Andiko zuri sana.
Kama hawatakusikiliza basi waache lakini kiburi kitawaumbua kama kinavyowaumbua kwa kuanzisha mikoa waliyokurupuka.
Wakati wanataka kuanzisha mkoa wa Katavi walipendekeza Wilaya ya Kaliua iende mkoa wa Katavi, Mungu mwema wale Wanyamwezi waligoma katakata na wengi tuliwasapoti. Kutoka Kaliua hadi Mpanda hakuna barabara ya moja kwa moja kuna reli tu. Ukiwa na gari mpaka urudi Tabora/Sikonge then Mpanda. Lakini pia wakasema wanaenzi utamaduni na asili yao inayowanasibisha na Mtemi Mirambo. Leo unawachukua Waha wa Kakonko na kuwafurusha kwenda Chato? Wakikubali nitajua Mha kabadilika.
Bora hata wangeanzisha mkoa wa Kahama, au wangeigawa Morogoro mara mbili maana ukubwa wake unatisha.