Kwanini Chato iwe Mkoa kutoka kwenye Mkoa mchanga wa Geita ulioundwa 2012?

[emoji106][emoji106][emoji106]
 
Ndo maana nasema wengi hapa wanachangia hoja kisiasa.


Mkoa utengenezwe lakin makao makuu ya wilaya yawe nyakanazi au biharamulo.
Kweli kabisa mkuu. Japo kuna baadhi watasema tunaionea gere chato, lakini nimejaribu kuongea na baadhi ya wenyeji wa Chato wamesema hata wao hii haijakaa vyema hapo ni swala la kisiasa
 
Morogoro wasubiri mpaka wapate Rais mzaliwa wa huko ndio igawanywe! Kutoka Moro mjini hadi Malinyi na Mahenge ni mbali kwelikweli! Jiwe angekuwepo hata makao makuu ya nchi yangepelekwa Chato, alikuwa mbinafsi sana yule mzee!
 
Ni ujinga kufikiria kukiwa na mikoa mingi ndiyo maendeleo.
Inawezekana kufikiri kwa busara kwenye jambo la kijinga, au kuwaza kijinga kwenye fikra zenye busara.
Tafsiri ya kusogeza huduma karibu na matokeo yake ya muda mrefu ni nini.
 
We ndo umechanyikiwa kwa sababu hujapenda Lakin mantiki ya mkoa mpya ni kumega mikoa ya geita, Kagera na Kigoma ili kusogeza huduma. Hivi mkoa ungeitwa nyakanazi na hizo wilaya za chato zimo bado ungelalamika bado??? Kinachoaumbua hapa naona ni jina chato
 
Inawezekana kufikiri kwa busara kwenye jambo la kijinga, au kuwaza kijinga kwenye fikra zenye busara.
Tafsiri ya kusogeza huduma karibu na matokeo yake ya muda mrefu ni nini.
Ni ujinga kufikiria kuwa ili kuwa na shule nzuri, lazima kuongeza mkoa, ili kuwa na huduma nzuri za afya, lazima uwe mkoa, ili kuwa na usalama mzuri ni lazima uwe mkoa. Ni ujinga wa hali ya juu.

Hivi ni nchi gani ina huduma nzuri kwa sababu ina mikoa mingi? Tuna viongozi ambao, wana akili kibaba.
 
Yaani mkuu umeandika kwa jaziba, hapa lengo si kuifanya chato kuwa karibu na huduma bali hizi wilaya zinazoizunguka chato kama biharamulo, ngara na kakonko. Sasa mkisikia choto akili zote zinaconcentrate hapo, ingawa kwa usahihi kabisa ilitakiwa makao yawe nyakanazi
 
Sina shida na jina, na nadhani kila mwenye akili timamu ndivto alivyo. Tatizo kubwa ni kuwa hakuna sababu ya msingi.
 
Wewe ulimpenda, endelea kumenda? I hate him and will hate him forever. Kila mtu ashinde mechi zake. This Mwendazake shot Ben Saanane by his own pistol while under torture. Kisa Ben Saanane anataka Mwendazake athibitise PhD yake kama siyo ya kunakili kwa Dr Y Philip

He was a DEVIL!! Alimtuma Paul Makonda na kundi la WASIOJULIKANA wakammuue Tundu Lissu na akapanga akazikwe Ikungi chap chap bila kuletwa kuagwa DSM.

Yeye kafoji PhD halafu anawatoa kazini waliofoji Certificate za Form IV tu. Akapotezea Forgery ya kwake, ya Makonda, Palamagamba, Kigwangalla na Mwigulu. Mungu hapendi double standards, kama vipi angewapotezea wote.

Alidhani kuwa Rais wa Tz ni sawa na kuwa Mungu. Takataka mkubwa yule Mungu akamuonyesha kuwa wewe si lolote si chochote pamoja na ulinzi wa ma helicopter, mabunduki na mitambo ya internet akafa kwa COVID19.
 
Muundo wa mikoa na wilya hutegemea idadi ya watu; haitegemei historia au ukubwa wa eneo! Halafu maamuzi haya yanafanyika wakati Magufuli hayupo tena, je yangefanyika akiwa hai ingekuwaje?
 
Ni uwendawazimu na ujinga wa hali ya juu kufikiria kuwa mahali pakiwa na watu wengi lazima pawe mkoa.

Chato haikidhi hata kigezo kimojakuwamkoa. RCC members nadhani wote ni low IQ.
Kwani umesikia kuwa wilaya ya chato ndo itakuwa mkoa peke yake???? Population ni kumaanisha wilaya zote zilizounganishwa zimekidhi population
 
Kwani Nyakanazi iko Mkoa wa Kigoma ? Nyakanazi iko wilaya ya Biharamulo Mkoa wa Kagera, kwanini uwaze kuunganisha na Kakonko na Kibobdo ?
Mkuu mbona unajichanganya???? Hakuna sheria inayosema mkoa uundwe kutoka mkoa mmoja. Mbona geita ilimegwa kutoka Mwanza na Kagera??
 
Sasa mkuu unachopinga ni kuundwa kwa mkoa au ni mkoa kuwa chato??? Chato ni jina na eneo tu lakini manufaa ni kwa ajili ya hizi wilaya zote zitakazounda mkoa huu
 
Tueleze ubora wa Nyakanazi kuzidi Chato ambayo pia iko kwenye mwambao wa Ziwa Victoria
Sizungumzii ubora kwa maana ya maendeleo bali nimeangalia urahisi wa kufikika kwa wilaya zote ambazo zimependekezwa maana lengo ni kurahisisha huduma.
 
Morogoro wasubiri mpaka wapate Rais mzaliwa wa huko ndio igawanywe! Kutoka Moro mjini hadi Malinyi na Mahenge ni mbali kwelikweli! Jiwe angekuwepo hata makao makuu ya nchi yangepelekwa Chato, alikuwa mbinafsi sana yule mzee!
Kuna mtu alishawahi kuniambia kuna sehemu ndani ya mkoa wa morogoro kutoka sehemu moja mpaka nyingine inafika mpk km 600 hii ni kweli?

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
 
Divide and role method ile ya wakoloni ndio naiyelewa Leo
Chato Hata haipendezei kuwa mkoa
 
Hivi mwananchi wa kijiji cha Mafisa huko Kilindi anapoteza gharama kiasi gani, muda na usumbufu kufuata huduma ofisi za mkoa Tanga?
Na endapo mkoa mkubwa kama Tanga, Morogoro na mingine ikigawanywa wananchi wapate huduma karibu wewe unayejataa utaoungukiwa nini?
Miundo mbinu itajengwa, watu wataziona fursa za biashara watafanya, ajira zitaongezeka pia nk.
Yapo mengi na unayajua lakini ukiwa na fikra za kupinga ni lazima upinge.

Ukosefu waa huduma bora za afya, elimu nk. ni udhaifu wa serikali katika usimamizi pamoja na sera mbovu ikiwemo kuchagua viongozi kwa kuwakomoa wengine bila kujali weledi.

Kasoro nayoiona huwa ipo kwenye ujenzi wa makao makuu ya hii mikoa mipya, ubinafsi na siasa vinawekwa mbele.
Ungeongelea hili ningekuunga mkono.
 
Mi nashangaa mtu anauliza swali eti chato ina population gani ya kuwa mkoa, hivi anaeunda mkoa ni chato au ni wilaya zote tano zilizopendekezwa??? Swali lao inabidi liwe general sio ku-deal na chato tu
 
Absolutely Rubbish, kwa nin chato iwe mkoa. wakati halimashauri yenyewe haijitoshelezi kimapato .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…