Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Tatizo wanasiasa wakipania kupata kitu chao ni rahisi sana kuwatwisha mzigo wananchi bila kusikiliza hoja zao. Vikao vya RCC mkoa wa Geita vina mamlaka ya kuamua kuumega mkoa mwingine?..Ni sharti waombe na wakubaliwe kwanza!!.. Kwani vikao vya RCC mkoa wa Kigoma vilikubali Kakonko imegwe kwa kuwa iko mbali na makao makuu ya mkoa?..!. Wakoloni waliigawa Afrika kwa mtindo huo na matokeo yake tunayaona hadi leo.Binafsi na mimi sipendezwi na makao ya mkoa kuwa chato, nyakanazi ndo pazuri kabisa lakini kama imetokea pakawa chato waache kakonko wajumuishwe maana ni afadhali kuliko kwenda Kigoma
Hata mimi nashangaa ngoja tuone hii kitu wanavyo fanya.Kama kuna kiongozi atabariki Chato uwe Mkoa kwa kusapoti uwendawazimu wa Magufuli aliotufanyia kwa miaka 5 basi itabidi tukampime akili.
Atakuwa mgonjwa kuliko alivyokuwa Kichaa tuliyemfukia March 27, 2012 pale kijijini Chato
Shukurani sana mkuu sasa kazi iwe kwao sisi tusubiri kama watatuelewa au Lah!!Andiko zuri sana.
Kama hawatakusikiliza basi waache lakini kiburi kitawaumbua kama kinavyowaumbua kwa kuanzisha mikoa waliyokurupuka.
Wakati wanataka kuanzisha mkoa wa Katavi walipendekeza Wilaya ya Kaliua iende mkoa wa Katavi, Mungu mwema wale Wanyamwezi waligoma katakata na wengi tuliwasapoti. Kutoka Kaliua hadi Mpanda hakuna barabara ya moja kwa moja kuna reli tu. Ukiwa na gari mpaka urudi Tabora/Sikonge then Mpanda. Lakini pia wakasema wanaenzi utamaduni na asili yao inayowanasibisha na Mtemi Mirambo. Leo unawachukua Waha wa Kakonko na kuwafurusha kwenda Chato? Wakikubali nitajua Mha kabadilika.
Bora hata wangeanzisha mkoa wa Kahama, au wangeigawa Morogoro mara mbili maana ukubwa wake unatisha.
Hata kama ni population hivi chato ya kuifikia Moro? Hata kama ni issue ya mapato bado tu.Mkoa hautengwi kwa kutazama ukubwa ma ardhi. Ingekua ukubwa wa ardhi Dar Es Salaam ingejua wilaya tu.
Mkuu wa mkoa anakama siku 10 mkoa hapo ila anajifanya kujua mambo.Halafu hao huyo mkuu wa mkoa wa Geita anatoa mapendekezo hadi ya Kigoma ,Kagera na Mwanza kama nani? Yeye ajiongelee ya Geita kuhusu kuitohoa Chato, na Busanda sijui Mbogwe, ya Kigoma,Kagera na Mwanza awaachie RCC husika. Je kama nawao wakizikatalia wilaya zao kama wao geita walivozikatalia zao na wamekataa hadi kutohoa kata kuunda wilaya ya Katoro/Buselesele.
Tofautisha mkuu wa mkoa na ofisi ya mkuu wa mkoaMkuu wa mkoa anakama siku 10 mkoa hapo ila anajifanya kujua mambo.
Ngoja tusubiri akina Msukuma waliongelee hili
Kutoka Kakonko(wilaya mpya) hadi Kigoma ni kilomita 284.2 wakati kutoka Kibondo(wilaya kongwe) kwenda Kigoma ni kilomita 238.0 Kuna tofauti ya kilomita 46.2 kati ya Kakonko na Kibondo zikihudumiwa kutoka mkoa wa kigoma. Suruhisho ili kuunda mkoa wa Chato ni kumega huko huko Geita bila kuingilia mkoa wa Kigoma. Kama Kakonko na Kibondo wakiamua kwenye RCC Yao, suruhisho ni kuunganisha Ngara na nyakanazi kufanya mkoa mpya wa Nyakanazi au Kibondo.....Siyo hii habari ya mkoa wa Chato.