongeaji siyo mtendaji kuna tofauti ya hawa watu wawili
 
Kitu cha kwanza kitendo cha kubadilisha Sura kwenye kiti hayo ni mafanikio tosha.

Vingine atabadilisha taratibu kwa sababu kama ni mti basi mzizi umekita chini kabisa. Miaka 20 sio mchezo.
hapa kuna point
 
Lisu kushika kijiti watu wamefurahi sana lakini pia chadema wanaona kama ndo watashika nchi vile??

Nini wanadhan Lisu atakibadilisha kama yule mzee asiye na bla bla wala maneno maneno ameshindwa
WASIRA
 
kwanza hana miaka 20, pili nafas aliyokuwq nayo asingeweza maana alikuwa na mtu juu yake
Rais asamia ataifanyia nn nchi wakati alikuwepo 15+ years ccm? Kipi kipya ambacho marais wenzie hawakufanya
 
Lisu kushika kijiti watu wamefurahi sana lakini pia chadema wanaona kama ndo watashika nchi vile??

Nini wanadhan Lisu atakibadilisha kama yule mzee asiye na bla bla wala maneno maneno ameshindwa
Ni euphoria tu. Mfupa uliomshinda Mbowe Lissu atauweza? Atafulia soon
 
Lisu ni muongeaji siyo mtendaji kuna tofauti ya hawa watu wawili
Ni angekuwa si mtendaji assinge kitetea chama kwenye kesi mbali mbali, mara ngapi ameenda head to head na serikali almost apoteze uhai?

Huna logic wala fact kwenye jibu lako
 
Lisu kushika kijiti watu wamefurahi sana lakini pia chadema wanaona kama ndo watashika nchi vile??

Nini wanadhan Lisu atakibadilisha kama yule mzee asiye na bla bla wala maneno maneno ameshindwa
Kwa nilivyowasikia wengi inaonyesha watu wameichoka tawala ya 6 na walihitaji mtu wa kuleta mshikemshike na tena amekuwa kilwleni basi wanaamini moto utakuwa mkali watawala wa ndioo wanabadilisha mambo
 
Lisu kushika kijiti watu wamefurahi sana lakini pia chadema wanaona kama ndo watashika nchi vile??

Nini wanadhan Lisu atakibadilisha kama yule mzee asiye na bla bla wala maneno maneno ameshindwa
Nadhani mambo ya CHADEMA tuwaachie wenyewe maana wanajua wanachokifanya
 
Lissu kushika kijiti watu wamefurahi sana lakini pia CHADEMA wanaona kama ndo watashika nchi vile?

Nini wanadhan Lissu atakibadilisha kama yule mzee asiye na bla bla wala maneno maneno ameshindwa
akili mbovu tu za akina lema et al
 
Nadhani mambo ya CHADEMA tuwaachie wenyewe maana wanajua wanachokifanya
Ni sawa ila ngoja nijaribu.
Wafuasi wengi wa CDM ni vijana na vijana wengi ni wapenzi wa Siasa za kianaharakati kama za Mdude Nyangali. Siasa za Hangalehangale. Siasa za kupinga kila kitu CCM inafanya. Walikuwa wapo sawa na Mbowe hadi ujio wa Lowassa ambaye alipenda CDM ibadilike ili kuacha siasa za kianaharakati. Kwa bahati mbaya, Mbowe alikubaliana na Lowassa (na pengine kutokana na umri), akabadili mwenendo wa siasa zake kutoka za kianaharakati. Kitendo cha kumpatia nishani Samia kiliwaudhi wengi. Matamko ya Mbowe kusifia Samia yalivunja nguvu vijana wengi.

Kwa bahati nzuri, akaibuka Tundu Lissu ambaye kwake siasa ni uanaharakati. Hivyo wakampata mwokozi wao. Na juzi alipotamka Tanganyika, akatu win na sisi ambao siyo CDM kutokana na makosa anayoyafanya Samia ya kuegemea upande wa kwao.

Tunategemea sasa kutakucha na CCM ambayo ilikuwa inasinzia kwa kumlambisha asali Mbowe, itaamka na kuanza kutambua kuwa kila siku si jumapili. Hivyo tuna matumaini makubwa na Lissu. Kila chama kinatakiwa kiwe na ideology, mbinu na mikakati tofauti na chenzake. Vyama vyote vikiwa sawa, hakuna vyama vingi tena. Lazima vyama vijitofautishe na chama tawala, ambapo wananchi wa kawaida waone utofauti kwa maneno na vitendo la sivyo vitakuwa CCM (B)
 
Alishafika njia panda ya kwenda kwa wafu, so nafikiri hana cha kumtisha,
 
Back
Top Bottom